¤Wapo wanaoamini kwamba Lowassa akihamia CHADEMA basi ataleta mafuriko zaidi ya yale ya mwaka 1995 pale Augustine Mrema alipohamia NCCR Mageuzi.
¤Nitatoa sababu 10 kwa nini bado naona kuhamia CHADEMA kwa Lowassa bado kutakuwa na athari ndogo za kisiasa kwa CCM.
1. Makamanda wengi wa Lowassa aliokuwa nao CCM wamemuangusha na kumsaliti Lowassa. Wengi wameomba ubunge kwa kupitia CCM na wengi wameishampongeza John Magufuli. Hapa nazungumzia Sophia Simba, Hussein Bashe, Mzee Mgeja na wengineo. Hawa wengi wanaamini mamba ana nguvu akiwa ndani ya maji na sio nje ya hapo. Kambi ya Lowassa wengi wangeendelea kuwa naye kama mgombea urais wa CCM angekuwa Bernard Membe.
2. Umaarufu wa Mrema ulikuwa ni wa kuwatetea wananchi kwa mfano kashfa ya V.G. Chavda ambaye alikula hela za serikali badala ya kuendeleza mashamba ya mkonge Tanga. Umaarufu wa Lowassa ni wa kununua kwa kufanya harambee na kununua makundi ya watu kumuunga mkono. Simulizi za "Maamuzi Magumu" ni za kuungaunga sana.
3. Lowassa akigombea urais kwa kupitia CHADEMA itaoneka kwamba kweli CHADEMA ni chama cha Kaskazini maana yeye na mwenyekiti wa chama wote ni wa ukanda huo. Mmoja Arusha mwingine Kilimanjaro.
4. Lowassa akigombea urais kupitia CHADEMA itasambaratisha UKAWA maana ukiachia James Mbatia ambaye ni rahisi kukubali mahitaji yoyote ya CHADEMA kwa vile tu anataka kupata msaada wa kugombea ubunge wa Vunjo, mtu kama Prof Lipumba sio rahisi kukubali Lowassa awe mgombea urais. Prof Lipumba alikuwa tayari Dr Slaa awe mgombea wa UKAWA. Lakini Dr Slaa tayari ameonyesha nia ya kurudia ubunge wake wa Karatu ili kumpisha Lowassa.
5. Mwaka 1995 mgombea wa CCM, Benjamin Mkapa alikuwa hajulikani sana kwa wananchi. Mwaka huu 2015 mgombea wa CCM, John Magufuli, kutokana hasa na uwaziri wake wa ujenzi (unaohusika na ujenzi wa barabara) anajulikana zaidi kwa wananchi ukifananisha na Mkapa wa mwaka 1995.
6. Katika chaguzi zote tokea mfumo wa vyama vingi uliporudishwa mwaka 1992 hakuna chama cha upinzani kilichopata hata nusu ya kura za urais wa CCM. Kwa mfano mwaka 1995 Mkapa (CCM) alipata 61.82% na Mrema (NCCR-Mageuzi) alipata 27.77%. Mwaka 2010, Kikwete (CCM) alipata 61.17% na Dr Slaa (CHADEMA) alipata 26.34%. Hii ni miaka miwili ambayo CCM ilifanya vibaya zaidi katika chaguzi zote. Miaka mingine ilikuwa ni majanga zaidi kwa upinzani.
7. CHADEMA wataonekana kulamba matapishi yao maana mpaka leo hawajawahi kukana hata sehemu moja ya "List of Shame" iliyotolewa katika uwanja wa Mwembeyanga Jumamosi ya tarehe 15-Sep-2007 (kabla hata ya Richmond) ambayo ilimgusa pia Lowassa.
8. CCM itatumia nguvu kubwa ya kiuchumi. Ikumbukwe kila mwezi CCM inapata tsh 800M kama ruzuku, CHADEMA hupata robo yake tsh 200M. Pia wafanyabiashara wengi huchangia CCM kipindi hiki cha uchaguzi ili wasishughulikiwe na vyombo vya kiutawala kwa mfano TRA.
9. Watanzania wengi bado wana kale kamsemo ka "mbunge nitamchagua wa upinzani ila rais nitamchagua wa CCM". Hii inatokana na watu wengi kutoamini upinzani kushinda urais kutokana na mikoa mingi kama Tanga, Dodoma, Mtwara, Ruvuma, Pwani na mingineo mingi kutopata "ukombozi". Upinzani upo zaidi kwenye miji ya mikoa maarufu na kusahau maeneo ya vijijini hususan baada ya kufa kwa "Operation Sangara". Pia washabiki wengi wa upinzani ni vijana wa mijini ambao sio wapiga kura wazuri ukifananisha na CCM ambayo bado inategemea sana akina mama wa vijijini.
10. CCM itatumia manufaa (advantage) yake ya kuwa chama tawala, kwa kutumia mfumo wa usalama wa Taifa (intelligence) wa nchi kufuatilia taarifa za Lowassa na kuzifanyia kazi.