Anayoyafanya RC Ally Hapi wa Iringa ndiyo yaliyoondoa uhai wa Dr Kleruu. Hawa vijana wajifunze kuongoza kwa hekima

Muasisi wa siasa za chuki, visasi, ubaguzi na ukatili nchi hii anajulikana na adhabu yake kwa Mungu huyu wa malipizi imeandikwa kwa moto! Wanachokosea hawa vijana ni kumuiga tembo kunya, huko waendako watalia na kusaga meno hiki kipindi cha mpito kikimalizika, sijui watajificha wapi! Gambo amebadilika sana, ameyaona maisha katika mwanga bora, ni muungwana sana siku hizi, tumwache Hapi achezee wanyalukolo atakiona cha moto!

Ni kweli...Gambo kwa sasa anajitahidi,lkn pengine anaendelea ila kwa tahadhari ya kutokuonekana kwenye vyombo vya habari
 
Nashukuru umekuja na mada tofauti maana toka asubuhi hili jukwaa ni Membe!Membe!Membe!Membe!...
Hizo mada za Membe zitasababisha mtu afanye kituko. Kuna namna nyingi ya watu kuandamana na hili la Membe ni mojawapo. Jamaa analazimika kutafuta na kufuatilia ukweli wa taarifa na kiwango cha threat ghafla mtaanza kusikia mipayuko. Maana kuna maswali mengi ya kujiuliza kama vile baada ya kimyaa kikuu why now? Ukweli Lowasa siyo threat kabisa. The real threat ni Sumaye, sasa Membe naye anaanza kuibuliwa kama uyoga from no where anaza genuine threat. Nakushauri nunua pop corn mkuu. Picha ndiyo limeanza hivyo.
 
Ni kweli...Gambo kwa sasa anajitahidi,lkn pengine anaendelea ila kwa tahadhari ya kutokuonekana kwenye vyombo vya habari
Sasa hivi Gambo anafanya s8asa mbaya na za hovyo sana. Alicho advance ni kutotoa vitisho kupitia media. Ila jamaa jinsi alivyoamua kuji advance ndivyo watu nao walivyoamia ku advance mbinu za kumkabili. Ila picha lake linaenda kuisha kijinga sana kama vile la Starling wa Kihindi na maua.
 
Hizo mada za Membe zitasababisha mtu afanye kituko. Kuna namna nyingi ya watu kuandamana na hili la Membe ni mojawapo. Jamaa analazimika kutafuta na kufuatilia ukweli wa taarifa na kiwango cha threat hhafla mtaanza kusikia mipayuko. Maana kuna maswali mengi ya kujiuliza kama vile baada ya kimyaa kikuu why now? Ukweli Lowasa siyo thrwat kabisa. The real threat ni Sumaye, sasa Membe naye anaanza kuibuliwa kama uyoga from no where. Nakushauri nunua pop corn mkuu. 0icha ndiyo limeanza hivyo
Nashukuru Mkuu, na vile wanajua jiwe hana kifua wanachokifanya ni kumpa moto tu..

Kwa hasira jiwe ataanza kuua hadi mijusi akihisi ni Nyoka...
 
Jiwe ana roho ya sauli, kila wakati anaandamwa na pepo na huhitaji mpiga kinubi kumburudisha ili atulie. Wapiga vinubi wake ni wakuu wake wa vipande vya ardhi aliowateua na wateule wake wengine. Mambo ya hovyo wayafanyayo hao wateule kwake ni kama sauti za vinubi.
 
Ni kweli...Gambo kwa sasa anajitahidi,lkn pengine anaendelea ila kwa tahadhari ya kutokuonekana kwenye vyombo vya habari

Hapana kabadilika sana sio kama mwanzo, mimi ndiye Gavana wangu, nipo hapa A city na kwa jinsi mkoa huu ulivyo na Chadema in Blood wengi na ngome kuu hawezi kukwepa social media hata kama anaweza kuwakwepa mainstream media. Yapo mengi ya maelekezo lakini anajitahidi kuyatekeleza kwa busara sana nadhani alipokea ushauri wa Rais mstaafu JK kwamba "usikubali kurithi adui wa mtu, bora kutengeneza wa kwako kama ikibidi"
 
Balack Lisited.
1. Bashiwashite
2. Halali Happy
3. Malisho ya Mgambo
4. Babati Walamiwa

Hawa jaa wajiangalie sana maana tayari timing clock imeanza kuwahesabia muda wao.
Ni bora tu watokee watu waliochoshwa na kuvurugwa na madharau, vitisho na kejeli za hawa vijana wawazabe makofi wakiwa jukwaani na wananchi wote washangilie kwa nguvu kubwa hilo tukio, hapo ndo baba yao atajua kuwa watu hawapendi hata kidogo uongozi wa kibabe na madharau
 
Mara kadhaa nimeandika humu jukwaani,na leo tena ninaandika,ninaandika baada yakuona muendelezo wa madudu aliyofanya RC wa Iringa dhidi ya daktari bingwa wa Mkoa,lakini ninaandika pia bada ya kufauatilia kwa njia mbalimbali udhalilishaji na vitisho vya kupotezwa kwa watu ambao RC huyu ametamka hadharani kuwa kuna watu "atawapoteza".

