Ananipenda, ninampenda...ila kuna mambo tunatofautiana....ushauri tafadhali.

Jan 25, 2012
13
2
Mimi ni Kijana mwenye umri wa miaka 24 na nipo Chuoni nikisomea ngazi ya stashahada(Diploma) na nipo mwaka wa tatu(mwisho).Katika maisha yangu nilipanga kuwa nitaoa nikiwa na miaka kama 35 hivi na hii inamaanisha kuwa nitakuwa nimepata fursa pia ya kujiendeleza kimasomo katika ngazi ya shahada(Degree) na pengine masters.Ila nimebahatika kukutana na msichana ambaye tumetokea kupendana na kwa sasa yeye yupo mwaka wa pili chuoni katika ngazi ya shahada(Degree) na umri wake ni miaka 23. Katika kushauriana juu ya maisha yetu nimegundua kuwa yeye anataka tufunge ndoa miaka mitatu kuanzia sasa, yaani mimi nikiwa na miaka 27 huku yeye akiwa na miaka 26.Pia akasema kama hilo halitawezekana basi angalau kwa muda huo awe amepata mtoto na ndoa itafuata baadaye kama nilivyopanga. Anasema anaamini atakuwa tayari kumtunza mtoto na wala hataleta pressure kwangu wakati ninaendelea na masomo yangu. Hilo nimelipinga kwa nguvu zote kwa kuwa mimi ninaamini sana juu ya dini na imani yangu hainiruhusu kuwa na mtoto nje ya ndoa kwani atakuwa mtoto aliyepatikana baada ya TENDO LA USINZI na sio TENDO LA NDOA. Pia binafsi kinachonifanya nifikirie kuoa muda amabao nilioupanga ni kuwa nadhani nitakuwa tayari vya kutosha kulea wanangu nikishirikiana na mama yao kwa ukaribu zaidi. Nimewaza sana juu ya hili, je niendelee kuwa naye, au ndio penzi letu lifikie mwisho kwani falsafa zetu zinatofautiana? Naombeni ushauri wenu wadau, kwani ninampenda sana na ninaamini ananipenda sana na vigezo vyote anavyo isipokuwa kutofautiana kwa falsafa zetu na mitazamo yetu juu ya MAISHA.
 
hujui utakalo, kua kwanza.

Kwani watu wanaoa kwa kufuata umri au wakipata wanaowafaa kuwa wenzi wao?
 
Kwahiyo unataka kuoa miaka 11 ijayo.na yeye atakua na miaka 34...yeye anataka mzae ila wewe hutaki sababu ya imani kuwa mtoto atakuwa amepatikana katika uzinzi.....swali langu kwako ...je huyo bint una hakika hujawahi kum-do?kama umewahi na unaendelea na huo mchezo unafikiria nini?je hiyo sio dhambi?au unaogopa sababu ukipata mtoto utadhihirisha matendo unayofanya nyuma ya pazia? Kama nyie wote ni washika dini wazuri kwa maana kuwa hamfanyi uzinzi ni vizuri mkawekana sawa kwa kuelezana wazi mipango na mikakati yenu ..labda unaweza kusema hutaki kufanya hivyo kwa maana dini yako hairuhusu ...pia naamini una point zako muhimu zilizokufanya uset muda unaotegemea kuoa,ni vizuri na ukisema umuache huyo bint will you find peace of mind? vinginevyo piga goti muombe Mungu akupe hekima pia akuongoze kwa maana mke mwema mtu hupewa na Bwana.
 
huyu msichana yuko 'matured ' kuliko wewe....

mimi namuelewa sana huyo msichana

wewe naona bado kidogo mtoto....

na utampoteza
 
Sasa unataka tukushauri ukafanye uzinzi?Hebu tumia akili bwana mdogo!Kuna mambo yanashaurika mengine unatakiwa uamue mwenye!
 
Kaka kusubiri kuoa hapo utakapofikisha miaka 35 kwa maoni yangu ni muda mrefu sana. Kwanza huna mkataba na Mungu kwamba utaishi kufikisha hiyo miaka 35, pili hata ukifikisha hiyo miaka 35 wakati huo unaweza usiwe na GF ambaye ungependa kufunga naye pingu za maisha hadi kifo kiwatenganishe. Changamka Mkuu sikiliza ushauri wa huyo dada kisha ufanye kweli. Using'ang'ane tu na vile utakavyo wewe msikilize mwenzio.
 
Acha kujidanganya wewe!! Eti anakupenda, mtu ni kitabu kisichosomeka, wewe umewezaje kukisoma? dini yako haikuruhusu kuwa na mtoto bila ya ndoa, je, inakuruhusu uwe na mahusiano ya kimapenzi? Mapenzi ya chuo ni ya kusogeza siku mbele na kuondoa upweke na si vinginevyo. Kwa sasa ningekushauri ukaze buti ktk masomo tu, ukimaliza masomo ndiyo ufikirie mambo ya ndoa, vinginevyo kitu atakachokufanya huyu dada huwezi sahau maishani mwako.
 
huyu msichana yuko 'matured ' kuliko wewe....

mimi namuelewa sana huyo msichana

wewe naona bado kidogo mtoto....

na utampoteza
the guy is trying to play God,looks like anajua exactly 2022 maisha yake yatakuaje,maana anasema at 34 atakuwa na mastaz digrii na pesa ya kutunza wanae,very strange way of thinking.
 
Aisee umenihuzunisha sana, hivi unadhani huyo msichana atakusubiri miaka yote hiyo. Embu funguka..!
 
Hilo unalolitaka ni ndoto..mwanamke akusubiri kwa miaka zaidi ya kumi ndo umuoe??kwa kipi hasa?umri wako bado ni mdogo hata uwezo wa kufikiri ni mdogo!mwanamke akae mpaka afikishe miaka 34 anakusubiri ukija kubadilisha mawazo mwishoni nani atamuoa??
 
mtoto hutaki mbunye unaila.....nipe mamba ya shemeji nimueleweshe kea niaba yako kakaa
 
unataka kumzalisha mwenzako na miaka 34 jamani na unataka watoto wangapi sasa mana kama ni wawili au watatu utataka mwenzako hadi 40 anazaa tu kisa wewe ulishajipangia kuoa na miaka 35 jah! hii kali ingekua mm huyo dada ningesepa zangu ya nini kuja kuzalishwa na miaka 34 na hapo sio guaranteed kua mukioana hapo hapo na mimba kushika je mungu akifanya ije kushika after 10yrs wewe si utatoka nje kwa kukosa uvumilivu jamani na uchu wa mtoto mana umri unaenda
 
Hilo unalolitaka ni ndoto..mwanamke akusubiri kwa miaka zaidi ya kumi ndo umuoe??kwa kipi hasa?umri wako bado ni mdogo hata uwezo wa kufikiri ni mdogo!mwanamke akae mpaka afikishe miaka 34 anakusubiri ukija kubadilisha mawazo mwishoni nani atamuoa??
hapo chacha
 
Back
Top Bottom