Anataka nimuoe na mtoto wake

Anataka nimuoe na mtoto wake

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2013
Posts
3,097
Reaction score
1,356
Jamani naomba ushauri wa kujenga tu!

STORI NI NDEFU KIDOGO TAFADHALI SOMA UPATE KUNISHAURI;
Kuna mdada mmoja alitokea kunipenda mpaka akanitamkia na kwa vile mimi sikuwa ktk mahusiano wakati huo nilimkubalia ila baada ya muda akaniambia kuwa ana mtoto wa kike ambaye alimzaa baada ya jamaa mmoja kumpa mimba kisha akaitaa nilimhoji sana mazingira ya mimba kukataliwa akasisitiza kuwa aliyempa mimba alimkataa yeye na mimba yake akasema nilikuwa muungwana sikuta kutoa mimba nikaamua kuzaa na kulea mtoto.

Sasa muda ulivyozidi kwenda huku mahaba yakikokelea kama treni la makaa ya mawe tulijikuta kwenye mahaba mazito sana. Ila mimi sikutaka kuwa mvivu wa kufikiri nikazidi fuatilia juu ya mtu aliyezaa naye baada ya muda nikaja kujua kuwa yule mzazi mwenzake alikuwa mchumba wake ambaye alifikia hatua ya kutoa mahari na kabla ya ndoa ndipo akawa amezaa naye mtoto huyo.

Safari ya mahaba haikusimama kwangu njiani humo humo nikaambiwa aliwahi kuishi na huyo jamaa na baada ya muda jamaa alibadirisha mwelekeo akaamua kuoa mtu mwingine. Nili hoji kama hadi ulilipiwa mahari wewe si mke wa mtu akakataa katakata kuwa yeye walikubaliana kuachana yule bwana akaja nyumbani kwao akutaka urudishiwe mahari yake alimua kusamehe akaandika barua kuvunja uchumba.

Kesi ya mtoto, jamaa anaonekana akumkataa mtoto ila walishindwa kuelewana jinsi ya kumtunza mtoto baba mtu anataka mtoto amchukue na mama mtu kakataa kwa madai mwanae atateswa kwa madai yule mke aliyeolewa alisha sema hamtaki huyo mtoto pale. Baba mtu akasema hatatoa ata senti kumtunza mtoto akiwa na mama yake alitia madai kuwa sasa hivi mtoto ana miaka mi 4 akasome boarding awe analipa huko mama hataki.

Sasa picha yangu na huyu mdada ikaanza hivi nikamwambia mbona uko kinyume na maelezo yako ya mwanzo kumbe mtoto baba yake anamtaka wewe tu ndiyo hutaki! Akaanza kulia na kunimbia kuwa yeye ni yatima hana baba wala mama amekuzwa na mjomba wake baada ya wazazi wake wote wawili kufariki.

Anadai eti yeye amekuwa kwa shida sana na hivyo akimwachia mtoto wake atateseka tena kama yeye. Anachodai kwenye mahusiano yetu nimuoe yeye na mtoto wake yaani hataki mtoto wake aende kwa baba yake nikimuuliza vipi mtoto atahudumiwa maana baba yake kagoma hawezi kumhudumia anasema huyu naye tutamhudumia kama wanetu wengine tutakaojaliwa na mola.

Mimi nikiangalia kuhudumia mtoto ambaye ana baba yake tena anakazi nzuri kiukweli napata ukakasi mara ya mwisho wamepelekana Ustawi wa jamii jamaa kakomalia msimo wake.

Naombeni ushauri wenu, stori ni ndefu, ila mwenzenu ndiyo tayari niko kwenye mahaba mazito sijielewi tena.

MAHABA NISHIKE NIFINYANGE NIPIGE GWALA NINYONGE MPAKA NIKUFE KABISA...!
 
Pls nitaomba ushauri chanya! Unaweza ukawa wa kuvunja uhusiano ila uwe unatoa postive solution.
 