Hawa vijana wa sasa wanatakiwa wafundishwe "historia za Wakuu wa Mikoa" ili waweze kujifunza na kuishi na jamii husika bila kupandikiza chuki.

Hili Mwalimu alilitambua baada ya tukio la Mkulima wa Kihehe wa Kijiji cha Mkungugu Isimani kumtandika risasi hadharani Mkuu wa Mkoa Kleruu kisa "lugha za kashfa na kukosa heshima".

Lakini vijana wa sasa wanaokuwa wakuu wa Mikoa na Wilaya wanadhani "chuki" ya Mzee Mwamwindi kwa Dr Wilbert Kleruu ilijengwa kwa siku moja;hapana...Ulikuwa ni muendelezo wa chuki za Wakuu wa mikoa waliotangulia kuweka dharau kwa wananchi.

Mwaka 1965- 1968 Mkuu wa Mkoa Iringa alikuwa anaitwa Said Shamshama,huyu alikuwa na maneno ya kejeli sana,dhihaka na lugha ya hovyo kwa wananchi.

Wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya Uhuru 1966 akihutubia wananchi wa Iringa,akahimiza walime mazao ya biashara ili wajipatie kipato cha ziada,hasa chai na kahawa.Wazee wakaitikia,muitiko huo ukasbabibisha mazao ya chakula kupungua,na hatimaye 1967 Iringa kama moja ya "basket of Southern Highlands" ikawa na chakula kichache.

Sherehe za Wakulima 1967,Wakiwemo kina Mzee Mwamwindi kama wakulima wakubwa Iringa walifika,RC akawatukana sana kuwa ni wajinga,walipoambiwa kulima mazao ya biashara wooote walilima bila kukumbuka ya chakula.Bwana Shamshama akatukana sana kama anavyofanya Ally Hapi kwenye ziara yake ya Tarafa za Mkoa wa Iringa.Jopo la Wazee Wakulima wa Iringa wakiongozwa na "bepari" Mwamwindi wakachukia sana.

Katikati ya hotuba akaonekana Mzee mmoja anapanda jukwaani,watu wakajua ni mzee wa TANU anakwenda kuchukua itifaki.Kumbe Mzee ana yake,alipofika Jukwaani alimuwasha RC Shamshama "kerebu" kadhaa za uhakika.Akamwambia mwaka jana ulituambia tulime mazao ya biashara,mwaka huu unatukashifu tena mbele ya wake zetu;Ikawa tafrani kwenye uwanja ule ambao sasa unaitwa Uwanja wa Samora,Mzee yule alifungwa gereza la Isupilo.

Nyerere akamtoa RC Shamshama akamleta RC John Mwakangale,ambaye hakukaa sana ndio akaja Dr Kleruu 1970-1971.

Dr Kleruu kaja kama kijana,damu inachemka,akiwa na PhD ya mambo ya Kilimo toka nje,na Mwalimu alimpeleka Iringa sababu wakati huo Isimani ndio ilikuwa inalima mahindi na kulisha Tanzania nzima,mpaka vitabu vya Jiografia elimu ya Msingi vilikuwa na mada inaitwa "Kilimo cha Mahindi Isimani".

Dr Kleruu akataka kuwakomesha wale wazee mabepari wa Iringa ambao mmoja wa mwanakambi wao alimpiga kerebu RC Shamshama.Matokeo yake akaingia anga za Mzee Mwamwindi akapigwa shaba,na siku hiyo Iringa nzima watu walisherekea kwa kunywa pombe kwenye vijiwe vya ulanzi vya Isoka na Mlandege.(Ingawa kuna sababu nyingine ya kijamii ya Kleruu kusababisha kupigwa risasi)

Lakini chuki kwa Kleruu ilianzia kwa RC Shamshama,watu wakawa wanaona hawa RC's mbona wanakuwa waonezi sana.Na ndio maana hata Mwamwindi ktk kujieleza kwake,inasemwa aliwahi kujibu "Siwezi kuomba msamaha,na hata mkiniachia,naweza kumfuata huyo aliyemleta huyu Gavana(RC) huku,na hakumwambia kuwa huku kuna wanaume wenye mkoa wao"

Nyerere akaona isiwe tabu,ngoja apige sahihi jamaa apigwe kitanzi kuwatisha Wazee wengine wa mji.

