Anayoyafanya RC Ally Hapi wa Iringa ndiyo yaliyoondoa uhai wa Dr Kleruu. Hawa vijana wajifunze kuongoza kwa hekima

Ni kweli...Gambo kwa sasa anajitahidi,lkn pengine anaendelea ila kwa tahadhari ya kutokuonekana kwenye vyombo vya habari
Kaska

Gambo yuko vizuri kuna jirani wake huko kwenye mavito ya thamani alikuja moto tunashukuru mungu kaa roho cha hekima kameanza kumyemelea .Ni bora swala la historia ya mtu iangaliwe sio kumpa cheo kikubwa afanye majaribio kwenye maisha ya watu.
 
Mara kadhaa nimeandika humu jukwaani,na leo tena ninaandika,ninaandika baada yakuona muendelezo wa madudu aliyofanya RC wa Iringa dhidi ya daktari bingwa wa Mkoa,lakini ninaandika pia bada ya kufauatilia kwa njia mbalimbali udhalilishaji na vitisho vya kupotezwa kwa watu ambao RC huyu ametamka hadharani kuwa kuna watu "atawapoteza".

Hawa vijana wa sasa wanatakiwa wafundishwe "historia za Wakuu wa Mikoa" ili waweze kujifunza na kuishi na jamii husika bila kupandikiza chuki.

Hili Mwalimu alilitambua baada ya tukio la Mkulima wa Kihehe wa Kijiji cha Mkungugu Isimani kumtandika risasi hadharani Mkuu wa Mkoa Kleruu kisa "lugha za kashfa na kukosa heshima".

Lakini vijana wa sasa wanaokuwa wakuu wa Mikoa na Wilaya wanadhani "chuki" ya Mzee Mwamwindi kwa Dr Wilbert Kleruu ilijengwa kwa siku moja;hapana...Ulikuwa ni muendelezo wa chuki za Wakuu wa mikoa waliotangulia kuweka dharau kwa wananchi.

Mwaka 1965- 1968 Mkuu wa Mkoa Iringa alikuwa anaitwa Said Shamshama,huyu alikuwa na maneno ya kejeli sana,dhihaka na lugha ya hovyo kwa wananchi.

Wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya Uhuru 1966 akihutubia wananchi wa Iringa,akahimiza walime mazao ya biashara ili wajipatie kipato cha ziada,hasa chai na kahawa.Wazee wakaitikia,muitiko huo ukasbabibisha mazao ya chakula kupungua,na hatimaye 1967 Iringa kama moja ya "basket of Southern Highlands" ikawa na chakula kichache.

Sherehe za Wakulima 1967,Wakiwemo kina Mzee Mwamwindi kama wakulima wakubwa Iringa walifika,RC akawatukana sana kuwa ni wajinga,walipoambiwa kulima mazao ya biashara wooote walilima bila kukumbuka ya chakula.Bwana Shamshama akatukana sana kama anavyofanya Ally Hapi kwenye ziara yake ya Tarafa za Mkoa wa Iringa.Jopo la Wazee Wakulima wa Iringa wakiongozwa na "bepari" Mwamwindi wakachukia sana.

Katikati ya hotuba akaonekana Mzee mmoja anapanda jukwaani,watu wakajua ni mzee wa TANU anakwenda kuchukua itifaki.Kumbe Mzee ana yake,alipofika Jukwaani alimuwasha RC Shamshama "kerebu" kadhaa za uhakika.Akamwambia mwaka jana ulituambia tulime mazao ya biashara,mwaka huu unatukashifu tena mbele ya wake zetu;Ikawa tafrani kwenye uwanja ule ambao sasa unaitwa Uwanja wa Samora,Mzee yule alifungwa gereza la Isupilo.

Nyerere akamtoa RC Shamshama akamleta RC John Mwakangale,ambaye hakukaa sana ndio akaja Dr Kleruu 1970-1971.

Dr Kleruu kaja kama kijana,damu inachemka,akiwa na PhD ya mambo ya Kilimo toka nje,na Mwalimu alimpeleka Iringa sababu wakati huo Isimani ndio ilikuwa inalima mahindi na kulisha Tanzania nzima,mpaka vitabu vya Jiografia elimu ya Msingi vilikuwa na mada inaitwa "Kilimo cha Mahindi Isimani".

