Anaomba ushauri juu ya mahusiano haya

Anaomba ushauri juu ya mahusiano haya

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,477
Reaction score
21,025
ANAOMBA USHAURI:

Mimi ni kijana wa miaka 29. Baada ya maisha kunipiga kwa muda mrefu kutokana na kutokuwa na msaada wa familia na kutokuwa na kazi na kuishia kuwa 'mishen town' tu, miaka mitatu iliyopita nilimpata mama mmoja wa miaka 45 (sasa ana miaka 48) ambaye alikuwa mjane ila mambo safi (hela anazo). Mapenzi yakanoga kiasi tukaamua kufunga ndoa. Ndoa yetu haikuhusisha watu wengi sana zaidi ya marafiki wachache tu, hata familia zetu hazikuhusishwa kutokana na hali yenyewe (kijana anaoa jimama). Huyu mama ana binti mwenye miaka 24 kwa sasa. Kifamilia, huyo ni binti yangu kwa kuwa mimi ni mume wa mama yake.

Kilichonitatiza sasa ni hiki: Miezi kadhaa iliyopita, binti amekuja kutuambia kuwa amepata mwanaume anayempenda wa kumuoa na kwa kuwa vijana wa siku hizi ni wasumbufu kwenye mapenzi wakiwa na vijana wenzao, amemkubali mwanaume huyo japo ni mtu mzima sana (anakaribia miaka 60). Kwa kuangalia hali yetu (mimi ni kijana na mama yake anaelekea uzee), tulishindwa kumkatalia.

Basi siku ikapangwa mwanaume aje kujitambulisha ili process nyingine zifuatwe. Kilichonishtusha sana siku ilipofika: Mwanaume huyo ni baba yangu mzazi ambaye kwa sasa anaishi mwenyewe kwa kuwa mama yetu alifariki miaka 10 hivi iliyopita. Baba yangu amekuwa akiishi mwenyewe tu, na kwa kuwa kipato chake kwa muda mrefu kilikuwa ni cha chini, hatukuwa na ukaribu sana kwani kila mmoja alikuwa anatafuta kivyake. Hata huyu mama (mke wangu) hajawahi kukutana naye.

Najiuliza: Niipinge hii ndoa? Kwa kuwa kama wakikubaliana kufunga ndoa, basi nitakuwa baba mkwe wa baba yangu mzazi. Na pia huyu binti mbali ya kuwa ni binti yangu (kwa huyu mama yake), pia atakuwa mama yangu (kwa baba yangu mzazi). Vipi wakizaa mtoto, nitamuitaje, mdogo wangu au mjukuu wangu?

Nimechanganyikiwa sijielewi, tafadhali naomba ushauri wenu!







copied and pasted from somewhere
Nawasilisha
 
Akiipinga ndoa huyo Binti atampiga yeye dudu?
 
Amshauri huyo binti wakafunge ndoa na huyo babu yake kwa siri (wasiwajurishe wao) kama yeye alivyofanya na bibi yake.
 
Imekuwa vizuri umekiri kuwa umekopi na ku paste maana huko tulishamshauri sana. Cha muhimu ungeleta kuwa kama ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Wat goes around comes around. Imeshatokea utafanyaje sasa imeshatokea kubali 2

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Amshauri huyo binti wakafunge ndoa na huyo babu yake kwa siri (wasiwajurishe wao) kama yeye alivyofanya na bibi yake.

teh teh hata namimi nilifikiria hivyo hivyo
 
Pamoja na ku copy na ku paste ningekuwa mimi ningempa baba huyu mama(Mke wangu) halafu mimi ningeoa mtoto(mchumba wa baba) mchezo kwisha age difference sorted.
 
Back
Top Bottom