Sasa hawa vijana kama kina Makonda,Gambo na huyu Happi aliyevamia Iringa wajifunze.Hatuombei yatokee ya Shamshama na kina Kleruu,wala si vyema,lkn binadamu ni mnyama;ana kiwango cha mwisho cha uvumilivu.Wasiongoze kwa kupandikiza chuki na visasi vya hadharani,bali kwa weledi,haki,kanuni,sheria na taratibu.

Hakuna uongozi wa kisasi na kukomoana uliowahi kushinda;kila palipo na hulka ya kisasi na kukomoana chuki hujengeka.Matukio ya Iringa kwa Kleruu na kwingine ambapo nyakati hizo hayakuripotiwa sana kutokana na "uhuru wa habari" kuwa finyu,yalimfundisha Nyerere.Na baadae alimleta RC Mohamed Kissocky kutuliza hali ya hewa.

Ndio maana ya kuwa na Chuo kama Kivukoni,zaidi ya kufundisha itikadi ya chama na TUNU za mwana-TANU,kiliwafunza vijana namna ya uongozi na maadili yake.Hapa ndipo tuliwapa watu kama Jakaya Kikwete,Nikodemus Banduka,Jaka Mwambi,Hussein Shekilango,Horace Kolimba nk.

Tuwafunze vijana,kuepuka siasa za visasi na kukomoana.Huwezi kutoka hadharanj unamtishia diwani au daktari au mtendaji wa kijiji,tena unajinasibu kabisa kuwa "Mimi ni mtu hatari,nitakupoteza".Hivi hawa vijana wanalelewa wapi siku hizi kujua miiko na kauli za kiongozi?

Wewe Mkuu wa Mkoa,mwenye cheo cha kisiasa,ambacho si cha kudumu,unapata wapi ujasiri wa kumtishia mtu kuwa utampoteza?.Mkoa mzima una daktari bingwa mmoja,anahudumia zaidi ya wagonjwa milioni mbili katika mkoa na wilaya zake,ana mshahara duni,mazingira mabovu ya kazi na hana hata posho za kumtosha,unapata wapi ujasiri wa kumtisha?

Unamtisha daktari bingwa,unamdhalilisha kwa maneno ya kuudhi,daktari pekee katika mkoa mnayepaswa kesho mkae pamoja mpange mikakati ya kunusuru sekta ya afya katika mkoa wako.Huyu ni daktari bingwa,ambaye mkeo wewe RC akiugua usiku ghafla,unampeleka kwake,unamuacha kwenye chumba cha huduma wakiwa wawili,ili apate nafasi ya kumpekua mkeo na kuokoa maisha yake,huyuhuyu daktari ndio atakuhudumia na wewe kabla hujatumiwa chopa kukupeleka Dsm kwa huduma zaidi.

Wewe bwana mdogo Hapi,uongozi ni hekima,siyo sifa za mbele ya Tv.Huo mkoa uliopo una historia yake,usifuate hao wazee wa chama waliopewa kitu kidogo wakakuvalisha mavazi ya kichifu ukadhani hao ndio wazee wa mji,hao ni wazee wataka fursa tu,wenyewe wakishitaki kwa wazee wao utapata tabu ya kuongoza.Kila mkoa una miiko yake,ndio maana mkoloni alitumia "Indirect Rule" kwa kutumia viongozi wa maeneo husika ili kuepuka kuwa na watu wanaovamia maeneo bila kujua utamaduni wao.

Hii iwe fundisho kwa wakuu wote wa Mikoa Tanzania;Na huko upinzani,jengeni vijana katika utaasisi,maana wanasema "A leader is born at home,and be made at School".Lets istitutionalize the leadership skills of our young generation for the coming line of leadership.

barafu wa Jf
Winter holiday somewhere in Africa.
Mkuu waache tu hao vijana, kibri yao mauti yao.
Mwamwindi is just around the corner.
 
Tatizo kubwa ni kuwapa madaraka makubwa vijana wadogo wa chipukizi kuliko uwezo waliokuwa nao.

Hivi CCM hakuna wataalamu wa unyago au mkole wa kuwafunda hawa vijana?
 
Tatizo anaewateua!! Mteuaji angekuwa mtu sahihi hao wapuuzi wangekuwa wanachunga mbuzi vijinini kwao
 
Umeikimbia baridi ya Toronto? Karibu tena Africa mkuu na kuhusu hao vijana acha waote mapembe maana ndo muda wao huo. Ila wakumbuke kuna maisha nje ya uongozi.
 
Back
Top Bottom