Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,946
- 38,656
Wapendwa Great Thinkers.
Nchi yetu inapitia kipindi kigumu sana. Nimewawekea taarifa ya video hapa ili mpate taarifa kamili.
===================
Anaandika Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
Usiku wa kuamkia leo, tarehe 5/9/2025 watu “wanaojulikana” wamechoma moto gari la Mchungaji Melckisedeki Iromba wa Usharika wa Nyakasimbi, Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Gari hilo limechomwa kijijini Nyakasimbi, Kata ya Nyakasimbi, Wilaya ya Karagwe.
Uongozi wa juu wa Dayosisi ya Karagwe ukiwa katika kikao cha kujadili jambo hilo, viongozi wa Wizara wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa na mkewe. Walipitla kusalimia wakiwa njiani kuelekea kwenye kampeni zao.
Walipofika ikawa ni kama mbuzi kufika kwa mzua supu. Tukalalamika kwa kishindo kikuu juu ya kitendo cha gari la Mchungaji kuchomwa moto. Pia tukalalamika kwa kishindo chote juu ya matukio ya ubakaji kwa watoto wadogo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, ndg Bashungwa alifika eneo la tukio. Lakini hakuonesha kuchukua hatua kwa tukio hilo la kigaidi