Dr Kleruu akataka kuwakomesha wale wazee mabepari wa Iringa ambao mmoja wa mwanakambi wao alimpiga kerebu RC Shamshama.Matokeo yake akaingia anga za Mzee Mwamwindi akapigwa shaba,na siku hiyo Iringa nzima watu walisherekea kwa kunywa pombe kwenye vijiwe vya ulanzi vya Isoka na Mlandege.(Ingawa kuna sababu nyingine ya kijamii ya Kleruu kusababisha kupigwa risasi)

Lakini chuki kwa Kleruu ilianzia kwa RC Shamshama,watu wakawa wanaona hawa RC's mbona wanakuwa waonezi sana.Na ndio maana hata Mwamwindi ktk kujieleza kwake,inasemwa aliwahi kujibu "Siwezi kuomba msamaha,na hata mkiniachia,naweza kumfuata huyo aliyemleta huyu Gavana(RC) huku,na hakumwambia kuwa huku kuna wanaume wenye mkoa wao"

Nyerere akaona isiwe tabu,ngoja apige sahihi jamaa apigwe kitanzi kuwatisha Wazee wengine wa mji.

Sasa hawa vijana kama kina Makonda,Gambo na huyu Happi aliyevamia Iringa wajifunze.Hatuombei yatokee ya Shamshama na kina Kleruu,wala si vyema,lkn binadamu ni mnyama;ana kiwango cha mwisho cha uvumilivu.Wasiongoze kwa kupandikiza chuki na visasi vya hadharani,bali kwa weledi,haki,kanuni,sheria na taratibu.

Hakuna uongozi wa kisasi na kukomoana uliowahi kushinda;kila palipo na hulka ya kisasi na kukomoana chuki hujengeka.Matukio ya Iringa kwa Kleruu na kwingine ambapo nyakati hizo hayakuripotiwa sana kutokana na "uhuru wa habari" kuwa finyu,yalimfundisha Nyerere.Na baadae alimleta RC Mohamed Kissocky kutuliza hali ya hewa.

Ndio maana ya kuwa na Chuo kama Kivukoni,zaidi ya kufundisha itikadi ya chama na TUNU za mwana-TANU,kiliwafunza vijana namna ya uongozi na maadili yake.Hapa ndipo tuliwapa watu kama Jakaya Kikwete,Nikodemus Banduka,Jaka Mwambi,Hussein Shekilango,Horace Kolimba nk.

Tuwafunze vijana,kuepuka siasa za visasi na kukomoana.Huwezi kutoka hadharanj unamtishia diwani au daktari au mtendaji wa kijiji,tena unajinasibu kabisa kuwa "Mimi ni mtu hatari,nitakupoteza".Hivi hawa vijana wanalelewa wapi siku hizi kujua miiko na kauli za kiongozi?

Wewe Mkuu wa Mkoa,mwenye cheo cha kisiasa,ambacho si cha kudumu,unapata wapi ujasiri wa kumtishia mtu kuwa utampoteza?.Mkoa mzima una daktari bingwa mmoja,anahudumia zaidi ya wagonjwa milioni mbili katika mkoa na wilaya zake,ana mshahara duni,mazingira mabovu ya kazi na hana hata posho za kumtosha,unapata wapi ujasiri wa kumtisha?

Unamtisha daktari bingwa,unamdhalilisha kwa maneno ya kuudhi,daktari pekee katika mkoa mnayepaswa kesho mkae pamoja mpange mikakati ya kunusuru sekta ya afya katika mkoa wako.Huyu ni daktari bingwa,ambaye mkeo wewe RC akiugua usiku ghafla,unampeleka kwake,unamuacha kwenye chumba cha huduma wakiwa wawili,ili apate nafasi ya kumpekua mkeo na kuokoa maisha yake,huyuhuyu daktari ndio atakuhudumia na wewe kabla hujatumiwa chopa kukupeleka Dsm kwa huduma zaidi.

Wewe bwana mdogo Hapi,uongozi ni hekima,siyo sifa za mbele ya Tv.Huo mkoa uliopo una historia yake,usifuate hao wazee wa chama waliopewa kitu kidogo wakakuvalisha mavazi ya kichifu ukadhani hao ndio wazee wa mji,hao ni wazee wataka fursa tu,wenyewe wakishitaki kwa wazee wao utapata tabu ya kuongoza.Kila mkoa una miiko yake,ndio maana mkoloni alitumia "Indirect Rule" kwa kutumia viongozi wa maeneo husika ili kuepuka kuwa na watu wanaovamia maeneo bila kujua utamaduni wao.

