Anaomba ushauri

cheguevara

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,348
649
Habarini wasomi,
Ninajamaa yangu anataabika sana baada ya kuamua kuuza nyumba yake akasome kuna mbunge mmoja wa chama tawala alimwambia atainunua wakakubaliana bei 30mln,mbunge akaomba namba ya akaunti akapewa na kuahidi kesho angeweka hiyo hela,baada ya hapo zikaanza chenga akawa anamuwekea 1mln kila mwezi na baadae akamblock kwenye simu na meseji alipopatikana akasema alikuwa nje ya nchi hivyo amtumie tena akaunti aweke akatumiwa chenga tena zikaanza,juzi kamwambia atafute mtu amuuzie halafu amrudishie hela yake,ndugu yangu katafuta wateja wale wa mwanzo wanamshusha bei hadi 15mln nayeye tayari keshafanya maandalizi ya kwenda shule na pia alikuwa kesha andaa sehemu ya kuanzisha biashara ya duka la dawa mhimu na alikuwa amehakikishiwa na huyo mbunge afanye maandalizi ya pango na vifaa akiwa tayari atampa hiyo hela mapema,je achukue hatua gani huyu ndugu yangu kwani tayari ana madeni ya gharama za uandaaji wa sehemu ya biashara?
 
Makubaliano ya awali waliingia kwa njia gani? (Maandishi&kwa mdomo) kama waliingia mkataba wa kuuziana na upande mmoja ukashindwa kutekeleza vipengele vya mkataba itapelekea mkataba wa mauziano kuvunjika na upande utakaokuwa umeathirika kwa kitendo hicho cha kuvunjwa kwa mkataba unaweza ukadai fidia kwa madhara yote yaliyotokea. Kwa upande wangu nnamshauri huyo kijana asmrudishie kwanza huyo mbunge pesa yake na ajaribu kumtafuta legal officer au kituo cha sheria kilichopo karibu ili aeleze nature ya makubaliano hayo na mwisho wa siku atapewa njia sahihi za kufuata ili adipate madhara kwa kitendo kilichotokea. Asante
 
Mkuu,

Kwa mujibu wa sheria ya mikataba kuna kitu kinaitwa matokeo ya kushindwa kutekeleza jukumu/ majukumu yaliyowekwa katika mkataba. Katika matokeo hayo Kuna vitu vitatu huwa vinaangaliwa kama itakavyojadiliwa hapa chini.

•Pale ambapo wahusika katika mkataba wanaamua kuwa muda uwe muhimu katika kutekeleza jukumu/majukumu yake katika mkataba. Hapa ukishindwa kutekeleza ahadi yako huo mkatabap unaweza kubatilishwa kwa hiari.

•Pale ambapo muda siyo muhimu sana katika mkataba yani hamkupanga kuwa mkataba utekelezwe ndani ya muda uliopangwa. Hapa mkataba hauwezi kubatilishwa.Hivyo una haki ya kudai fidia kwa hasara yoyote iliyojitokeza.

•Pale ambapo umeendelea na mkataba ambao ungewezwa kubatilishwa kwa kutokufanyika kwa wakati uliopangwa na ukapokea ahadi kwa muda tofauti hapa hauwezi kudai fidia isipokuwa tu kama ulimpa taarifa (mtoa ahadi)ya kukubali kutekelezwa mkataba huo. Hapa unaweza ukadai fidia.

Kwa maoni yangu nenda mahakamani ukadai fidia kama kweli kuna hasara yoyote iliyotokea na hiyo hasara iliyotokea ujiandae kuithibitishia mahakama kuwa kweli kuna hasara umepata yani uwe na hoja nzito za kutetea utakachokisema mahakamani. Kwa lugha nyepesi uwe na hoja nzuri na zenye mashiko kuishawishi mahakama kuamini na kukubali unachokisema.

•Mind you, "he who alleges must prove"

Utakaposhindwa kuthibitisha kuwa kuna hasara iliyotokea kwa upande wako hakika hapo unajua kitatokea nini.

Mwisho, ushawishi wako ndiyo unapelekea upate ushindi au ushindwe kesi.
 
Back
Top Bottom