Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia njia mpya ya Wachina kutafuta wachumba!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ldleo, Jan 25, 2010.

 1. l

  ldleo Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Muda mfupi uliopita, "supamaketi maalum ya mapenzi" ilizinduliwa katika mtaa wenye maduka mengi mjini Beijing,. Supamaketi hiyo haiuzi matunda wala vyakula na matumizi ya kila siku, kinachouzwa ni mapenzi tu. Katika supamaketi hiyo, watu wasio na wachumba wanaweza kuchagua watu wanaoona wanawafaa. ​

  Tarehe 9 Novemba "Supamaketi ya mapenzi ya ninakutafuta" iliyoko katika uwanja wa Xihuan mjini Beijing ilizinduliwa. Baada ya kuzinduliwa tu, kazi yake ilifanyika katika hali motomoto. Kila siku watu wengi wasio na wachumba wanakwenda kwenye supamaketi hiyo kuwatafuta na kuwachagua watu wanaowapenda. Katika supamaketi hiyo, data za watu wasio na wachumba zinawekwa katika rafu kwa kufuata utaratibu wa jinsia, umri na mapato, kwa hiyo watu wote wasio na wachumba wanaokwenda kwenye supamaketi hiyo, wanaweza kuchagua watu wanaoona wanawafaa kwa mujibu wa data hizo, kama wakiona watu fulani wanawafaa, basi wanaweza kuwasiliana na watu hao kwa kupitia wafanyakazi wa supamaketi hiyo baada ya kuthibitisha vitambulisho vyao. Mhusika wa supamaketi hiyo Bibi Zhang Ying alifahamisha kuwa, wazo la kuanzisha supamaketi hiyo lilitokana na uzoefu na raslimali zao za kuendesha tovuti ya kutafuta mchumba. Bibi Zhang alisema,
  "Tovuti ya kutafuta mchumba inayoitwa 'ninakutafuta' imeendeshwa kwa miaka mitatu, kwa kupitia uendeshaji wa tovuti hiyo, na kuwasiliana na watu wasio na wachumba, tumegundua kuwa watu hao wanataka kuwa na njia ya moja kwa moja, pia wanataka kupata data husika zinazoaminika zaidi. Kwa hiyo tulifikiri kuzindua supamaketi hiyo. Watu wasio na wachumba wakija wanaweza kuona data hizo zinazoaminika. Wanalokuta ni jukwaa kubwa zaidi kuliko tovuti."
  Katika "supamaketi ya mapenzi", data zote zinathibitishwa, na kila data ina picha ya mtu mhusika asiye na mchumba, kwa hiyo inawapa watu wasio na wachumba urahisi wa kuchagua, na wakiridhika wanaweza kuwasiliana nao mara moja. Supamaketi hiyo inafunguliwa kila siku, na haipumziki hata wakati wa wikiendi na sikukuu, hivyo watu wasio na wachumba wakiwa na wakati, wanaweza kutembelea supamaketi hiyo, huenda watakutana na watu wanaweza kuwapenda. Katika mchakato huo, washauri kuhusu mambo ya ndoa kwenye supamaketi hiyo wanafanya kazi muhimu. Bibi Zhang Ying alisema,
  "Kazi za washauri kuhusu mambo ya ndoa ni kufahamu matakwa ya watu wasio na wachumba, na kuwasaidia kujua matakwa hayo halisi, kazi hii ni muhimu sana, kwa sababu watu wengi wasio na wachumba hawajui matakwa yao halisi, au matakwa yao hayaendani na hali zao."
  Washauri kuhusu mambo ya ndoa wanapaswa kuthibitisha kwanza data husika za watu wasio na wachumba walioandikishwa kwenye supamaketi hiyo, halafu wanaweza kutoa huduma nzuri na mapendekezo kwa watu wasio na wachumba, ili kuwasaidia wakutane na watu wanaowafaa zaidi. Bibi Gao Shan ni mshauri kuhusu mambo ya ndoa, alisema hivi sasa vijana huwa wanakutana na matatizo mengi wakati wa kuchagua watu wanaowapenda, na "supamaketi ya mapenzi" inataka kuwapa watu wasio na wachumba fursa nyingi zaidi na kuwasaidia kuondoa matatizo. Alisema,
  "Watu huona kuwa kutafuta marafiki kupitia mtandao wa internet si jambo halisi, na wanahitaji muda kuwafahamu marafiki hawa kwa undani, labda mpaka mwisho wanakuwa hawajui wanachofahamu kama ni kweli au la, kwa hiyo mchakato huo umesababisha matatizo kadhaa wakati wa kutafuta marafiki. Baadhi ya watu wanawaomba jamaa au marafiki zao wawasaidie kuwatambulisha kwa kujuana na kujulisha mtu fulani, lakini huenda jamaa na marafiki zao hawajui kwa uhalisi ni nini. Hivyo tunawasaidia kuondoa matatizo hayo mawili makubwa, kwanza data zote katika supamaketi yetu zinaaminika, tumekutana na watu hao, na picha zao pia ni za maishani, kwani uaminifu ni jambo la kwanza na la msingi, pili kwa kuwa hapa ni supamaketi, hivyo watu wanaweza kuwachagua wenyewe, wanaochagua ni wanaowapenda." ​
  [​IMG]