Ninachokushauri ndg yangu,husipende kuingilia na kufuatilia sana,mambo ya mwanamke wako na mzazi mwenzake ww hayo hayakuhusu nakushangaa unapata tabu ya nini?,wewe hoa huyo mwanamke wako hata kama huyo mtoto atakuwa pamoja na mama yake,kiubinadamu unawajibika kulea pia huyo mtoto kwasababu huko na mama yake,malumbano ya mwanamke wako na mzazi mwenzake kuhusu huyo mtoto ww hayakuhusu,waache wenyewe wapambane kama wataenda ustawi wa jamii au mahakamani ww hayakuhusu,na kama huyo mwanamke wako anataka aishi na mwanae hapo kwako mpokee na lea huyo mtoto tatizo nini kaka?na mama yake unae na unampenda?,

mambo ya kusema baba yake huyo mtt ana uwezo ww hayakuhusu kabisa,waache wenyewe wapambane mpaka hapo taratibu na sheria zitakapoamua kama mtoto anabaki kwa mama au aende kwa baba yake,kwahiyo nakushauri malumbano yao achana nayo,na story za mwanamke wako kusema huyu mtt yatima pia ww hayakuhusu, kwanini unaumiza kichwa?,kama baba yake yuko anafuatilia mwanae mwache afuatilie husiingilie na wala story za huyo mwanamke wako kusema mtoto ni yatima husisikilize,

kikubwa kwasasa kama huyo mwanamke wako atakuja kuishi na mwanae kwako naomba wapokee na watunze kama mzazi! huyo mtoto hana makosa yoyote,mpaka siku watakapokubaliana na mzazi mwenzake mtoto aende wapi,kwaiyo ww hoa huyo na mwanamke hata kama mwanae atakua nae,siku baba yake atakapomchukua sawa tu,ww utaendelea na maisha na mkeo lkn mambo yao husiyaingilie vyombo vya sheria vipo vitaamua na huyo mtoto husimnyanyapae mtunze hata kama baba yake ana uwezo kwakuwa kuna mgogoro
 
Kama baba mtoto anataka kumpeleka mwanae boding mshauri mchumba wako akubali.Kama vipi jaribu kwa kujifanya wewe ndo unataka kumpeleka boding angalia pumzi zake kama atakubali ndo uanze kumshauri amkuballie baba mtoto wake kumpeleka mwanae bweni.
Lakini waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake.Vinginevyo ukiacha mawasiliano yao yaendelee watakuwa wanakumbushia enzi.Mpende mtoto wa demu wako.
 
Ninachokushauri ndg yangu,husipende kuingilia na kufuatilia sana,mambo ya mwanamke wako na mzazi mwenzake ww hayo hayakuhusu nakushangaa unapata tabu ya nini?,wewe hoa huyo mwanamke wako hata kama huyo mtoto atakuwa pamoja na mama yake,kiubinadamu unawajibika kulea pia huyo mtoto kwasababu huko na mama yake,malumbano ya mwanamke wako na mzazi mwenzake kuhusu huyo mtoto ww hayakuhusu,waache wenyewe wapambane kama wataenda ustawi wa jamii au mahakamani ww hayakuhusu,na kama huyo mwanamke wako anataka aishi na mwanae hapo kwako mpokee na lea huyo mtoto tatizo nini kaka?na mama yake unae na unampenda?,mambo ya kusema baba yake huyo mtt ana uwezo ww hayakuhusu kabisa,waache wenyewe wapambane mpaka hapo taratibu na sheria zitakapoamua kama mtoto anabaki kwa mama au aende kwa baba yake,kwahiyo nakushauri malumbano yao achana nayo,na story za mwanamke wako kusema huyu mtt yatima pia ww hayakuhusu, kwanini unaumiza kichwa?,kama baba yake yuko anafuatilia mwanae mwache afuatilie husiingilie na wala story za huyo mwanamke wako kusema mtoto ni yatima husisikilize,kikubwa kwasasa kama huyo mwanamke wako atakuja kuishi na mwanae kwako naomba wapokee na watunze kama mzazi! huyo mtoto hana makosa yoyote,mpaka siku watakapokubaliana na mzazi mwenzake mtoto aende wapi,kwaiyo ww hoa huyo na mwanamke hata kama mwanae atakua nae,siku baba yake atakapomchukua sawa tu,ww utaendelea na maisha na mkeo lkn mambo yao husiyaingilie vyombo vya sheria vipo vitaamua na huyo mtoto husimnyanyapae mtunze hata kama baba yake ana uwezo kwakuwa kuna mgogoro

Asante mkuu kwa ushauri nitaufanyia kazi.
 