Hii iwe fundisho kwa wakuu wote wa Mikoa Tanzania;Na huko upinzani,jengeni vijana katika utaasisi,maana wanasema "A leader is born at home,and be made at School".Lets istitutionalize the leadership skills of our young generation for the coming line of leadership.

barafu wa Jf
Winter holiday somewhere in Africa.
Mkuu barafu umetimiza wajibu wako kwa taifa, sasa kazi kwao watoto wa "malyatabu"
 
Umeikimbia baridi ya Toronto? Karibu tena Africa mkuu na kuhusu hao vijana acha waote mapembe maana ndo muda wao huo. Ila wakumbuke kuna maisha nje ya uongozi.

Toronto sasa bila kulala na heated blanket,heated walls na kujipandika manguo,unapanda ngiri ya uzeeni.Bora kukimbia
 
Gambo baada ya kufiwa na mama amenyooka ...alidhan kuwa mkuu wa mkoa kunamtenganisha yeye na ndugu zake na vifo . Na juzi tena kafiwa na dada yake lazima displn iwepo ..... unajua hapa duniani ukiwa na pesa ukaeshimika na kila uliwazalo lina fanyika,hakuna ndugu yako aliye hospitalin wote mna sherehekea uzima.....uwa kunakuwa na kiburu sana lakin ukipatwa na misukosuko ya dunian lazima uwaheshimu watu wa rika zote....
Muasisi wa siasa za chuki, visasi, ubaguzi na ukatili nchi hii anajulikana na adhabu yake kwa Mungu huyu wa malipizi imeandikwa kwa moto! Wanachokosea hawa vijana ni kumuiga tembo kunya, huko waendako watalia na kusaga meno hiki kipindi cha mpito kikimalizika, sijui watajificha wapi! Gambo amebadilika sana, ameyaona maisha katika mwanga bora, ni muungwana sana siku hizi, tumwache Hapi achezee wanyalukolo atakiona cha moto!
 
Tatizo la Watanzania mmezoea "kubembelezwa bembelezwa" sana, akitokea mtu ambaye yuko "serious" mnaanza kulia lia. Anachokifanya Hapi, yuko sahihi kabisa, kama mtu ni mzembe ni haki yake kukaripiwa hata kama ni mbele ya watoto na mke wake.

Watanzania wazembe wazembe mtanyooka tu, Magufuli na Serikali yake wapo mpaka 2025, lazima mtanyooka tu!
 
Hiyo kauli kamwambie Jaffo alieomba radhi kwa niaba ya serikali.!
 
Story ndeeefuuu, maneno meeewngiiii kumbe ni upuuzii mtupu. Kajipange upya.
 
Boss barafu Umenena Vyema, Natumaini Ujumbe umefika,
Mhusika na Wahusika wa Hulka yake wanatakiwa kujua:
1. Uongozi ni Dhamana.
2. Kuna maisha nje ya Uongozi na Siasa.
3. Uongozi sio lazima uwe kwenye Tv kila uchwao, hii itafanya uchokwe mapema.
4. Uongozi mzuri ni wa Maneno machache ila Matendo zaidi yawe mengi.
Na mengineyo

Mara kadhaa nimeandika humu jukwaani,na leo tena ninaandika,ninaandika baada yakuona muendelezo wa madudu aliyofanya RC wa Iringa dhidi ya daktari bingwa wa Mkoa,lakini ninaandika pia bada ya kufauatilia kwa njia mbalimbali udhalilishaji na vitisho vya kupotezwa kwa watu ambao RC huyu ametamka hadharani kuwa kuna watu "atawapoteza".

Hawa vijana wa sasa wanatakiwa wafundishwe "historia za Wakuu wa Mikoa" ili waweze kujifunza na kuishi na jamii husika bila kupandikiza chuki.

Hili Mwalimu alilitambua baada ya tukio la Mkulima wa Kihehe wa Kijiji cha Mkungugu Isimani kumtandika risasi hadharani Mkuu wa Mkoa Kleruu kisa "lugha za kashfa na kukosa heshima".

Lakini vijana wa sasa wanaokuwa wakuu wa Mikoa na Wilaya wanadhani "chuki" ya Mzee Mwamwindi kwa Dr Wilbert Kleruu ilijengwa kwa siku moja;hapana...Ulikuwa ni muendelezo wa chuki za Wakuu wa mikoa waliotangulia kuweka dharau kwa wananchi.