  Hivi sasa katika "supamaketi ya mapenzi", kuna watu zaidi ya 500 wanaoweza kuchaguliwa. Ni rahisi kushiriki kwenye supamaketi hiyo, unapaswa kutoa habari yako halisi ya kimsingi, na kutoa Yuan 20 kutengeneza data, halafu data zako zinaweza kuwekwa kwenye rafu. Unaweza kutembelea supamaketi hiyo bila malipo, na kama unaona kuna mtu fulani uliyevutiwa naye, unaweza kumwuliza na kusaidiwa na washauri kuhusu mambo ya ndoa kwenye supamaketi hiyo, na kuna wanaopenda kukusaidia. Kwa upande mmoja, pia unapaswa kutoa Yuan 20 kutengeneza data zako, baada ya kuthibitisha wanaweza kutoa data hizo kwa mtu unayependa kukutana naye; kwa upande mwingine, kama mtu huyo anakubali kukutana nawe, watawasaidia kuwapa njia ya kuwasiliana, au kuwasaida kuchagua muda na sehemu ya kukutana. Supamaketi ikiwasaidia watu wawili kukutana, itatoza Yuan 100. Fedha hizo sio nyingi na data zinaaminika, kwa hiyo supamaketi hiyo inawavutia "wateja" wengi.
  Msichana Zhou Xianyu kutoka Hangzhou amefanya kazi hapa Beijing kwa zaidi ya miaka 10, kwa kuwa hakuwasiliana na watu wengi, hivyo bado hana mchumba. Baada ya kuiona "supamaketi ya mapenzi", alitembelea na kutaka kutafuta mtu anayempenda. Alisema,
  "Kwa kuwa sikuwasiliana na watu wengi, hivyo fursa ya kukutana na mtu ninayeona ananifaa anayefaa sio nyingi, kwa hiyo bado sijakutana na anayefaa. Naona haya kwenda sehemu za kutafuta wachumba. Lakini wazazi wangu wana wasiwasi. Nimetembelea "supamaketi" hiyo kutazama kama kuna mtu anayenifaa. Naona hapa ni salama."
  Mjini Beijing kuna vijana wasio na wachumba kama msichana Zhou. Habari zilizotolewa na shirika la habari la China zinasema, hivi sasa mjini Beijing wasichana zaidi ya laki 5 bado hawana wachumba, na wavulana wasio na wachumba hata ni mara 1.5 kuliko wasichana, na idadi hiyo inaongezeka siku hadi siku. Basi "supamaketi ya mapenzi" inatoa fursa kubwa kwa watu hao, lakini vipi njia hiyo inakubaliwa na watu bado inahitaji muda. Bibi Zhang Ying alisema, "Matumaini yetu ni kuwasaidia wale wanaotaka kutafuta mchumba na kufunga ndoa. Tuna matumaini kuwa siku moja watu wakitaja supamaketi yetu, wanaweza kuisifu na kusema kuwa, data zinazotolewa hapa ni za kuaminika, na watu wasio na wachumba wanaweza kwenda kwenye supamaketi hiyo kutafuta wachumba, naona hayo yametimiza lengo letu la kuanzisha tovuti hiyo."
  (Makala hii inatoka http://swahili.cri.cn/)
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mh dunia inakwisha sasa ikija bongo itapata wateja sana
   
 3. l

  ldleo Member

  #3
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Is it amazing that wachina wengi wanaochapa kazi, hawana wakati wa kutafuta wachumba au kudate, hivyo imekuwa njia mkato, lakini labda siyo nzuri.
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  swaaafi sana, sasa mambo ya kuliana bia na mishikaki kwisha, unaenda market unachukua mzigo, mchezo umeisha! da soko huria limetukomboa, tulikuwa tunahangaika kutongoza weeeeeeeeeeeee tunaliwa pesa na demu anayeyuka!!!!

  jamani wadau tuungane tupate wawekezaji haraka watuwekee haya maduka bongo immediately.

  itabidi nipitie china nikiwa njiani kurudi home niangalie uwezekano wa kuibuka na mchina,

  tehe tehehehe...................
   
 5. D

  Darwin JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Iko Warrant kwamba unayemnunua!!! oops unayempata kama utadumu naye? na ni siku ngapi unaweza kupewa unayemtaka nakumjaribu kwamba anafaa!!? Kama hafai unarudishiwa pesa zako?
   
 6. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dah! hii kali sasa mpaka watu wameanza kuuzwa utu wa mtu sasa umekuwa hauna samani mh!
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hii habari imenifanya nitabasamu tu kisha kubaki na mshangao
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mbona wabongo wanafanya indirectly pale mlimani city
   
 9. l

  ldleo Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuishi kwingi ni kuona mengi, lakini sipendi utamaduni huo wa fastfood!Mapenzi siyo mchezo.
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145

  hii nzuri saana wakuuu inawapa mwanya hata wanawake kufanya choice nzuri na Inakupa Uhuru wakuchagua umpendaye hureeeee chainese ila kutuletea bandia ndo noma
   
 11. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .. I like this...Kweli ndugu yangu maana vi-date na mizinga na uhakika wa mzigo huna...
   
 12. bht

  bht JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kule HEz ni wengi Kuliko Shez, sasa we AK si ni he? hautapata!!!
   
Loading...