Anatishia kuniua kisa ananipenda

Anatishia kuniua kisa ananipenda

belie

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2014
Posts
387
Reaction score
261
Habari zenu jamani, wakubwa shikamoo.

Natumai wote mko fine, ngoja niwape kisa hiki mwenzenu maana nina bahati mbaya kweli na wanaume.

Kuna kaka mmoja tulisoma nae o-level, akaanza kunitongoza kuanzia form 2 akidai ananipenda sana, mimi nilimkatalia kwa sababu kwa kipindi kile sikutaka kujihusisha na mambo ya mapenzi akawa anaendelea kila kukicha haishi vituko. Akawa ananitoa breakfast na kuniletea zawadi kila siku, mara ya kwanza nikawa nakataa, nikikataa wakati wa kurudi home navikuta kwenye begi langu, na nikifungua daftari usiku kusoma nakuta barua na hela nikawa nimemzoea hivyo.

Basi bwana, nikawa kila siku napewa zawadi za nguvu kama viatu, nguo, peni za maana zile na kuna siku aliniletea pure gold chain. Nikawa nitake nini mie nikose, lakini kumbuka nilimkatalia (sasa sijui alikuwa anajua nikimaliza shule nitamkubalia? sijui) basi ikafika mwisho wa mwaka tukafunga shule na kurudi nyumbani, siku hyo aliniletea box kubwa lenye mazaga zaga kibao ikiwemo simu (siemens kipindi hicho) akanambia tutakuwa tukiwasiliana.

Muda ukapita tutakutana tena mwaka mwingine, mambo yakawa yale yale, lakini safari hii naona wivu ulimjaa sana, kwa sababu alikua hataki niongee wala kukaa na mwanaume yoyote yule akiniona nae anamfata yule mwanaume anampiga, mambo yakawa mabaya zaidi kwani ilifika mpaka kwa headmaster wetu wakaniuliza nini chanzo wananitaja mimi.

Baba yangu akawa anaitwa shule kila siku kusikiliza kesi za kijinga, nikawa nachukia sana coz sipendi nishushe heshima yangu hasa kwa mambo ya kipuuzi.

Siku hiyo nikamrudishia vitu vyaake vyote kasoro hela coz nilikua nishazitumia, akakataa kuvichukua nikavitupa chini nikaondoka, kurudi nyumbani nikavikuta alikua amempa dada wetu wa kazi na kudai nilivisahau shule, nikavichoma moto vilivyochomeka na vingne nikaviweka ndani ili ikitokea siku anavihitaji nimpe.

Nikamwambia sitaki mazoea na wewe na usinisumbue kumbe ndo nilikua nazidi kuharibu, nikawa namkwepa shule, nikija home namkuta nje ya geti ananisubiri, yaani alikua king'ang'anizi sijapata kuona.

Nikawa namkwepa hivyo hivyo, tukafika form 4, nakumbuka nilifanya vizuri kwenye mtihani wa mock hivyo kaka yangu aliyeko nje, akaninunulia simu, nilifurahi sana, sasa yeye alivyoniona nayo akajua nimepewa na bwana yangu sijui, kuna siku tulikua tunafanya mtihani mabegi tunaacha kwenye chumba kimoja hivi, yeye alikua wa mwisho kuingia hivyo alivyoenda kuweka begi lake akatafuta begi langu lilipo na kuichukua simu yangu, ikumbukwe vile vitu vyake vingine ikiwemo simu nilibahatika kumrudishia.

Basi bwana, natoka kwenye mtihani sioni simu yangu yaani nilipata shock ya ajabu nikaanza kulia, na kwenda kuwaelezea walimu ofisini, baadae akaja rafiki yake mmoja akaniambia huyo mkaka anataka kuongea na mimi kwenye simu yake, nikapokea na kuongea nae.

Akaniambia naomba tuonane posta sehemu moja hivi ya fast food, nikamjibu sitaki, akanambia kama unaitaka simu yako njoo kama huitaki basi usije, nikawa sina jinsi nikaenda, nilivyofika akaanza kuexpress feeling zake pale nikamwambia mimi nataka simu yangu, usinieleze upuuzi, akasema sikupi simu yako mpaka unikubali mimi nikawa nabishana nae.