Mwaka 1965- 1968 Mkuu wa Mkoa Iringa alikuwa anaitwa Said Shamshama,huyu alikuwa na maneno ya kejeli sana,dhihaka na lugha ya hovyo kwa wananchi.

Wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya Uhuru 1966 akihutubia wananchi wa Iringa,akahimiza walime mazao ya biashara ili wajipatie kipato cha ziada,hasa chai na kahawa.Wazee wakaitikia,muitiko huo ukasbabibisha mazao ya chakula kupungua,na hatimaye 1967 Iringa kama moja ya "basket of Southern Highlands" ikawa na chakula kichache.

Sherehe za Wakulima 1967,Wakiwemo kina Mzee Mwamwindi kama wakulima wakubwa Iringa walifika,RC akawatukana sana kuwa ni wajinga,walipoambiwa kulima mazao ya biashara wooote walilima bila kukumbuka ya chakula.Bwana Shamshama akatukana sana kama anavyofanya Ally Hapi kwenye ziara yake ya Tarafa za Mkoa wa Iringa.Jopo la Wazee Wakulima wa Iringa wakiongozwa na "bepari" Mwamwindi wakachukia sana.

Katikati ya hotuba akaonekana Mzee mmoja anapanda jukwaani,watu wakajua ni mzee wa TANU anakwenda kuchukua itifaki.Kumbe Mzee ana yake,alipofika Jukwaani alimuwasha RC Shamshama "kerebu" kadhaa za uhakika.Akamwambia mwaka jana ulituambia tulime mazao ya biashara,mwaka huu unatukashifu tena mbele ya wake zetu;Ikawa tafrani kwenye uwanja ule ambao sasa unaitwa Uwanja wa Samora,Mzee yule alifungwa gereza la Isupilo.

Nyerere akamtoa RC Shamshama akamleta RC John Mwakangale,ambaye hakukaa sana ndio akaja Dr Kleruu 1970-1971.

Dr Kleruu kaja kama kijana,damu inachemka,akiwa na PhD ya mambo ya Kilimo toka nje,na Mwalimu alimpeleka Iringa sababu wakati huo Isimani ndio ilikuwa inalima mahindi na kulisha Tanzania nzima,mpaka vitabu vya Jiografia elimu ya Msingi vilikuwa na mada inaitwa "Kilimo cha Mahindi Isimani".

Dr Kleruu akataka kuwakomesha wale wazee mabepari wa Iringa ambao mmoja wa mwanakambi wao alimpiga kerebu RC Shamshama.Matokeo yake akaingia anga za Mzee Mwamwindi akapigwa shaba,na siku hiyo Iringa nzima watu walisherekea kwa kunywa pombe kwenye vijiwe vya ulanzi vya Isoka na Mlandege.(Ingawa kuna sababu nyingine ya kijamii ya Kleruu kusababisha kupigwa risasi)

Lakini chuki kwa Kleruu ilianzia kwa RC Shamshama,watu wakawa wanaona hawa RC's mbona wanakuwa waonezi sana.Na ndio maana hata Mwamwindi ktk kujieleza kwake,inasemwa aliwahi kujibu "Siwezi kuomba msamaha,na hata mkiniachia,naweza kumfuata huyo aliyemleta huyu Gavana(RC) huku,na hakumwambia kuwa huku kuna wanaume wenye mkoa wao"

Nyerere akaona isiwe tabu,ngoja apige sahihi jamaa apigwe kitanzi kuwatisha Wazee wengine wa mji.

Sasa hawa vijana kama kina Makonda,Gambo na huyu Happi aliyevamia Iringa wajifunze.Hatuombei yatokee ya Shamshama na kina Kleruu,wala si vyema,lkn binadamu ni mnyama;ana kiwango cha mwisho cha uvumilivu.Wasiongoze kwa kupandikiza chuki na visasi vya hadharani,bali kwa weledi,haki,kanuni,sheria na taratibu.

Hakuna uongozi wa kisasi na kukomoana uliowahi kushinda;kila palipo na hulka ya kisasi na kukomoana chuki hujengeka.Matukio ya Iringa kwa Kleruu na kwingine ambapo nyakati hizo hayakuripotiwa sana kutokana na "uhuru wa habari" kuwa finyu,yalimfundisha Nyerere.Na baadae alimleta RC Mohamed Kissocky kutuliza hali ya hewa.

