Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Nimesikitishwa na taarifa niliyoisikia kwenye taarifa ya magazeti ya leo kuwa waziri Mkuu Pinda amesitisha zoezi lililokuwa linaendelea nchi nzima la kuwaondoa wavamizi wa barabara zetu. Kwa hakika haya ni maamuzi ya hovyo kabisa na hayatakiwi kuungwa mkono kwani yataendeleza uvunjaji wa sheria bila wahalifu kuadhibiwa.
Wanasiasa waliochoka hujitahidi kufanya maamuzi yanayopendwa na wengi tu, yale yote yasiyoungwa mkono na wengi huyaepa... lakini ukweli ni kwamba bila maamuzi yasiyopendwa dunia hii ingebaki kuwa ya ujima.. historia inatuambia kuwa maamuzi yaliyoonekana kuwa ya kijinga na kupingwa na watu wengi ndiyo yamelete neema kwenye maisha yetu ya leo {safari za mwezini,mawasiliano ya simu, redio, safari ya Ulaya-Mareka ya Christopher Collumbus, n.k.}
Bila kuwa na miundombinu inayoendana na maendeleo ya wanadamu basi tujue tunakaribisha maafa.... bomoa bomoa ni uamuzi mgumu na ambao unapingwa lakini manufaa yake ni makubwa kuliko manung'uniko yake.
Uamuzi uliochukuliwa na Pinda unafanana kabisa na maumuzi kadhaa aliyochukua Kikwete siku za karibuni.. Katiba mpya na Dowans ndiyo nayakumbuka kwa karibu..
Katiba Mpya - Waziri wa Sheria na Katiba na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikataa kata kata kuwa serikali yetu haikuwa na nafasi ya kutengeneza katiba mpya kwa wakati huu kutokana na ukosefu wa rasilimali pesa, sitaki kuamini kuwa kauli hizi zilikuwa zao binafsi.. huu ulikuwa ndio msimamo wa Rais na serikali yake.. lakini baada ya kuona kuwa uamuzi huu haukupendwa na wengi Rais alijitokeza na kusema kuwa ataanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya.. kwa juu juu huu ulikuwa uamuzi mzuri lakini kwa uthabiti wa maamuzi huu ulikuwa uamuzi wa hatari kwa serikali (ni muhimu serikali kusimamia misimamo yake kama kweli inaamini ni mizuri hata kama wananchi hawataipenda.. unaweza kubadilisha tu pale unapogundua kuwa maamuzi ya awali yalifanyikwa kwa taarifa ambazo hazikuwa sahahi.. hii siyo mojawapo ya sababu zilizoifanya serikali ya Kikwete kubadili msimamo wake kuhusu katiba mpya bali ilitaka kufanya maamuzi yanayopendwa na wengi).
Dowans.. kamati kuu ya CCM ilisema Dowans walipwe (Kikwete ndiye mwenyekiti wa kikao kilichoidhinisha Dowans walipwe). Kikwete alipokutana na wabunge wake aligundua kuwa wengi wao hawakuupenda uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu ya Chama chao.. akabadili msimamo tena na kuanza kutuambia kuwa hapendi kuona Dowans inalipwa.
Kwangu mimi nachukilia hivi kuwa ni moja wapo ya dalili za mwanzo kabisa kuwa serikali yetu inaanguka kwa kasi ya ajabu.. serikali isiyokuwa na ujasiri wa kusimamia sheria zake haifai kuwepo madarakani!