Anasema hawezi kwenda kujieleza Mbele ya Kamati ya Bunge bila kuandikiwa barua, Je yeye alivyowaita

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
" Hilo suala la Mimi kuitwa kwenye Kamati [ ya Haki , Kinga na Madaraka ya Bunge ] Mimi nimelisikia na kulisoma kwenye magazeti. ..... sijaletewa barua rasmi ". Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Hii ni hoja ya msingi Sana. Nakubaliana na ndugu Makonda. Lazima kuwe na wito rasmi Ndio uitike wito.

Bahati mbaya Sana mlalamikaji alitumia njia hiyo hiyo kutuhumu watu hadharani na kuwaita watu waende polisi. Gwajima alipewa barua? Manji alipewa Barua? Mbowe mumempa barua? Wasanii wamepewa barua? Si waliitwa kwa kutumia TV?

Kweli Mkuki wa Nguruwe.

Bunge litamwita Mkuu wa mkoa wa Dar na mwenzake DC wa Arumeru kwa wito wa kisheria ( Amri ya kufika mbele ya Kamati). Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ina mamlaka ya kimahakama na inaweza kumfunga mkaidi.

Sasa nasikia wameagizwa wasiitikie wito. Tutaona kati ya ubabe na sheria mshindi Nani.
 
Back
Top Bottom