Ndio maana ya kuwa na Chuo kama Kivukoni,zaidi ya kufundisha itikadi ya chama na TUNU za mwana-TANU,kiliwafunza vijana namna ya uongozi na maadili yake.Hapa ndipo tuliwapa watu kama Jakaya Kikwete,Nikodemus Banduka,Jaka Mwambi,Hussein Shekilango,Horace Kolimba nk.

Tuwafunze vijana,kuepuka siasa za visasi na kukomoana.Huwezi kutoka hadharanj unamtishia diwani au daktari au mtendaji wa kijiji,tena unajinasibu kabisa kuwa "Mimi ni mtu hatari,nitakupoteza".Hivi hawa vijana wanalelewa wapi siku hizi kujua miiko na kauli za kiongozi?

Wewe Mkuu wa Mkoa,mwenye cheo cha kisiasa,ambacho si cha kudumu,unapata wapi ujasiri wa kumtishia mtu kuwa utampoteza?.Mkoa mzima una daktari bingwa mmoja,anahudumia zaidi ya wagonjwa milioni mbili katika mkoa na wilaya zake,ana mshahara duni,mazingira mabovu ya kazi na hana hata posho za kumtosha,unapata wapi ujasiri wa kumtisha?

Unamtisha daktari bingwa,unamdhalilisha kwa maneno ya kuudhi,daktari pekee katika mkoa mnayepaswa kesho mkae pamoja mpange mikakati ya kunusuru sekta ya afya katika mkoa wako.Huyu ni daktari bingwa,ambaye mkeo wewe RC akiugua usiku ghafla,unampeleka kwake,unamuacha kwenye chumba cha huduma wakiwa wawili,ili apate nafasi ya kumpekua mkeo na kuokoa maisha yake,huyuhuyu daktari ndio atakuhudumia na wewe kabla hujatumiwa chopa kukupeleka Dsm kwa huduma zaidi.

Wewe bwana mdogo Hapi,uongozi ni hekima,siyo sifa za mbele ya Tv.Huo mkoa uliopo una historia yake,usifuate hao wazee wa chama waliopewa kitu kidogo wakakuvalisha mavazi ya kichifu ukadhani hao ndio wazee wa mji,hao ni wazee wataka fursa tu,wenyewe wakishitaki kwa wazee wao utapata tabu ya kuongoza.Kila mkoa una miiko yake,ndio maana mkoloni alitumia "Indirect Rule" kwa kutumia viongozi wa maeneo husika ili kuepuka kuwa na watu wanaovamia maeneo bila kujua utamaduni wao.

Hii iwe fundisho kwa wakuu wote wa Mikoa Tanzania;Na huko upinzani,jengeni vijana katika utaasisi,maana wanasema "A leader is born at home,and be made at School".Lets istitutionalize the leadership skills of our young generation for the coming line of leadership.

barafu wa Jf
Winter holiday somewhere in Africa.
 
Tatizo la Watanzania mmezoea "kubembelezwa bembelezwa" sana, akitokea mtu ambaye yuko "serious" mnaanza kulia lia. Anachokifanya Hapi, yuko sahihi kabisa, kama mtu ni mzembe ni haki yake kukaripiwa hata kama ni mbele ya watoto na mke wake.

Watanzania wazembe wazembe mtanyooka tu, Magufuli na Serikali yake wapo mpaka 2025, lazima mtanyooka tu!
Unaonekana hakuna unachokijua wewe
 
Umemsahau Mnyeti
 
Unaonekana hakuna unachokijua wewe
Ninachokijua mimi ni kwamba hii nchi imejaa "wazembe" wengi sana, na akitokea mtu wa kukemea uzembe hadharani mnaanza kulia lia kama wewe unavyolia lia hapa. Lazima mtanyooka tu na kuacha uzembe, baada ya 2025 wazembe watakuwa wamepungua sana Tanzania.
 
Boss barafu Umenena Vyema, Natumaini Ujumbe umefika,
Mhusika na Wahusika wa Hulka yake wanatakiwa kujua:
1. Uongozi ni Dhamana.
2. Kuna maisha nje ya Uongozi na Siasa.
3. Uongozi sio lazima uwe kwenye Tv kila uchwao, hii itafanya uchokwe mapema.
4. Uongozi mzuri ni wa Maneno machache ila Matendo zaidi yawe mengi.
Na mengineyo
Nilicheka sana kuona Hapi eti mikutano yake ya kikazi ya hadhara anaita wasanii kutoka Dar wanaanza kuchekesha watu kisha anakuja yeye.
 
Back
Top Bottom