Angalia Mwezi Ukipatwa Leo Jioni – Watch Lunar Eclipse Tonight

Je umehamasika kuangalia leo tukio la Kupatwa kwa Mwezi

  • Ndiyo

    Votes: 20 76.9%
  • Hapana

    Votes: 5 19.2%
  • Ninahofu

    Votes: 1 3.8%

  • Total voters
    26
Ndugu Mtaalamu naomba kujuzwa kuhusu hili jambo hapa nimeliona kwenye "Taarifa kwa Umma toka Hali ya Hewa"

Kwa ujumla kupatwa kwa Mwezi huwa hakuna athari kubwa katika hali ya hewa. Hata hivyo, kutokana na Mwezi, Dunia na Jua kukaa katika mstari mmoja, nguvu za uvutano huongezeka na hivyo kuweza kusababisha maji ya bahari kupwa na kujaa kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo kawaida.

Je kuna ukweli wowote hapo kwenye maandishi mekundu?
Tunaomba namba yake, itakuwa jambo jema nina hamu ya kupata clarification ya jambo hili

Kujaa na kupwaa huongezeka mara mbili kila mwezi, siyo tu wakati wa kupatwa kwa Mwezi au Jua.

Dunia,Mwezi, na Jua, huwa katika mstari mmoja kila mwezi mara mbili. Yaani kila Mwezi mwandamo pamoja na kila Mwezi mpevu ambazo hutokea kila mwezi.

Kwa hiyo mara mbili kila mwezi maji ya bahari hujaa na kupwaa kwa kiasi kikubwa kila Mwezi mwandamo na Mwezi mpevu, yaani, kila mwezi mara mbili.

Mvuto wa graviti hunaongezeka wakati huo kwa vile Mwezi na Jua vyote vinavuta maji kwao kwa hiyo hujaa kiasi kikubwa na pia hupwaa kiasi kikubwa.
 
Hao ndiyo wataalamu wetu, nimeshangaa kuona taarifa hiyo kwakuwa kujaa na kupwaa kwa kaji baharini ni kitendo endelevu mwaka mzima, lakini Hali ya hewa wanatuaminisha kuwa kitendo hicho husababishwa na lunar eclipse
 
Yaap.nafikiri ungekuwa baharini usiku huu ungeona.au kesho nenda baharini.ukaone maji yalipo fikia usiku wa leo.
TUMUACHE MUNGU AITWE MUNGU.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kwamba yamejaa kuliko siku zingine au imekuwaje

Tazama Mtaalamu alivyoandika hapa chini

Tunaomba namba yake, itakuwa jambo jema nina hamu ya kupata clarification ya jambo hili

Kujaa na kupwaa huongezeka mara mbili kila mwezi, siyo tu wakati wa kupatwa kwa Mwezi au Jua.

Dunia,Mwezi, na Jua, huwa katika mstari mmoja kila mwezi mara mbili. Yaani kila Mwezi mwandamo pamoja na kila Mwezi mpevu ambazo hutokea kila mwezi.

Kwa hiyo mara mbili kila mwezi maji ya bahari hujaa na kupwaa kwa kiasi kikubwa kila Mwezi mwandamo na Mwezi mpevu, yaani, kila mwezi mara mbili.

Mvuto wa graviti hunaongezeka wakati huo kwa vile Mwezi na Jua vyote vinavuta maji kwao kwa hiyo hujaa kiasi kikubwa na pia hupwaa kiasi kikubwa.
 
Hao ndiyo wataalamu wetu, nimeshangaa kuona taarifa hiyo kwakuwa kujaa na kupwaa kwa kaji baharini ni kitendo endelevu mwaka mzima, lakini Hali ya hewa wanatuaminisha kuwa kitendo hicho husababishwa na lunar eclipse
SIO KILA KITU MNAKOSOA TUU MUWE MNASOMA TAARIFA KWA UMAKINI MIMI SIYO MTAALAMU WA HAYA MAMBO LAKINI NILICHO KIELEWA KWENYE HIYO TAARIFA NI KWAMBA MAJI UPWA NA KUJAA BAHARINI KILA MARA ILA KWA TUKIO HILI MAJI YANAWEZA KUPWA NA KUJAA KWA ZAIDI ILIVYO KAWAIDA NANUKUU

Kwa ujumla kupatwa kwa Mwezi huwa hakuna athari kubwa katika hali ya hewa. Hata hivyo,
kutokana na Mwezi, Dunia na Jua kukaa katika mstari mmoja, nguvu za uvutano huongezeka
na hivyo kuweza kusababisha maji ya bahari kupwa na kujaa kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo
kawaida.
 