Mara akaingia mfukoni akatoa sumu ya panya na kuiweka kwenye kile chakula kilichobaki na kula, mimi nikawa namuangalia 2, akanambia bora afe tu coz simpendi, mara akameza akataka kumeza, nikamwambia basi nimekubali akatema pale yakaisha, nikamwambia sasa simu yangu vipi akatoa simu nyingine nzuri zaidi ya ile akanipa akanambia tumia hii, ile achana nayo, nikamwambia mimi sitaki simu nzuri wala mbaya nachotaka simu yangu, tukagombana pale hakunipa nikaondoka kwa hasira na hakunipa tena simu yangu ikabidi nyumbani nidanganye nimepoteza.


Ngoja nifupishe stori kidogo, ugomvi ukawa mkubwa hadi tukapigana na wakati tunapigana nilikua nimeshika peni mkononi nikamkwaruza nayo usoni, akatoka damu nyingi na likawa jeraha kubwa.

Tukamaliza tukapotezana coz nilienda kusoma boarding so hakuniona tena, sasa lengo la haya yote niliyohadithia hapa ni kwamba juzi kati sijui alipata wapi no yangu na kunipigia, akaniambia bado ananipenda, na akaniambia anakataliwa na wanawake kwa sababu ya kovu usoni nililomsababishia, hivyo lazima nimkubali la sivyo na mimi ataniweka zaidi ya hilo au kuniua kabisa.


Nimelifikiria sana hili, nikaamua nililete kwenu jamani, embu nishauri nifanye nini, maana kuna watu ambao ni familia yake nimeongea nao wameniambia alishauguaguaga ugonjwa wa akili, na alishaiba kwao na kutaka kuchoma moto nyumba yao, na baba yake akampeleka jela apate adabu.

Sasa jamani nafanyaje hapa?

Ushauri please
 
Kuna wakati najiuliza sana maswali kuhusu haya mapenzi halafu nakosaga majibu.

Nini hutokea kiasi cha kumfanya mtu ashindwe kufikiria na kufanya mambo ya ajabu hivyo.
 
anaitwa belie ladies and gentlemen...
habari zenu jaman, wakubwa shikamoo. natumai wote mko fine, ngoja niwape kisa hiki mwenzenu mana nna bahat mbaya kweli na wanaume.....

kuna kaka mmoja tulisoma nae o-level, akaanza kunitongoza kuanzia form 2 akidai ananipenda sana, mimi nilimkatalia coz kwa kipindi kile sikutaka kujihusisha na mambo ya mapenzi akawa anaendelea kila kukicha haishi vituko. Akawa ananitoa breakfast na kuniletea zawadi kila siku, mara ya kwanza nikawa nakataa, nikikataa wakati wa kurudi hom navikuta kwenye begi langu, na nikifungua daftari usiku kusoma nakuta barua na hela.... nikawa nimemzoea hivyo.

basi bwana, nikawa kila siku napewa zawadi za nguvu kama viatu, nguo, peni za maana zile na kuna siku aliniletea pure gold chain. Nikawa nitake nini mie nikose, lakini kumbuka nilimkatalia (sa cjui alikua anajua nikimaliza shule nitamkubalia??? sijui!!!) basi ikafika mwisho wa mwaka tukafunga shule na kurudi nyumban, siku hyo aliniletea box kubwa lenye mazaga zaga kibao ikiwemo simu (siemens kipindi hicho) akanambia tutakuwa tukiwasiliana.

mda ukapita tutakutana tena mwaka mwingine, mambo yakawa yale yale, lakini safari hii naona wivu ulimjaa sana, coz alikua hataki niongee wala kukaa na mwanaume yoyote yule.... akiniona nae anamfata yule mwanaume anampiga, mambo yakawa mabaya zaidi kwani ilifika mpaka kwa headmaster wetu wakaiuliza nini chanzo wananitaja mimi. baba angu akawa anaitwa shule kila siku kusikiliza kesi za kijinga.... nkawa nachukia sana coz sipendi nishushe heshima yangu hasa kwa mambo ya kipuuzi.