Kama baba mtoto anataka kumpeleka mwanae boding mshauri mchumba wako akubali.Kama vipi jaribu kwa kujifanya wewe ndo unataka kumpeleka boding angalia pumzi zake kama atakubali ndo uanze kumshauri amkuballie baba mtoto wake kumpeleka mwanae bweni.
Lakini waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake.Vinginevyo ukiacha mawasiliano yao yaendelee watakuwa wanakumbushia enzi.Mpende mtoto wa demu wako.

Asante mkuu!
 
Kwanza nikuombe samahani kwa ushauri wangu. Pili nikushauri kuogopa akinamama ambao wana watoto maana huwezi kuoa mtu na mtoto. Tatu mtoto kama ni wa kiume akikua takuchapa tu na ndiye atakuwa chanzo cha kuachana na mkeo. Nne mtoto na mzazi wake ni kidole na pete unaweza kuivua ila huwezi kuiacha aslani, nina maana wewe tunza lakini mwisho wa yote atarudi kwa baba yake tu
 
Duuh...! Huyu mtoto ni wakike hilo la kurudi kwa baba yake sina mgogoro nalo shida why should i agree to take someone responsibilities jamaa ana uwezo wake but amegoma kwa mashart aliyoyaweka... Hapo sasa.
 
Ndugu yangu hawa akinamama hututambia pale mahaba yapogeuka shubiri, wanatamba kuwa asibabaishwe atamtunza mtoto wake hata kwa kuza K. Lakini hukimbilia ndugu na jamaa kuomba misaada bila aibu. Mtoto anatunzwa na baba mtu si baba wa kufikia wamjoba, mashangazi au mama wadogo. Achana naye huyo kwa nini ugharamikie mtoto ambaye baba yake yupo hai? Tell her straight kuwa akubaliane na matakwa ya mzazi mwenzie. Ila kumbuka ukubwani ni bakora nusu kwa vile ni wa kike. Angalikuwa wa kiume nisingekushauri uoe (enyailya) maana urafiki na ndoa ni vitu vipo parallel kimahesabu
 
Mtoto asiende boarding bado mdogo sana.Pia asiende kwa baba yake,mama wa kambo atamtesa.Wewe kijana,muoe huyo dada na mlee mtoto.Je ungekuwa wewe ungejisikiaje kuachwa kwa ajili ya mtoto?Mpende mtoto,mfanye mwanao.HABARI YA BABA YAKE,ACHANA NAYO!UNAFATILIA ILI IWEJE?MBONA KUNA WANAUME WENZIO WANALEA HADI WATOTO WATATU,TUMIA BUSARA!
 
Duuuh! Jamani mimi ata sielewi what to do...!
 
Kiukweli mpenzi wangu analalamika sana, analia mno anasema maneno ya kuumiza eti bora angekuwa na mama, dada, kaka au baba anasema isingekuwa shida pakumpeleka mtoto wake...! Hii kitu inaniumiza sana mkuu licha ya kwamba ushauri nauona makini...!
 
Mtoto asiende boarding bado mdogo sana.Pia asiende kwa baba yake,mama wa kambo atamtesa.Wewe kijana,muoe huyo dada na mlee mtoto.Je ungekuwa wewe ungejisikiaje kuachwa kwa ajili ya mtoto?Mpende mtoto,mfanye mwanao.HABARI YA BABA YAKE,ACHANA NAYO!UNAFATILIA ILI IWEJE?MBONA KUNA WANAUME WENZIO WANALEA HADI WATOTO WATATU,TUMIA BUSARA!

Kiukweli mpenzi wangu analalamika sana, analia mno anasema maneno ya kuumiza eti bora angekuwa na mama, dada, kaka au baba anasema isingekuwa shida pakumpeleka mtoto wake...! Hii kitu inaniumiza sana DADADori shida kuna wakati nawaza sioni sababu ya kumlelea mtu aliyepo mtoto wake bila sababu ya msingi.
 
Last edited by a moderator:
hizi stori izingine jamani acheni tu mbona zikifunguka leshu tutapona hapa jamvini
 
Back
Top Bottom