101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,122
Anaandika Dr Primus Saidia
Kwako Spika wa Bunge la Tanzania Mh. Tulia Akson
Kwa muda sasa bunge lako linatumika vibaya kubagaza elimu na wabunge wanaojiita wa la saba wakiongozwa na Msukuma.
Karibu kila mara wakisimama wanajaribu kuonesha taifa kwamba wao si wasomi na wamefanikiwa, na mazungumzo yao mara nyingi kama sio zote yanabeza elimu, kinyume na mtizamo, sera, imani namwenendo mzima wa serikali yetu sasa na baadae!
Si kweli kuwa kufanikiwa kupata senti mbili tatu na kumiliki gari moja au mbili ndiyo msingi wa mafanikio kama taifa.
Wasomi walio wengi hata wale waliogundua spika ambazo hawa la saba wanatumia kutukana usomi hawakuwa au hawakuhitaji utajiri. Waliogundua ndege ambazo zinawapeleke hawa wa la saba dunia nzima sio matajiri ila mchango wao ni mkubwa kwa dunia nzima.
Wanaotibu wagonjwa mahospitalini hawapimwi kwa magari wanayoendesha bali kwa wagonjwa wanaopona wakiwepo hawa wanaojiita la saba bungeni.
Nichukue fursa hii kama mtanzania kuwaasa waache hiyo tabia maana inaathiri mtizamo wa watoto wetu na mustakabali wa taifa kwa ujumla.
Pia nikuombe utumie kanuni na kiti chako kukemea kauli za kudumaisha elimu na kama wakiendelea wapate adhabu zinazostahili.
Wabilahi Tawfiq