Mivyumba
JF-Expert Member
- Apr 20, 2017
- 275
- 533
NIMEICOPY SEHEMU.
NJIA PANDA!!
Dada Shangwe shikamoo. Naomba unipelekee ITY ,Yamenifika...
Mimi nilisoma Advance msalato girls, sasa kipindi hicho nilikuwa na rafiki yangu ana Asili ya Ethiopia kwao ni Arusha.
Amelelewa na baba tu wazaz wake waliachana kwa mujibu wake, na Mama yake anaishi nje ya nchi kwahiyo kwa baba yake ni mtoto pekee.
Sasa kipindi tupo shule maisha yangu yalikuwa magumu sababu kwetu hatuna uwezo kila kitu nilikuwa nasaidiwa na huyo rafiki yangu....
Alimweleza baba yake kuhusu mimi na baba yake ni mtu mwenye pesa sana akawa kila kitu kizuri atakachomfanyia mwanae lazima anifanyie na mimi.
Ilifikia mpaka tukifunga Shule huyu rafiki yangu anaenda kwetu Moshi, tunakaa kama wiki baba yake anatununulia familia yetu mahitaji ya hapo kwetu kwa muda huo kisha, tunaenda kwao Arusha.
Basi baada ya kumaliza A level mimi nilipangiwa chuo MUST , kipo Mbeya, huyu rafiki angu yeye Alienda UDSM uzuri nilipata mkopo lakini yule baba kila mwezi alikuwa ananitumia laki 5 ya kujikimu.
Mpaka nilipomaliza chuo 2020, Akaniomba twende Zanzibar hapo huyu mwanae Alienda Belgium kwa mama yake, Tulifikia hotel nzuri tukala basi kwa mara ya kwanza yule baba akanitamkia ananipenda kipindi nipo shule alishindwa kuniambia sababu nilikuwa mdogo.
Hapo nilikuwa nina mahusiano lakini sijawahi kusex na nilikuwa nina 24 yrs old, nilimshangaa, niliogopa sababu nilikuwa ninamchukulia kama baba yangu japo hana miaka 50 had saivi ana 40+, Nikajikuta ninalala naye na anakuwa mwanaume wa kwanza kunigusa.
Tulikaa Zanzibar almost wiki mbili nikarudi Dar tukatafuta nyumba nzima akanipangia, nikafungua biashara zangu yeye kila wiki akawa anakuja Dar kwangu sasa mimi yule mwanaume wangu tuliyekutana MUST amepata kazi nzuri, alishakuja kwetu kutoa mahari na pete nimevalishwa sendoff ni mwez wa saba na harusi.
Sasa nimejikuta siwezi kuishi bila huyu baba wa rafiki yangu, na yeye alisema anataka kunioa ila nikaogopa haitaleta picha nzuri kwa rafiki yangu nikawa ninamchenga na hapa nilipo nina mimba ya huyu baba ina miezi minne.
Huyu mwanaume wangu anajua ni yake na yule baba anajua nina mimba yake sasa hivi haji Dar mimi ndo ninaenda Arusha na ndege anakuja kunichukua kisongo Airport
Nimebaki njia panda nikisema nimzae huyu mtoto lazma katakuwa chotara na huyu kaka wa kunioa ni mweusi tii mimi pia mweusi.
Nishaurini wamama nisitishe ndoa nimkubali huyu baba nimzalie huyu mtoto, au nikubali ndoa nitoe mimba?
Kwetu maisha yalikuwa magumu mno ametujengea nyumba nzuri pale nyumbani nimemfungulia mama duka maana ile nyumba ina frem na pesa ananipa huyu baba. Kwetu wanajua yule baba alinisaidia tu