koboG
JF-Expert Member
- Apr 3, 2016
- 2,656
- 4,854
Habari zenu wakuu.
Poleni na majukumu na mihangaiko ya maisha ya kila siku.
Nina mpenzi wangu ambaye tulianza mahusiano yetu tangu mwaka jana.
mara nyingi amekua akiniomba nizae nae (anizalie) lakini nimekuwa nikimkatalia. Kwani kwa sasa ninahitaji kujiimarisha kiuchumi kabla ya kuingia katika majukumu mazito ya kulea.
Katika hali isiyo ya kawaida mara kwa mara ninapokuwa nazungumza nae amekuwa akiniuliza swali hili"Hivi ikitokea nimepata ujauzito wako kwa sasa utachukua uamuzi gani?"mara ya kwanza sikulitilia maanani lakini kadri siku zinavyo zidi ananiuliza tena na tena.
Wanajukwaa mimi nashindwa kuelewa kabisa nia ya huyu msichana kwani amekuwa akikazia sana juu ya hili swala.
Naomba ushauri wenu wakuu.