Hali ya kuwa mstari mmoja inatokea kila mwezi mara mbili, siyo tu wakati wa kupatwa. Kiasi cha maji kujaa au kupwaa hauna tofauti kati ya siku za mwandamo au mpevu au kupatwa. Mara zote hizi tatu maji yanavutwa kiasi hicho hicho. Siyo kwamba wakati wa kupatwa maji yanavutwa zaidi kuliko wakati wa mwandamo na mpevu.
 
NAENDELEA KUWATETEA HAO JAMAA WA HALI YA HEWA KWA KUNUKUU MAELEZO YAO KUWA WAmesema kupatwa kwa mwezi hakuna athari kubwa katika ya hali ya hewa.msitari wa kwanza kabisa hapo nilipo nukuu sasa mkuu sijui wewe unaelewa tofauti.
 
Nilielewa kuwa tunazungumzia nukuu tofauti uliowekwa rangi nyekundu:

Hata hivyo, kutokana na Mwezi, Dunia na Jua kukaa katika mstari mmoja, nguvu za uvutano huongezeka na hivyo kuweza kusababisha maji ya bahari kupwa na kujaa kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo kawaida.

Inaelekea tulikuwa tumepishana katika nukuu tunazozungumzia
 
NAENDELEA KUWATETEA HAO JAMAA WA HALI YA HEWA KWA KUNUKUU MAELEZO YAO KUWA WAmesema kupatwa kwa mwezi hakuna athari kubwa katika ya hali ya hewa.msitari wa kwanza kabisa hapo nilipo nukuu sasa mkuu sijui wewe unaelewa tofauti.

Mkuu tazama sentesi hizi mbili hapa chini, ya kwanza ni nukuu yako na ya pili ni nukuu ya Mtaalamu wa mambo ya anga

Hata hivyo,
kutokana na Mwezi, Dunia na Jua kukaa katika mstari mmoja, nguvu za uvutano huongezeka
na hivyo kuweza kusababisha maji ya bahari kupwa na kujaa kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo
kawaida.

Siyo kwamba wakati wa kupatwa maji yanavutwa zaidi kuliko wakati wa mwandamo na mpevu.
 
Muulize.ana kipimo cha kujua.kuwa maji leo yamejaa sababu ya kawaida.au yamejaa sababu ya kupatwa kwa mwezi?
Inawezekana hyo sababu aliyotoa ni sawa.lakini pia .NA WATAALAM WAKO SAWA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nafahamu baadhi ya maeneo huwa na vipimo moja wapo ni kwenye baadhi ya mahoteli makubwa yaliyopo mwambaoni mwa bahari, ila sasa Mtaalamu - Mbobezi anaonekana kuwa na uhakika zaidi juu ya anachokikanusha kwa watu wa hali ya hewa
 
Sawa.lakini dunia nzima inajua kupatwa kwa mwezi,ni sababu moja wapo ya kupwa na kujaa kwa bahari.
Sija kataa maelezo yake.ni kweli sio lazma mwezi upatwe ndo kutokee kupwa na kujaa kwa bahari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa.lakini dunia nzima inajua kupatwa kwa mwezi,ni sababu moja wapo ya kupwa na kujaa kwa bahari.
Sija kataa maelezo yake.ni kweli sio lazma mwezi upatwe ndo kutokee kupwa na kujaa kwa bahari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika enzi hii ya muamsho wa kisayansi tutumie nafasi zote kuwajuza wananchi kuwa upana kuliko kubana maelezo. Nia ni kutumia nafasi za matukio maarufu kwaelimisha wananchi ili waelewe sayansi ya tukio kwa upana pamoja na kwa undani.
 
Back
Top Bottom