siku hiyo nkamrudishia vitu vyaake vyote kasoro hela coz nilikua nishazitumia, akakataa kuvichukua nikavitupa chini nkaondoka, kurudi nyumbani nikavikuta alikua amempa dada wetu wa kazi na kudai nilivisahau shule, nikavichoma moto vilivyochomeka na vingne nkaviweka ndani ili ikitokea siku anavihitaji nimpe. nikamwambia sitaki mazoea na wewe na usinisumbue kumbe ndo nilikua nazidi kuharibu, nikawa namkwepa shule, nikija hom namkuta nje ya geti ananisubiri, yani alikua king'ang'anizi cjapata kuona.

nkawa namkwepa hivyo hivyo, tukafika form 4, nakumbuka nilifanya vizuri kwenye mtiani wa moko hivyo kaka angu alieko nje, akaninunulia sim, nilifurahi sana, sasa yeye alivyoniona nayo akajua nimepewa na bwana angu sijui, kuna siku tulikua tunafanya mtihani mabegi tunaacha kwenye chumba kimoja hivi, yeye alikua wa mwisho kuingia hvyo alivyoenda kuweka begi lake akatafuta begi langu lilipo na kuichukua simu yangu, ikumbukwe vile vitu vyake vingine ikiwemo simu nilibahatika kumrudishia. basi bwana, natoka kwenye mtihani sioni simu yangu yani nilipata shock ya ajabu nkaanza kulia, na kwenda kuwaelezea walimu oficin, badae akaja rafiki ake mmoja akaniambia huyo mkaka anataka kuongea na mimi kwenye simu yake, nikapokea na kuongea nae.

Akaniambia naomba tuonane posta sehem moja hivi ya fast food, nikamjibu sitaki, akanambia kama unaitaka simu yako njoo kama huitaki basi usije, nikawa sina jinsi nkaenda,, nilivyofika akaanza kuexpress feeling zake pale nkamwambia mi nataka simu yangu, usinieleze upuuzi, akasema sikupi simu yako mpaka unikubali mi nikawa nabishana nae, mara akaingia mfukoni akatoa sumu ya panya na kuiweka kwenye kile chakula kilichobaki na kula, mi nkawa namuangalia 2, akanambia bora afe tu coz simpendi, mara akameza akataka kumeza, nkamwambia basi nmekubali akatema pale yakaisha, nkamwambia sasa cm yang vip akatoa sim nyngine nzuri zaid ya ile akanipa akanambia tumia hii, ile achana nayo, nikamwambia mi sitaki simu nzuri wala mbaya nachotaka simu yangu, tukagombana pale hakunipa nikaondoka kwa hasira..... na hakunipa tena simu yangu ikabidi nyumbani nidanganye nimepoteza.


ngoja nifupishe stori kidogo, ugomvi ukawa mkubwa hadi tukapigana na wakati tunapigana nilikua nmeshika peni mkononi nikamkwaruza nayo usoni, akatoka damu nyingi na likawa jeraha kubwa..... ikaendaaaaaa..... tukamaliza tukapotezana coz nilienda kusoma boarding so hakuniona tena, sasa lengo la haya yote niliyohadithia hapa ni kwamba juzi kati sijui alipata wapi no yangu na kunipigia, akaniambia bado ananipenda, na akaniambia anakataliwa na wanawake kwa sababu ya kovu usoni nililomsababishia, hivyo lazima nimkubali la sivyo na mimi ataniweka zaidi ya hilo au kuniua kabisaaaa.....


nimelifikiria sana hili, nikaamua nililete kwenu jaman, embu nishauri nifanye nini, mana kuna watu ambao ni familia yake nimeongea nao wameniambia alishauguaguaga ugonjwa wa akili, na alishaiba kwao na kutaka kuchoma moto nymba yao, na baba ake akampeleka jela apate adabu....

sasa jamani nafanyaje hapa..??? ushauri plz!!!

