Ananitesa jamani

ndugu wana jf nina mpenzi wangu nampenda sana, nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuwa mwaminifu kwake lakini tangu amegundua kuwa nampenda ananitesa sana, muda mwingi hapokei sim zangu, text sometimes hajibu, anadai yuko bize sana na majukum ya kujenga taifa,sina la kufanya jaman mnishauri ndugu zangu mana nampenda sana

Kama unaona kweli umeteseka vya kutosha na unasema inatosha, fanya hivi, futa number zake zote za simu, futa sms zote ulizowahi kumtumia na alizowahi kukutumia, futa all calls zake zote. Baada ya hapo muombe Mungu akusaidie umsahau. najua utateseka sana na itakuchukua mda lakini vumilia yatakwisha na utarudi katika hali yako ya kawaida. Huyo hana mapenzi na wewe hata kidogo majukumu hayazuii hata kidogo kuwasiliana na umpendae.
 
BAADHI YA wasichana wa siku hizi wanajiangalia wao tu na nafsi zao. Utakuta msichana anafanya mambo mengi ya ajabu lakini anapoambiwa kuhusu hayo anaigiza kulia na kuomba msamaha lakini baada ya siku chache anarudia tena yaleyale. Mvulana mwenye busara akiona ameshindwa kumudu tabia ya msichana wake huamua kujiweka mbali kwa muda ili kupumzisha akili, na hapa ndipo malalamiko kama ya mleta mada hujitokeza.

Hali kadhalika BAADHI YA wavulana hupenda kuwachezea wasichana na kuwatelekeza huku wakiwaachia maumivu ya mapenzi kama ya mleta mada. Kiukweli wavulana wa namna hii si vizuri kuwa nao lakini kwa bahati mbaya hakuna alama/dalili za kumjua huyu ni mbaya/mzuri kitabia. Kinachobaki ni kumshirikisha Muumba wako akujaalie upate mtu atakayekufaa.

Kwa ujumla wapo wasichana/wavulana wasio na mapenzi ya kweli ila kuna wengine wapo wenye mapenzi ya kweli.

Kwa mleta mada nashauri ajaribu kumwuliza huyo mtu wake kama hamtaki basi avumilie maumivu kwa kipindi kisha baadaye atapata mtu wa kweli atakayemfaa maishani.

Kwa wavulana/wasichana wote kumbukeni hakuna kosa kubwa na lisilorekebishika maishani kama kukosea kuchagua mke/mume. Kwa hiyo umakini unahitajika.

Naishia hapa kwa leo.
 

akufukuzae hakwambii toka bidada
jikatae tartiiibu maana kashakuchoka huyo!!

Huenda wamechokana wote na huenda wamefanyiana visa ila huyu yeye kawahi hapa jf (labda) ili aonekane hana makosa.
Binafsi ningependa kupata maelezo kutoka upande wa pili pia ili nisiegeme wala kupendelea upande wowote.
 
Huenda wamechokana wote na huenda wamefanyiana visa ila huyu yeye kawahi hapa jf (labda) ili aonekane hana makosa.
Binafsi ningependa kupata maelezo kutoka upande wa pili pia ili nisiegeme wala kupendelea upande wowote.

tusubiri afunguke zaidi
maana mapenzi kizungumkuti!!
 
Kama wewe ni mdada pole sana coz umejipa jukumu ambalo hata Mungu hakukupa coz aliagiza WAUME KUPENDA WAKE ZAO NA SISI WANAWAKE TUWATII.So jitahidi kusimama unapohusika

 
nasaidia kukujib kwa experience ya wanaume-ukiona hivyo ujue ashapata alichokua anataka kama vp tafuta tu na wewe uwe busy na huyo mwingine
 
thax all dear friends, i feel a little bit relief from your advice. thax alot najitahidi kuufanyia kazi ushauri wenu stay blessed all.
:)
 
for sure hakuna cha ziada jaman mimi binafsi nampenda sana mpenzi wangu kiasi kwamba anavonifanyia hurts me very much, hatujawah kugombana wala kutukanana, sema tu umbali umetutenganisha lakin karibu kila weekend we visit each other.na tukiwa pamoja ananionyesha mapenzi,lakin nikiondoka tu balaa huanza. no text,no call
 
Pole sana ina uma sana, jamaaaaaaaaaaaaani, anza kwa kuzoe hali ya kuchuniwa, pili mnapokutana mwambie unaumia sana, fanya hivy kwa mkazo sana. Nakuambia yalisha nikuta sana nakuoneahuruma,.. Kama atakua hamaindi, kaa mkao wa kula, yawezekana kuna njemba somewhere linatikita.
 
Kufumbua macho ni dalili ya kutoka usingizini, kama ulikua umelala awali.
 
Back
Top Bottom