Ili mradi ni Muhongo ndo anasimamia hii sektaIn way, anajejeli akina Mengi. Bado serikali itawekeza kwenye Nishati ya umeme lakini ushiriki wa sector binafsi ni muhimu.
Kikubwa ni uzalendo katika kuuziana umeme huo. Majizi ya 10 yakiingia tena hapo, we are finished!
nadhani pia kwa usalama wa uchumi na taifa kwa ujumla utaratibu wa kubinafsisha uzalishaji wa umeme huenda ukawa hatari!fikiri kama mzalishaji kwa sababu yoyote ile akashindwa kuelewana na TANESCO na kuamua kusitisha uzalishaji nini kitatokea...nchi inaweza kuwa gizani!na vipi huyo mzalishaji akisema hapati faida au ghafla 'akafirisika' kama home shopping centre...tutakaa gizani!!!!
Mfano TTCL.nadhani pia kwa usalama wa uchumi na taifa kwa ujumla utaratibu wa kubinafsisha uzalishaji wa umeme huenda ukawa hatari!fikiri kama mzalishaji kwa sababu yoyote ile akashindwa kuelewana na TANESCO na kuamua kusitisha uzalishaji nini kitatokea...nchi inaweza kuwa gizani!na vipi huyo mzalishaji akisema hapati faida au ghafla 'akafirisika' kama home shopping centre...tutakaa gizani!!!!
The Boss,
Inawezekana hizi taarifa zilikupita lakini si za jana wala leo... in short ni mpango ambao uliasisiwa kabla ya Magufuli hajaingia madarakani na kabla wakati sakata la Escrow halijachukua kasi. Ikiwa umesahau, basi rejea ule mpango wa kuivunja TANESCO na kuwa mashirika matatu-- la uzalishaji, usafirishaji na usambazaji. Kwenye huo mpango ndo unakutana na hilo suala la sekta binafsi kuzalisha umeme!
Kwa upande mwingine usisahau-- pia hakuna jipya katika hilo manake tayari sekta binafsi zinazalisha na kuwauzia umeme TANESCO. Hawa ni pamoja na Symbion as well as IPTL. Kinachotokea hivi sasa ni kama tu kurasmisha suala la sekta binafsi kuingia huko kwavile wawekezaji binafsi karibu wote waliingia kwenye biashara hii kwa sababu maalum ambayo ilikuwa ni kutatua dharura ambayo ilitokea! Rejea ujaji wa IPTL na Richmond including PAN Energy (sina hakika na hili jina)! Hawa wote waliingia kwa dharura! So, the idea ni kwamba, badala ya kusubiri dharula itokee (upungufu mkubwa wa umeme) ndipo kuwataka sekta binafsi wazalishe umeme wa dharula basi ni heri wale wenye uwezo waruhusiwe kuingia kwenye hiyo biashara moja kwa moja ili kuzuia hizo dharula zisitokee! Kinyume chake ni TANESCO wenyewe wawe na uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kwa kutumia vyanzo mbalimbali ambao hata kama utatokea ukame wa kutisha; isiwe tena sababu ya kuingia kwenye dharula! Now the question is: Je, TANESCO wanao huo uwezo? Ikiwa tunajiridhisha hawana na serikali haina uwezo au sababu ya ku-finance basi hakuna mbadala zaidi ya sekta binafsi kuingia mchezoni na sio kusubiria ukame halafu zabuni zianze tena kutolewa kwa vi-memo.
Kwa ajili ya usalama wa nchi, sector ingebaki mikononi mwa serikali. Nchi nyingi ambazo ni developed ndiyo sera yao. Au angalau kampuni ya nchi husika sio ya njeMfano TTCL.
Ili mradi ni Muhongo ndo anasimamia hii sekta
tegemea business as usual ..
Muhongo anadai asilimia 90 ya umeme Tanesco inunue...
hatari sana
Kuna vitu viwili ambavyo kwa maoni yangu serikali isingeachia sekta binafsi ivitawale. Kimoja ni uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme na cha pili ni uagizaji na uuzaji wa nishati ya mafuta. Hivi ni vitu vya muhimu sana kwa uchumi na usalama wa nchi na nadhani ni kosa kuiachia sekta binafsi. Nilikuwa nangoja nisikie wakisema kuwa wanafufua kiwanda cha uchakataji wa mafuta ghafi-TIPER- ambapo serikali ingeagiza na kuchakata mafuta hayo humu nchini. Bei ya mafuta ingepungua sana na serikali ingepata faida kubwa licha ya ajira lukuki ambazo zingetengenezwa. Kwa sasa ambapo bei ya mafuta katika soko la dunia ni $30 sidhani kuwa bei ingekuwa wastani wa sh. 1800 kwa lita ambazo tunauziwa kwa sasa. Ni ukweli unaouma kuwa TANESCO ilishanyanganywa uwezo wake wa kuzalisha umeme isipokuwa ule wa vyanzo vya maji. Kwa gesi yetu ungedhani kuwa umeme ushuke bei lakini sivyo. Kuna vigogoi wanaoitwa wawekezaji ambao wamekopeshwa na serikali pesa za kununulia majenereta na wameyategesha wakaunganisha na gesi na wao ndo wanaoiuzia TANESCO umeme. Wananunua gesi kwa makampuni ya gesi inayoitwa ni yetu??? na wanazalisha umeme na kuiuzia TANESCO kwa bei juu. Nini kingekuwa kigumu kwa tanesco kumiliki majenereta hayo? Ilianza wakati wa Net group solutions wakati ule wa Mkapa....!!!!
Mzimu wa Muhongo unawasumbua kwelikweli tueleze ni wapi na lini muhongo katamka kkwamba tanesco haitazalisha umeme??? Kinachosisitizwa na jembe hili ni wawekezaji binafsi pia kuzalisha umeme ili uwe wa kutosha na si kutegemea tanesco pekee. Kukiwa na mgawo wa umeme mnalalamika monopoly ya tanesco, watu wakialikwa kuzalisha umeme zaidi mnalalamika ooohhh tanesco inanyang'anywa jukumu lake. Acheni jembe lifanye kazi hizi cheap politics hazitawasaidia
Miaka 50 sasa; huo umeme wanaozalisha uko wapi ukiacha ule wa maji?! Mara zote inapotokea dharula ya umeme TANESCO wameshawahi kuwa na uwezo ku-accommodate hiyo dharula zaidi ya kurudi kwenye sekta binafsi? Sasa kwanini tusubirie dharula kisha tuje na project za zima taa kama zile ya IPTL na Richmond?! Na ndio maana nikauliza; je tumejiridhisha ikiwa TANESCO wanao uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha ambao haitajalisha kwamba kuna ukame mwaka mzima au mvua mwaka mzima... bado umeme unaozalishewa na TANESCO uwe na uwezo wa kuhudumia wataje wake!Why tanesco wazuiwe kuzalisha sasa?
why generation ya Tanesco iwe ya kwanza kubinafsishwa?
why now? why so fast?
Why Tanesco inyang'anywe generation? na itakiwe kununua aslimia 90?
huku uwezo haina wa kununua? nani atakaeumia?