SI KWELI PreGE2025 Andiko hili limeandika na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

SI KWELI PreGE2025 Andiko hili limeandika na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
KIKWETE23JULAI2025.jpg
 
Tunachokijua
Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alihudumu katika nafasi hiyo kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.

Katika mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Januari 19, 2025 uliompitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho, Kikwete alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika mkutano ambapo alisema,

"Hakuna mwingine isipokuwa Samia Suluhu Hassan, hakuna mwingine isipokuwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Kila chama kina utaratibu wake na wakati wake wa kuteua wagombea, na uamuzi ni wa kikao hiki. Wenzetu wengine kama Namibia kule wanafanya uamuzi mwaka mzima kuteua wagombea, sasa kama tunataka tuamue leo kwamba Samia ndiyo mgombea wetu na Dkt. Mwinyi ndiyo mgombea wetu mamlaka hayo tunayo"

Tarehe 18, Julai 2025 Balozi Humphrey Polepole alifanya mkutano na waandishi wa habari mbashara kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alikosoa utaratibu uliotumika kumpata mgombea wa Urais pamoja na makamu wake ndani ya CCM ambapo alisema

"Ule mchakato ni kama mtakatifu, hautakiwi kuwa na waa lakini ukiingiza waa unatia doa wagombea wetu, hilo moja nimeona lilikwenda ndivyo sivyo, mimi nilishindwa hata kuwapongeza, sijawapongeza mpaka leo, unapongeza vipi kisicho halali?


Ipo picha ya andiko iliyochapishwa katika mtandao wa Facebook likidaiwa kuchapishwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mtandao wa X na kusema

"Nimesikia kelele nyingi sana mtandaonikuhusu mgombea wetu, Tukisema tutoe fomu kwa wagombea wengi wa uraisi Raisi wetu kipenzi mama Samia atawekewa pingamizi maana kwa mujibu wa katiba yetu ukitumikia nafasi ya umakamu wa raisi huruhusiwi kuchukua fomu ya uraisi ni bora nilivyompitisha juu kwa juu vinginevyo angekwama"


Je, ni upi uhalisia wa andiko hilo?


Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha andiko hilo si la kweli kwani utafutaji wa maneno muhimu (Key words serch) umeonesha kuwa halijachapishwa kwenye ukurasa wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Andiko hilo ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani katika ukurasa wa X wa Kikwete taarifa ya mwisho mpaka kufikia leo Julai 23, 2025 alichapisha ujumbe wa kumpongeza Profesa Mohamed Janabi kwa kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa shirika la afya duniani (WHO) kanda ya Afrika, ambapo ujumbe huo ulichapishwa Mei 19, 2025.

Kumbuka wapotoshaji wanaweza kutengeneza machapisho kwa kutumia utambulisho wa watu maarufu kama wanasiasa, viongozi wa serikali, wasanii ama watu wenye ushawishi, ili kusambaza taarifa zisizo za kweli. Rejea hapa, hapa na hapa.​
Back
Top Bottom