Angalieni wizi huu-huu ni uozo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalieni wizi huu-huu ni uozo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Apr 19, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  huitaji kuwa na PhD kutoka China,elimu ya shule za kata inatosha kulielewa hili

  "tunadaiwa tilioni 14 deni linakuwa kwa 36% wakati huo tunaelezwa uchumi unakuwa kwa 6%"​
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ni wakati muafaka wa kubadilisha serekali sasa CCM imeshindwa kazi labda kama kipofu tu ndio haoni.
   
 3. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Tunaibiwa nini? mbona mie sioni? tuseme nini sasa?
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Tumeibiwa nini tena ?
   
 5. T

  Tewe JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Mods ondoeni hii post inajaza wingi tu
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Pamoja na wizi kama huo, bado watu wanajihalalisha kuwa ndio viongozi bora kupata kutokea Tanzania. Hii mizaha itaisha lini? Hatuogopi kuja kuchekwa?
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mkuu

  tunahitaji kupambana,hii nchi wajukuu wetu hawata tuelewa kabisa
   
 8. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Eng. Mtolera,
  Nchi hii tulishauzwa kwa deni hilo tulichobakiza ni kuendelea kuwatumikia hawa mabwana zetu wanaotuhonga Neti za mbu na kondom vitu vya kutufanya tuzidi kuwa wazinzi na kuongeza idadi ya watumwa. Fikiria kipato cha mtz kwa siku anaingiza shilingi ngapi ili imuwezeshe kulipa deni hilo japo kwa kundunduliza? Na mkulu naye angejaribu kupunga safari nje japo mara nne kwa mwaka na safari zingine zikapunguza makali ya deni hili ambalo mpaka vitukuu vilivyoko kiunoni vitatoka vikiwa na madeni.
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nakumbuka,wakati mkapa anaondoka alisema amepunguza deni kwa kiwango kikubwa sana mpaka ikawa rahisi kukopesheka,sasa nini kimetokea hadi deni lipande kwa kiasi hicho?

  wameshachukua kigamboni watanunua na barabara zetu
   
 10. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Na mpaka ardhi tuliosimamisha nyumba zetu zitakuwa halali yao. Ukuwaji wa uchumi ukoje jamani ni kwenye makaratasi tu? na maisha yatu walau yawe yenye ahueni kila kukicha ni afadhali ya jana!
   
 11. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tunaibiwa nini we huna macho na maskio????Ushaambiwa maisha bora kwa kila Mtanzania lakini tunadaiwa tilioni 14 deni linakuwa kwa 36% wakati huo huo uchumi unakuwa kwa 6% sasa hizi takwimu unaona kuwa ziko sahihi? Huo uchumi unaokuwa kwa nini usitumike kupunguza deni la taifa na kama sio hivo hiyo 6% inayakua inakulia kwenye mifuko ya wajanja basi
   
 12. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tunaibiwa nini we huna macho na maskio????Ushaambiwa maisha bora kwa kila Mtanzania lakini tunadaiwa tilioni 14 deni linakuwa kwa 36% wakati huo huo uchumi unakuwa kwa 6% sasa hizi takwimu unaona kuwa ziko sahihi? Huo uchumi unaokuwa kwa nini usitumike kupunguza deni la taifa na kama sio hivo hiyo 6% inayakua inakulia kwenye mifuko ya wajanja basi
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  hesabu jamani hesabu au hamjui hesabu ni baba mkwe....??????
   
 14. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #14
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imenisikitsha sana, nilitamani nilie wakati mbunge wa CCM viti maalum anakokota hesabu hii jamani???? haya ni maisha bora au bora maisha?
   
 15. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi hii imekuwaje? Mwinyi alipandisha deni hadi hali ikawa inatisha (watu wanasema alifikia mahali pa kutaka kukimbia nchi). Mkapa akalipunguza hadi tukaanza kusahau habari ya nchi kudaiwa. Huyu tena amepandisha deni katika hali ya kutisha kabisa. What does this mean? Hata kama wataingia wapinzani mwaka 2015, bado wanaweza kujikuta kwenye wakati mgumu sana, kwa kuwa watatumia muda wao mwingi kulipa deni la Kikwete. Ndiyo maana mimi huwa nasema hapa ujanja yafanyike mapinduzi, na serikali mpya itangaze kwamba haiyatambui madeni ya awali kwa kuwa inaamini rais aliyetangulia alizitumia hizo pesa kwa shughuli zake binafsi. Ila kama ni kwa kupokezana madaraka kwa hali ya kawaida, ni lawama hii!
   
 16. N

  NFH New Member

  #16
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani hivi14,000,000,000,000 ndio deni au co?
   
 17. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Actually, ukitaka ujue serikali imetufikisha pabaya kiasi gani, fikiria kwamba budget yetu ya mwaka ni kiasi gani, na sasa utaona kwamba ikiwa tuna deni la trilioni 14 linallokua kwa 36% kila mwaka, ina maana tunafikia mahali ambapo budget yetu ni ndogo kuliko ukuzi wa deni la kila mwaka. Na pia ujue kwamba budget yetu ni kubwa sana zaidi ya ya pato la taifa la mwaka.

  Hivyo basi - nchi iko mufilisi kabisaaa, kwenye severe vicious cycle of recession.

  Ingekuwa kampuni ingekabidhiwa kwa mfirishaji. Yaani hapa ndipo unafikia kwamba ujikabdidhi kwa taifa jingine uwe koloni lake. Labda sie tuseme bwana USA, tunakukabidhi nchi na kila kitu kilichomo uamue jinsi ya kutuendesha.

  Kimsingi, inatakiwa serikali ijiuzuru uchaguzi uitishwe upya. Na hili ni la msingi katika katiba mpya, kwamba serikali ya kiongozi yeyote ikiendesha nchi hadi kufikia riba la deni la taifa kwa mwaka ni zaidi ya pato la taifa la mwaka basi serikali hiyo inapaswa kujiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya ambao utatoa nafasi ya miaka mitano kwa serikali mpya kurekebisha hali hiyo.
   
 18. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haya ni matokeo ya safari 350 nje ya nchi ndani ya Utawala wa mzee wa maisha bora kwa mtanzania, twafaaaaaa
   
Loading...