Angalia nae huyu hv hawa viongozi wana akili kweli??

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Yaani Tanzania ina viongozi vilaza sana embu angalia video hapo chini baada ya habari hii ndipo utajifunza kitu

Sakata la kashfa ya uuzaji wa rada kwa Tanzania kutoka kampuni ya Uingereza- BAE Systems bado inaendelea, baada ya kampuni hiyo kusita kuilipa serikali ya Tanzania fedha hizo moja kwa moja serikalini na badala yake ilipe asasi za serikali za Uingereza. Kampuni hiyo inadai kutokana na sera zake hairuhusiwi kuilipa serikali na hivyo njia mbadala ni kupitia mashirika hayo.

Kampuni ya BAE imetakiwa kuilipa Tanzania fidia ya paundi milioni 29.5 baada ya kuiuzia Tanzania rada kwa gharama ya paundi milioni 41 za Uingereza wakati bei halisi ilikuwa paundi milioni 12.
Ujumbe wa wabunge watano wakiongozwa na naibu spika wa Tanzania Bw Job Ndugai wamefika nchini Uingereza kuishinikiza kampuni hiyo kuilipa serikali ya Tanzania. Mazungumzo mpaka sasa bado yanaendelea na yanaonekana kuwa na mwelekeo mzuri.
Mwandishi wa BBC Zuhura Yunus amefanya mahojiano na Bw Ndugai kujua zaidi kuhusu suala hilo.


[video]http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2011/06/110624_tz_rada_uingereza.shtml[/video]
 
hii iko humu mkuu toka asubuhi sema heading yake inafanya iwe kama habari ya zamani huko iliko
 
ok maana naona jamaa amejibu pumba sana mpaka nimepatwa na kisilani hv hii serikali inacheza na akili za watu eeeh
hii iko humu mkuu toka asubuhi sema heading yake inafanya iwe kama habari ya zamani huko iliko
 
Eti hatua zitachukuliwa ... lini..? ?? huyu ms""" kaniudhi kweli..

hana info yeyote....
 
ndio hicho na mimi nimemshangaa sana hv inakuwaje hata serikali inawatuma viongozi vilaza kwenda kufuatilia masuala mazito kama haya???sasa kama yeye hajui kitu unategemea atatetea nini au ameenda kutalii???aisee sasa kweli naamini tz ya sasa ni kudesa tu kwa kwenda mbele kweli nimeangalia na kusikiliza nimeumia sana!
Eti hatua zitachukuliwa ... lini..? ?? huyu ms""" kaniudhi kweli..

hana info yeyote....
 
Halafu huyu naambiwa ndiye Naibu Spika na Spika mwenyewe ni Makinda ! Naona watu wanataka kuvuna wasichopanda lakini si ndio sera ya serikali ya CCM ? Kilicho wazi ni kuwa a fool and his money soon part ways ! Come easy, go easy !
 
Na huyu ndiye naibu kiongozi wa moja ya mihimili mitatu ya dola akisaidia na Bi. Makinda. Kweli safari bado ni ndefu jamaa hajui kujenga hoja alichokua nakifanya kwa wazee wa saikolojia wanaita "argumentum ad misericordiam=Appeal to pity"
 
Back
Top Bottom