Mheshimiwa Msigwa hasemi huo uzalishaji uongezwe vipi. Kasema yeye mwenyewe kwamba CCM hawawezi kutatua matatizo maana wao ndio "wametuweka kwenye mess hii, you guys are tired." Sasa suluhisho lake yeye ni nini?
Ameshambulia wazinzi na wanaotembea na wake za watu (shambulizi kwa Mwigulu mwenye sifa hiyo, ambae ndie alisema CHADEMA waombewe) lakini hapo hapo amekosoa majadaliano ya "khanga na ngonjera." Yale yale ya vijembe!
Kwenye theology kuna matundu kwenye hoja zake. Amesema hakuna nadharia ya maombi katika uchumi wala theology na kwamba Mtume Paulo alisema "asiyefanya kazi na asile," sio aombewe. Ni kweli, lakini Kristo Yesu alisema tuige mfano wa ndege wa angani, "ndege wao hawapandi wala hawavuni wala hawahifadhi chochote kwenye ghala lakini Baba wa Mbinguni anawalisha." Kesheni Mkiomba. Kwa hiyo hata Biblia hapa haina majibu.
Amesema serikali haisikilizi ushauri wa ma professa. Ushauri gani? Toa mfano!
Yeye ni mpinzani, hajaja hapa kuisifia serikali, ana wajibu wa kuipinga. Ok. Na CCM wana kosa gani kutokukusifia wewe, kwani CCM ni upinzani wenzako?
Asilimia 42% ya watoto wamedumaa ubongo, unadai. Sawa. Sasa hapa Waziri wa Fedha iandike vipi bajeti ili watoto wasidumae akili, atenge fungu la kulisha watoto samaki mashuleni kuwapanua akili?
Na mwisho, kama unadai CCM hawawezi kuwa solution kwa sababu ndio chanzo cha tatizo kwa nini unawasihi CCM hao hao walete suluhisho? Amedai watu wa "stretch their brains," lakini yeye hajatupanulia mjadala.