Anaomba ushauri afanyeje?

Lisa

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
1,549
1,074
kuna rafiki yangu anamatatizo katika ndoa yake, ameolewa ana miaka mitatu sasa, anadai mumewe amebadilika sana baada ya kupata kazi yenye kipato kikubwa, kununua gari na kujenga nyumba ambayo wanaishi sasa, anadai mume kwa sasa hashindi tena ndani kama zamani, hamshirikishi tena katika maamuzi ya kifamilia kama zamani, na akimuuliza anakuja juu sana, imefikia stegi hampi hela ya matumizi na akimpa 10000/= basi ni kwa wiki nzima asiulize tena kuhusu pesa ya matumizi , ihali ndani hakuna kitu chochote.mume huyu anatoka kazini saa 9, lkn anafika home saa 5 usiku. na hanywi pombe anakuwa wapi?
wana JF ambao mnajua nn maana ya ndoa , na uchungu wake . naomba mchango tafadhali, na pia wale wenye kejeli tafadhali naomba msichangie maana ni muhimu sana mpk nimeleta hapa kwenye jukwaa hili.
 
Jamani ndio ndoa hizo zinahitaji uvumilivu sana ..lakini hivi kwani wanaume wengine wakipata hawatulii hata kidogo
Pesa zinawasha mifukoni mwao ..kesho nitakuja na ushauri mzuri hapa sasa kichwa kimechoka sana
 
Akae chini afikirie kwa nama yeyote ambavyo amesaidia au anasaidia kumsukuma nje mmewe! Ninauhakika anachangia, kama halipo basi, hiyo ndume imepotoka! Ushauri toka kwa wazazi, marafiki wa karibu unahitajika!
 
.Kanunua gari na kajenga nyumba baada ya kupata kazi yenye kipato kikubwa....hapo bado pana hitaji ufafanuzi...je kama moja kati ya hivyo viwili au vyote ni mikopo?,,,..maana hiyo kazi yenye kipato kikubwa yaweza kuwa ndio ilikuwa thamanisho lenyewe, lililomfanya mzee akopesheke.. mama maendeleo huambatana na maumivu .

Kupungua kwa pesa ya matumizi inaweza kuwa ni moja ya njia ya kujibana ili kufidia deni.Anakuamini bado huyo na anakutegemea ndio maana anajua hata akikuachia laki bado mambo yataenda hii inategemea mlikuwa mnaishi vipi tangu mwanzo.

Kama anakupatia hela ya matumizi na nyumbani anarudi,hamna ubaya,..amini nakwambia mawazo ya kimaendeleo hupatikana kwenye social areas ambazo ni baa au sehemu nyingine zenye michanganyiko ya watu,na sio lazima uwe mlevi.Kukaa ndani na kujitengenezea dunia yako peke yako utajikuta uko pale pale au utarudi chini. Mwisho tumia ile mbinu yako ya siku zote muulize mwenzio kwa utaratibu kuhusu mabadiliko hayo,.huku ukionyesha nia ya kumsaidia kulipa kama ni mkopo ,nadhani jibu zuri litatoka kwake
 
Mie naona akae na mume wako na waongee kuhusu hayo matatizo... na kama asipompa sababu za maana, mie naona bora atafute kazi ya kumshughulisha ili asikae ndani ataumia zaidi, avumilie labda mme wake anamatatizo na hapendi kuongelea ... hawa wanaume ni tabu sana...specially when they dont wanna talk about their problems... frankly how do we supposed to know if you dont tell us ur problems?
 
Asante kwa ushauri, na yeye amesoma haya mashauri yenu ila anasema amejitahidi sana kuongea naye kwa upole lkn anakuja juu mpk majirani wanasikia , anajisikia aibu sana, na kuna wakati wakikosana ndani basi ujue asubuhi atamwacha hampakii kwenye gari lake, inabidi mke akapande basi. inamuuma sana na hajui afanye nn.
 
kuna rafiki yangu anamatatizo katika ndoa yake, ameolewa ana miaka mitatu sasa, anadai mumewe amebadilika sana baada ya kupata kazi yenye kipato kikubwa, kununua gari na kujenga nyumba ambayo wanaishi sasa, anadai mume kwa sasa hashindi tena ndani kama zamani, hamshirikishi tena katika maamuzi ya kifamilia kama zamani, na akimuuliza anakuja juu sana, imefikia stegi hampi hela ya matumizi na akimpa 10000/= basi ni kwa wiki nzima asiulize tena kuhusu pesa ya matumizi , ihali ndani hakuna kitu chochote.mume huyu anatoka kazini saa 9, lkn anafika home saa 5 usiku. na hanywi pombe anakuwa wapi?
wana JF ambao mnajua nn maana ya ndoa , na uchungu wake . naomba mchango tafadhali, na pia wale wenye kejeli tafadhali naomba msichangie maana ni muhimu sana mpk nimeleta hapa kwenye jukwaa hili.

Pole dada yangu, huyo mshikaji kapata jipapa la town ndilo linamfanya haoni wala hasikii, nashauri uwaone wazazi wake ili wamuite kumuliza kulikoni na kumkanya hio tabia aiache la siyo gonjwa linakuja au kama kuna watu wazima anaowaheshimu awaambie ili wamuonywe.
 
Asante kwa ushauri, na yeye amesoma haya mashauri yenu ila anasema amejitahidi sana kuongea naye kwa upole lkn anakuja juu mpk majirani wanasikia , anajisikia aibu sana, na kuna wakati wakikosana ndani basi ujue asubuhi atamwacha hampakii kwenye gari lake, inabidi mke akapande basi. inamuuma sana na hajui afanye nn.
...PESA IMELETA KIBURI AU KUJISAHAU??? mwanamke naye ajichunguze labda kuna jambo ambalo limuhundi mume wake anakuficha//
 
Back
Top Bottom