[h=3]Nahisi bado nampenda[/h] Started by belie, Yesterday 13:4

Habari zenu jamani, mimi ni mgeni kidogo humu, sina muda sana. Nilikuwa napitia tu maongezi na comment za watu na nikavutiwa kujiunga, anyway turudi kwenye point ilionileta hapa.

Nlikua nina mpenzi wangu ambaye alikua workmate wa kaka yangu, akatokea kunipenda na mimi nikampenda tukaanza mahusiano hapo.

Kiukweli nilimpenda sana na nikahisi ndie atakaekuja kuwa mume wangu coz alikua na sifa zote nilizozihitaji. Tulianza mapenzi vizuri sana mpaka nikawa nahisi duniani tumebaki wawili tu mimi na yeye.

Lakini kuna siku alinipa mashaka kidogo. Ikumbukwe kuwa mimi bado nakaa kwetu na nilikua ndo nimemaliza chuo nasubiri majibu nianze na utaratibu wa kutafuta kazi. Kwa jinsi nilivyokuwa nampenda nililazimika kusema uongo nyumbani na kwenda kulala kwake, na hata siku nyingine kutoroka kabisa ili tu niwe na yeye.

Basi bwana, siku hiyo nilienda kwake nikalala huko, sasa asubuhi mapenzi yakazidi akasema haendi kazini anataka tushinde wote ilkuwa siku ya jumatatu. Baadae kama saa tatu akapigiwa simu aende ofisini, ikabidi aende, kufika akapewa barua ya kusimamishwa kazi akarudi akawa upset sana.

Basi nikajaribu kumpoza pale akatulia kidogo sasa baadae akawa ameweka simu kwenye chaji, na mimi nimeweka ya kwangu huku naitumia pale pale, ikawa simu yake ikiita ananiambia nimpe anapokea.

Ikapigwa simu ya mdada ikiwa imeseviwa na picha yake nikampa hakupokea, akaimute, akapiga tena kama mara 5 hivi nikwamwambia mbona hutaki kupokea akanijibu 'aah! msumbufu huyu' akapiga tena akapokea akamwambia nitakupigia badae.

Basi bwana, mimi nikaendelea na zangu, kwakuwa huwa sipendi kugusa simu ya mpenzi wangu nikamuacha na sikumuuliza.

Siku nyingine tukiwa tunaangalia TV mchana nikapitiwa usingizi kwenye kochi, nikalala, simu yangu niliiacha pembeni kidogo na yeye alikua karibu yangu, basi akachukua simu yangu na kuanza kusearch. Sasa kwa sababu simu yangu kila ukiitouch inatoa mlio fulani hivi, nikastuka lakini hakujua kama nipo macho coz nilikua nimegeukia upande mwingine, akaikagua sana siku hiyo na mimi nikamuacha coz nlikua najiamini.

Basi alivyomaliza baadae nikajifanya nimeamka, kushika simu yangu nakuta vitu viko shagalabagala, si unajua mtu chako bana, akitumia mwingine unajua tuu, nikamuuliza umeshika simu yangu akataa huku akiwa amebadilika usoni.

Baadae akaniuliza kuna watu nilikuwa nachat nao kama friends akajua ni mabwana zangu, nikamtoa wasi wasi na kuwapigia kabisa akaamini.

Sasa baada ya hapo nikahisi kuna kitu kinaendelea, kuna siku usiku tunataka kulala namba ile ile ilipopigwa siku ile mara nyingi ikapigwa tena, hakupokea. Nikaona anamtumia message asubuhi yake wakati yupo bafuni nikachukua simu yake na kuangalia nikakuta message zaa ajabu, nikaja kumuuliza akaniambia yule ni rafiki yake tu wamezoeana sana.

Niliumia sana coz huwa sipendi kudanganywa, yakapita hayo akaomba msamaha yakaisha.

Sasa visa vikawa haviishi mara nimpigie asipokee, mara aanze kunambia kama simtaki nimwambie kisa sijampigia wala kumtext wakat na yeye kakaa kimya, kuna kipindi tukaa siku 3 bila mawasiliano yoyote yale, nkaanza kuchoka sasa.

