Anayejidhani Amesimama angaalie asianguke


ladyfurahia

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Messages
13,908
Likes
1,409
Points
280
ladyfurahia

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined May 10, 2011
13,908 1,409 280
Hello marafiki zangu

Ni siku ingine tena iliyojaa furaha na mihangaiko na mishughuliko yahapa na pale
marafiki zangu leo nimekuja na mada hapo juu isemayo kuwa USIJIDHANIE
UMESIMAMA ANGALIE USIJEANGUKA.

Mara nyingi wanadamu tumekuwa watu wa kujisahau na kudhani kuwa tu pekee
yetu, wala hatuoni kuwa tuko kwa uweza wa Mungu, na tuliumbwa kwa mfano
wake, hivyo yote tufanyayo tumepewa uwezo kwayo. Wakati mwingine watu
au mwanadamu anajiona kuwa yeye ni bora zaidi ya mwingine na anajisahau
kuwa iko siku yeye hatakuwa si bora tena yaani hafai mbele za jamii iliyomzunguka.

Wakati mwingine tumeweza kujifikiria zaidi kuliko kumfikiria au kumwona mwenzako
ni bora zaidi ya wewe ujionavyo. Na wakati mwingine tumeweza fanya mambo
maovu kwa wenzetu tukiona inafaa zaidi kuwafanyia hivyo, kwani tumejiweka
sehemu ambayo sisi ni zaidi ya wengine. Nitanukuu kidogo maneno aliyosema
Hayati Baba wa Taifa. Mwl Nyerere yeye alisema hivi: 'Tutakapokulana na kuumana
na kuona kuwa wewe ni bora zaidi na unafaa utendewe vitu bora zaidi, tutapelkea
kujiita sisi ni bora zaidi ya wengine na kusema hichi ni changu na kile ni chao usiguse
na hapo kutakuwa na tabaka la wao ni wazanzibari na sisi ni wazanzibara......"

mwisho wa kunukuu. Kama nimesahau kidogo hapo mtaniweka sawa wapendwa
marafiki zangu si unajua,

Sasa ikifika hapo utakuta mtu hata kule kusalimiana, kutakiana kheri, kupendana
na hata kuchukuliana kwenye mambo ya jamii kutapotea tena hakutakuwa na
upendo wala kujaliana tena itakuwa hichi ni changu usikiguse wala kuchukua
sasa itafikia hata kuwepo na vita vya wenyewe kwa wenyewe, ndo mana hata
sasa kuna vita vya kidini kwani ilikuwaje mpaka tumefikia hatua hii. ni hiyo hali
kuona kuwa wewe ni bora zaidi ya ndugu yako. Wakati mwingine ule umimi
unafanya uwe mchoyo, mbinafsi na mwenye kujilimbikizia mali na utajiri uoni kuwa
kuna wengine ndugu yako wanakula mchanga na wala hawajaona hata mbilimbi
ya kuweza kujishibisha. Angalia rafiki yangu usiwe mtu mwenye kujiona wewe ni
bora zaidi ya mwingine na kuijiona kuwa umesimama uko vyema kumbe unachungulia
kaburi.
Ndo maana hapo awali nimesema kuwa ajidhanie amesimama angaalie asianguke,
utakwaa kisiki na wala hutaona atakayekusidia kwani ulimdharau mwenzio na kuona si
bora kwako, tumeumbwa tupendane, tujaliane, kuwa wamoja. KUWA MAKINI MY FRENDO

 
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
11,314
Likes
111
Points
145
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined Sep 30, 2009
11,314 111 145
Asante kwa ujumbe murua
 

Forum statistics

Threads 1,273,818
Members 490,485
Posts 30,492,972