Andiko latimia mapinduzi ya redio yakamilika 93.7 EFM yatinga hewani

Andiko latimia mapinduzi ya redio yakamilika 93.7 EFM yatinga hewani

shifta

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
474
Reaction score
192
Miezi ikapita, mawiki yakasonga hatimae siku, masaa na dakika zake zikapotea na sasa EFM inayopatikana katika masafa ya 93.7 imesikika hewani kwa majaribio kwa mara ya kwanza.

Redio hii iliobeba watangazaji mahiri, waandaaji wa vipindi wenye umakini, ma DJ wanao sadikiwa kuwa walishushwa kwa ajili ya kazi hii, uongozi thabiti na yenye usikivu mujarab, habari zake zilianza kupenya kwenye masikio ya washashi mwishoni mwa mwaka jana na kupelekea wamiliki na wadau wa redio nyengine kukosa usingizi na hata siku wakiupata basi huweweseka usiku na kupiga mayowe ama kujikuta wakikosa hata nguvu ya kuzuia haja ndogo kutoka.

Redio hii itadili kwa asilimia 85 na burudani...na watakaoongoza balaa hilo ni watu wenye kulijuwa game kwa kipindi kirefu saana na burudani iliolengwa hapa hakika ndio mwiba mchungu utaowatesa weengi waliowanyonya na kuwanyanyasa wasanii kwa miongo kadhaa sasa.

Nanga ndio imeshainuka...
Unyonyaji ndio umekwisha...
Wanyonge mtafarijika...
Game litabadilika...
Vilaza wataaibika...
Walio makini watasikika...
 
hii redio iko mji gani?? mwanza, dodoma, dar, arusha au kilwa?
 
nikiwa arusha nitaipata 93.7, nikiwa mbeya 93.7, mtwara 93.7, kagera 93.7......!!!??
 
Hongereni wana Itigi kwa kuanzisha radio ya jamii.
 
Asante ndoto njema.mbwembwe zote za nn? Ila mjue ya kua cloudsfm n:do ya Mungu ukweli unauma ila nifanyeje
 
nikiwa arusha nitaipata 93.7, nikiwa mbeya 93.7, mtwara 93.7, kagera 93.7......!!!??


nina hakika Jumatano ya leo haitaisha bila kusikia habari zaidi juu ya hii Redio...
 
Asante ndoto njema.mbwembwe zote za nn? Ila mjue ya kua cloudsfm n:do ya Mungu ukweli unauma ila nifanyeje


nina hakika ndani ya mawiki 8 wewe utarudi hapa ukiwa kama shuhudi uliesilimu...
 
Back
Top Bottom