Anataka kulipa fadhila ya mapenzi wakati mwenzake ameshaoa nae kaolewa

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,007
5,446
wana jamvi habari za HARDTALK....

kuna jambo nataka kushare na ninyi hasa wanawake waniambie nini huwa wanafikiria.

nina rafiki yangu alikua very decent na mtu mwenye misimamo hasa swala kuwa na mpenzi tukiwa wanafunzi, mara nyingi tulikua tukizinguana kwakua mimi ujana (utoto) ulikua unanisumbua sana kwakua nilikua napenda sana mademu wakati tunasoma.
ofcoz mi nilikua karibu saana na mshakaji nikamshawishi walau na yeye apate demu kuliko kujikaza kama atapewa tuzo ya u bachela,
wakati ukafika tukiwa tupo advance tukajikuta tupo team ya watu ka wanne sisi wakiume na wanawake wawili, ghafla yeye akaanza mahusiano na mmoja wa wale wanawake penzi likakolea balaa mpaka kumtambulisha kwa mama yake na dada yake na kumhonga vitu hata vya nje ya uwezo wake kwakukolea.
baada ya miezi miwili yule demu kabadilika hataki hatakuongea nae anamsonya, anamfokea nakumwambia yeye na jamaa si wapenzi na hawajawahi kua wapenzi.
jamaa aliumia saana akadhoofika kwasababu hakujua chanzo cha kubadilika hivo ni nini, wakati walikua marafiki wazuri na kisha wapenzi wazuri tuu.
tukamaliza shule jamaa akijihisi pengine kuna kasoro akonayo ikamfanya yule demu amkane wapi yule demu hakumwambia hata.... japo nilimwambia kwasababu hakulala (sex) nae ndio maana demu alimkataa... basi maisha yakaendelea.

Baada ya miaka karibu kumi kupita yule demu akiwa ameolewa na anawatoto na jamaa ameoa anawatoto, yeye anakuja kumbembeleza jamaa eti amsamehe kwakua alimuumiza saana wakati ule na hata ikiwezekana penzi yupo tayari kumpa ili asemehewe. mshikaji wangu kagoma hataki hata kupokea simu yake lakini mwanamke anakomaa hadi kwa ndugu wa jamaa aombewe msamaha.

nikamuuliza vip kwani unatatizo na mume wako akasema hapana tena mme wake anahela na yeye anahela na wanaishi vizuri tuu tatizo linalo msumbua ni hatia aliyonayo juu ya alichomfanyia rafiki yangu hivo anaomba nimsaidie apate hio nafasi ashiriki nae japo mara moja hatia imtoke.......mhhh hapa nimebaki na maswali wallah ndoa zina mambo!!!!

sasa kina mama/wanawake mtujuze hili la HATIA na kulipa fadhila je ni kweli mna moyo wa kulipa fadhila kiasi hiki au ni kwa huyu tuu??
 
Kumbe wanakuwaga na hatia!? Sasa mtu kachoshwa na mitoto kadhaa ndo analeta makombo! Pumbav sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom