Anasema anatafuta dawa amnase huyu mwanaume

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kuna vibwanga duniania aisee, unaweza ukawaza mpaka usipate jibu

Huyu mdada akiwa na umri wa miaka 20 aliwahi kutongozwa na mwanaume mwenye umri wa miaka 38 hivi,lakini huyu dada alimkataa kwa kumpa sababu kuu mbili

1. Sababu ya Kwanza unanizidi umri mbali sana, yaani inapaswa wewe uwe mzazi wangu

2. Una familia yako na mke wako, siwezi kuingilia familia yako

Basi mwanaume akawa ameridhika na majibu ingawa awali binti alikuwa anapokea vizawadi na hela ya matumizi kabla hajampa jibu la hivyo

Binti akawa ameingia kwenye mahusiano na mwanaume mwingine miaka 25 hivi mpaka wakaoana wakaenda kuishi mkoa mwingine. Baada ya miaka miwili binti karudi ana mtoto na maisha yamempiga hatari,hadi muda mwingine anawaza ajiuze ili mwanae ale na avae maana baba yake alisha toweka akaingia mikoani huko

Sasa binti amekuwa anatumia njia za kuomba watu wamwambie huyu mwanaume mwenye familia yake yule ya mwanzoni wawe kwenye mahusiano. Mbaba anamwambia siwezi kuwa na wewe maana umewahi kunikataa na sababu nzito

Binti anadai alikuwa hana akili kipindi hicho, hata hivyo mbaba amemkataa ila cha ajabu binti anawambia watu mtaani kuwa anatembea naye. Cha ajabu zaidi anawasiliana na mganga mmoja wa kienyeji ili ampe dawa amnase mbaba wa watu na kuwauliza wanawake wengine wampe dawa au njia ya kumnasa huyo mbaba awe chini yake

Mbaba anafanya juu chini mambo hayo yaishie mitaani yasije yakamfikia mke wake yakaleta mtafaruku kwenye familia yake

Yaani mambo yanaenda kwa kasi kwenye hii dunia. Na nyie wanaume mkome kutongoza ovyo
 
Sioni ajabu maan nyinyi wanawake korabo na mambo ya kishetani hayajaanza leo!! Mnamuenzi mhasisi wenu Eva sijui ndo hawa!!

Jamani kina adamu tunamsaidiaje baharia mwenzetu..?
Mi naona amkubalie tu kwa kabla hajatiwa kiganjani
Hahahaha:Hatari
 
Na wanawake wajifunze kuwa na akiba ya maneno.

Kila siku nasema hii battle ya opposite sex wanawake hatuwezi shinda unless we are a step ahead kiakili.

Men have every advantage over us. They are born hunters. They know their prey very well and they always have smart tactics up their sleeves to make sure they corner their prey.

And they rarely have anything to lose.
 
Majuto ni mjukuu,yeye kipindi kile angemkubali hayo yote yasingetokea,

Mkataa pema pa baya pana mwita
 
Sioni ajabu maan nyinyi wanawake korabo na mambo ya kishetani hayajaanza leo!! Mnamuenzi mhasisi wenu Eva sijui ndo hawa!!

Jamani kina adamu tunamsaidiaje baharia mwenzetu..?
Mi naona amkubalie tu kwa kabla hajatiwa kiganjani
dah! Adam mwenzetu hawezi kudhurika jambo la msingi ni awe mbali na huyo mwanamke, asiwe na ukaribu naye Wa aina yoyote.

Hicho kimwanamke kitaishia kuvuliwa chupi tu huko kwa mganga.
Maana waganga nao hawachelewi Ku take advantage?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wanawake wajifunze kuwa na akiba ya maneno.

Kila siku nasema hii battle ya opposite sex wanawake hatuwezi shinda unless we are a step ahead kiakili.

Men have every advantage over us. They are born hunters. They know their prey very well and they always have smart tactics up their sleeves to make sure they corner their prey.

And they rarely have anything to lose.
Smart woman!
 
Back
Top Bottom