Anasa zawanyima mishahara wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anasa zawanyima mishahara wabunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Feb 14, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  WAKATI mjadala wa nyongeza ya posho za wabunge ukiwa umepamba moto nchini, kwa wananchi na makundi mbalimbali wakipinga hatua hiyo, wabunge wengi wa nchini Uganda wanaambulia patupu mwisho wa mwezi kutokana na kukatwa fedha nyingi za mishahara yao kulipa madeni yao.

  Wabunge hao wanadaiwa kuwa walikopa fedha nyingi wakati wa kampeni za kuwania nafasi hiyo na hivyo fedha wanazopata hulazimika kukatwa ili kufidia madeni hayo. Mikopo hiyo imeelezwa kuwa wamekuwa wakiitumia kwa maisha ya kifahari kama kununua magari na nyumba za kifahari.


  Habari kutoka kwenye Tume ya Bunge hilo, zilieleza kuwa wabunge takriban 50 huondoka na chini ya shilingi milioni moja mwisho wa mwezi, kiasi kilichoelezwa kuwa ni kidogo sana. Kutokana na ukata unaowakabili wabunge hao, hulazimika kuvizia semina, warsha na safari za masomo zinazofanyika ndani na nje ya Uganda ili kuweza kukabiliana na ukali wa maisha unaowakabili.


  Mmoja wa makamishna wa tume hiyo ya Bunge, Eliya Okupa, aliripotiwa akiwaambia wenzake kuwa zaidi ya wabunge 70 mwisho wa mwezi wanajikuta hawana cha kupeleka nyumbani kutokana na kiasi kikubwa cha mishahara yao kupelekwa kwenye kulipia madeni. Okupa alisema wabunge wengi mbali na kudaiwa fedha nyingi kutokana na mikopo, pia hawana nidhamu ya matumizi ya fedha, kuishi maisha ya kifahari kwa kuwa na nyumba na magari ya kifahari na kusaidia wananchi maskini kwenye majibo yao.


  "Kwa Uganda mbunge anaonekana kama benki ndogo ambayo jamii imewekeza matumaini kwake kwa maisha yao ya baadaye. Kuna asilimia takriban 83 ya vijana ambao hawana ajira...watu wanawaona wabunge kuwa ni sehemu ya maisha yao," alisema Okupa. Kamishina huyo alishauri kutolewa kwa elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha kwa wabunge wa sasa kwani tatizo hilo ni kubwa na la kwanza kutokea katika Bunge hilo.


  Awali wabunge hao kila mmoja alipata mkopo wa sh milioni 103 kwa ajili ya kununulia gari. Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Kupambana na Rushwa Uganda, Cissy Kagaba, alisema wabunge hao wamekuwa wakitumia fedha nyingi kwa rushwa na kwamba hali hiyo haishangazi kwa wabunge hao kutokana na wengi wao kutumia sh milioni 20 kununulia magari na zilizobakia huzitumia kwa rushwa, kauli ambayo ilipingwa na Mwenyekiti wa Chama cha NRM, David Bahati.


  Mbunge wa Buyaga, Barnaba Tinkasiimire, alisema yeye amewekeza katika mali isiyohamishika ambayo humuingizia sh milioni 12 kutoka kwa wapangaji wake 44.
   
 2. K

  Kwaito Senior Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wabunge wananiboa sana kujifanya wao ni exceptional!kabla ya kuwa wabunge, howe were managing?shwain kabsa
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,229
  Trophy Points: 280
  na anasa kweli ingawa wenyewe wanaita"kupanda kwa maisha dodoma", maisha yamepanda dodoma tu? tena kwa wabunge tu?
  au wanapodai wana wategemezi, mtanzania gani asiye na wategemezi?

  wamekera kwa kweli
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nashangaa wabunge wengi wamenywea sana, ni dalili walikopa sana kutegemea kwamba kutakuwa na ziada ya malipo ya kuzunguka vitini wakishachoka kusinzia, mambo yamewawia magumu, na mikopo ingali pale pale, wanachoambulia kunyang'anywa mashangingi kufidia madeni.
   
Loading...