Lakini siku hyo ndo nilichoka zaidi, alikua amesafiri kwenda kwao kwa ajili ya arobaini ya babu yake, akarudi, akataka niende siku ambayo anarudi nikamwambia haiwezekani nitakuja kesho.

Basi kesho nikaenda nikakuta mafuta ya mwanamke hizi lotion za kujichubua na yametumika limebaki kama nusu kopo, nikamuuliza akaniambia ni ya mdogo wake wakati wanarudi akayasahau kwenye begi lake wakati huyo begi lipo sebuleni amelitupa na kuniambia hajalifungua amefika na kuliweka hapo na kulala, na mimi nilienda asubuhi mida ya saa 3 na wakati nafika ndo aliamka kunifungulia geti (shangaeni maajabu hayo) basi nikakaa kimya tu. Nikawa nafanya usafi wa kupanga nguo kabatini nikakuta nguo zimefichwa kwenye mfuko za kike, nikamuuliza za nani akasema za dada ake mmoja hivi aliziacha wakati anahama, nikamwambia mbona siku zote napanga nguo humu sijawahi kuziona na mimi huwa nikipanga nguo natoa kabati zima linakua tupu kabisaa naanza kuwekaa upyaaa.

Akakosa cha kunijibu ndipo nikachukua simu yake baadae kuangalia kwenye picha nakuta picha za utupu za mwanamke na zimetumwa jana yake, na mwanamke mwenyewe ndo yule wa awali aliyekua hapokei simu zake.

Kumuuliza ananiambia kuna rafiki yake alimtumia kitamboo akasema aangalie watoto wa chuo wanavyofanya uchafu wa kupiga picha za uchi, nikamuuliza una uhakika unachokisema ni kweli akajibu ndiooo, nikamuonyesha tarehe siku mwezi na saa iliyotumwa akawa anajing'ata hana cha kujibu mara akawa mkali anataka tugombane, mimi niIichukua vitu vyangu nikaondoka nyumbani nikamwambia 'its over' akajibu 'poaa maisha mema' tukaachana.

Ikumbukwe penzi hili halina hata miezi miwili, lakini imepita mwezi sasa hatuna mawasiliano, na nahisi bado nampenda, kuna siku nimemtumia message hakunijibu, lakini bado nampendaa nawishi arudi na kuadmit mistake zake.

Sijui nyie wenzangu mnaonaje.
Naombeni ushauri.

Nifanyaje
 
Una familia wewe???

Mwanaume anakusubiri getini familia yako ipo kimya???

Unaletewa zawadi familia yako ipo kimya

Kesi ofsn mdingi yupo kimya...

Malezi haya ya kijiditali....

Cha kufanya toa taarifa polisi

Kwanza hiyo ni harrassment
 
Mapenzi ni upofu! Anae ona mapenzi,mapenzi hayamuoni!!

Ndugu wa huyo kijana wameshakushauri vizuri! Ni wewe kuamua kusuka au kunyoa!

Nenda na polisi pia katoe taarifa itakusaidia kwenye record hapo baadae kama huyo mwenzio atakudhuru kwa chochote.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Mrudishe jela kama alivyofanya baba yake kwa kukutishia kukuua. Period!!
 
Una familia wewe???

Mwanaume anakusubiri getini familia yako ipo kimya???

Unaletewa zawadi familia yako ipo kimya

Kesi ofsn mdingi yupo kimya...

Malezi haya ya kijiditali....

Cha kufanya toa taarifa polisi

Kwanza hiyo ni harrassment

yani hapo nimefupisha sana, lakin upande wa familia baba angu alionana na baba ake na wakaongea lakin akaamishia makazi stend ya gari linaponishushia..... walimu nao walimshindwa pamoja na kwao pia,
 
swali kwa wanawake eti ni kweli ndefu inakera na fupi nene ndio nzuri ?

maana ingekuwa fupi nene(maelezo ya kutosha) nimgejibu ila ndefu(story) imenichosha sijamalizia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom