Mkurugenzi TANESCO atakiwa kujieleza mbele ya Kamati ya Bunge (PIC)

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imewatimua vigogo wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi wa shirika hilo.

Mbali na hilo, kamati hiyo imewataka vigogo wa shirika hilo kuandika barua kueleza ni kwanini viongozi wakuu wa shirika hilo wameshindwa kufika katika kikao hicho cha kamati licha ya taarifa ya wito kuwafikia tangu Januari 5, 2023.

Akizungumza leo Jumatatu Januari 23, 2023 jijini Dodoma, mwenyekiti wa kamati hiyo, Jerry Silaa amesema kitendo cha Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi kutofika katika kikao hicho bila taarifa ni dharau kwa Bunge.

“Barua ya kuwaita iliandikwa tangu Desemba 2022 lakini wao waliipata Januari 5, 2023 hakusema chochote leo wanakuja baadhi ya watumishi, hii ni dharau kwa Bunge,” amesema Silaa.

Kwa upande wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Silaa amesema licha riba za mikopo katika taasisi za fedha kupungua baada ya BoT kufanya usajili wa taasisi zinazotoa mikopo lakini kwa taarifa walizonazo kuna gharama nyingine anawekewa mteja.

“Inawezekana mtu akaambiwa gharama za mkopo ni Sh1 milioni, ukichukuwa gharama za mikopo, riba na gharama nyingine inarudi pale pale na wananchi wanaumia,” amesema mwenyekiti huyo wa PIC.

Amesema wameitaka BoT kujielekeza katika maeneo mengine ya mtandao, miamala ya fedha ya simu na kuhakikisha wanakuwa na mfumo bora wa malipo ya kieletroniki, mfumo ambao unahusisha mabenki, miamala ya simu na watoa huduma wengine.

Silaa ameongeza kwamba BoT inatakiwa kuhakikisha gharama za mikopo na riba zinakuwa za chini kwa ajili ya kutomuumiza Mtanzania wa chini.

MWANANCHI
 
kwa afrika unaposikia kiongozi/ Viongozi yeyote wa taasisi anatakiwa ajielezee inakuwa na maana kuwa

ATOE MAELEZO YA KUJITETEA TU BASI NA ATAKUWA KASHAMALIZA KESI YAKE/ KESI YAKE IMEISHA.

#MUSISHTUKE_WALA_NINI
 
Tupo Tanzania Lakini.
Kiongozi wa Pwani
na Tuna siasa za Kistaarabu.
Maelezo ya Afrika tena?
hashtagi pongezi
 
Mheshimiwa Slaa ana moyo wa utetezi kwa watanzania hata sauti yake inatushuhudia. Siku zote Slaa hapendi watanzania waonewe. Siku moja Mungu atuinulie Slaa awe kwenye nafasi moja kubwa katika taifa letu. Amen
20230111_230219.jpg
 
Naona sawa tu maana wanatunyanyasa sana wateja wao na wengine kama wapo waiteni wasipo kuja timuwa.
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imewatimua vigogo wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi wa shirika hilo.

Mbali na hilo, kamati hiyo imewataka vigogo wa shirika hilo kuandika barua kueleza ni kwanini viongozi wakuu wa shirika hilo wameshindwa kufika katika kikao hicho cha kamati licha ya taarifa ya wito kuwafikia tangu Januari 5, 2023.

Akizungumza leo Jumatatu Januari 23, 2023 jijini Dodoma, mwenyekiti wa kamati hiyo, Jerry Silaa amesema kitendo cha Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi kutofika katika kikao hicho bila taarifa ni dharau kwa Bunge.

“Barua ya kuwaita iliandikwa tangu Desemba 2022 lakini wao waliipata Januari 5, 2023 hakusema chochote leo wanakuja baadhi ya watumishi, hii ni dharau kwa Bunge,” amesema Silaa.

Kwa upande wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Silaa amesema licha riba za mikopo katika taasisi za fedha kupungua baada ya BoT kufanya usajili wa taasisi zinazotoa mikopo lakini kwa taarifa walizonazo kuna gharama nyingine anawekewa mteja.

“Inawezekana mtu akaambiwa gharama za mkopo ni Sh1 milioni, ukichukuwa gharama za mikopo, riba na gharama nyingine inarudi pale pale na wananchi wanaumia,” amesema mwenyekiti huyo wa PIC.

Amesema wameitaka BoT kujielekeza katika maeneo mengine ya mtandao, miamala ya fedha ya simu na kuhakikisha wanakuwa na mfumo bora wa malipo ya kieletroniki, mfumo ambao unahusisha mabenki, miamala ya simu na watoa huduma wengine.

Silaa ameongeza kwamba BoT inatakiwa kuhakikisha gharama za mikopo na riba zinakuwa za chini kwa ajili ya kutomuumiza Mtanzania wa chini.

MWANANCHI
Mbona habari zimejikanganya hizi?
Umeanza na Tanesco ukaishia na Bot, why why why wyh?
 
Back
Top Bottom