Anauliza kuhusu mkopo benki

Anauliza kuhusu mkopo benki

Mtendaji wa kaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
334
Reaction score
60
Naleta swali la ndugu yangu ambaye ni mwajiriwa miezi miwili sasa! mshahara wake ni laki sita na hamsini na ushee hela za kitanzania! anataka kuomba mkopo wa milioni 10 benki yoyote japokuwa mshahara wake unapitia NMB,kama nilivyosema ana miezi miwili tu kwenye utumishi! je anaweza kupata kiasi hicho cha pesa kwa haraka? riba yake ni kiasi gani na kama si benki ni wapi anaweza kupata mkopo huo kwa riba nafuu? Lengo la mkopo ni kununua gari! Nawasilisha
 
Naleta swali la ndugu yangu ambaye ni mwajiriwa miezi miwili sasa! mshahara wake ni laki sita na hamsini na ushee hela za kitanzania! anataka kuomba mkopo wa milioni 10 benki yoyote japokuwa mshahara wake unapitia NMB,kama nilivyosema ana miezi miwili tu kwenye utumishi! je anaweza kupata kiasi hicho cha pesa kwa haraka? riba yake ni kiasi gani na ikama si benki ni wapi anaweza kupata mkopo huo kwa riba nafuu? Lengo la mkopo ni kununua gari! Nawasilisha

Kuna majibu mawili hapo
1. Hawezi kupata mkopo benki yoyote Tanzania mpaka awe amethibitishwa kazini.

2.Ningemshaur akichukua mkopo ajege walau chumba kimoja cha kulala na afannye biashara yoyote maana hataweza kuhudumia hilo gar na hatimae ataliuza kwa bei ya kutupwA.
 
mkuu huyo mtu mwenye ajira ya miezi miwili bado ni trainee au tuseme yuko kwenye probation period ivo kiutaratibu si mfanyakazi kamili na ivo hawezi kupata mkopo benki kwa dhamana ya mwajiri mpaka awe amethibitishwa kazini.
Lazima afanye kazi miezi kadhaa ili athibitishwe kazini...ivo sitegemei kama ataweza kupata huo mkopo bila kudhibitishwa kazini na iyo uthibitisho si chini ya miezi 6 au 12
Pia mwajiri hawezi kumdhamini mkopo wa milioni 10 mwajiriwa wa miezi2 na zaidi ya apo, mshahara wa laki6 ili alipe mkopo ndani ya miaka 3 (36moths au less) kama benki nyingi wanavofanya plus interest itabidi akatwe si chini ya laki 3 na ushee benki, je ataishi vipi kama akinunua gari?

Ushauri wangu ni kuwa awe na subira, baada ya mwaka mmoja mpaka miwili anaweza kuanza kuwaza ivo , vinginevo sijui kama kuna mwajiri au/benki itamsikiliza
 
Back
Top Bottom