Habar wa jf najitokeza kwenu kuomba ushauri kwenu kwani nipo njia panda mi kijana wa miaka 24 ni mfanyabiashara mdogomdogo nilikuwa na mpenzi wangu x ambaye nilikuwa nampendana sn! Lkn yeye alikuwa ni mwingi wa habari nishawahi kumfumania mara kadhaa na washikaji! Na kila nilipokuwa namwambia me na ye tuachane alikuwa akinimbeleza na kulia sn akidai ananipenda lkn anafanya ivyo kutokana na shinikizo la dada yake anamwambia atafute mwanaume mwenye pesa! Na kweli me kwakipindi kile nilikuwa bado sipo vizuri kipesa kwani nilikuwa sina kazi! Bac kwakuwa nilikuwa nampenda nilikuwa na msamehee na kuendelea kuwa nae, lkn bado tatizo likawa lipopalepale kwan baadae akawa anaweza kuondoka kwao hata day 4 hata pasipo me kuniaga na nikimuuliza mbona me ckuelewi unakwenda wapi? Alikuwa ananiambia oooh!nilikuwa kwa baba angu mdogo mara oooh! Nilikuwa kwa shangazi bagamoyo nikawa namuuliza mbona unapokuwa unaondoka huwa huji kuniaga kwan na me nataman niwe nakucndikiza mpaka uko! Kisha me narudi akawa ananijibu safari zenyewe uwazinakuwa za glafa lkn ucjali me bado nipo pa1 na ww! Kwakuwa nilikuwa nampenda ckuwa na chakufanya nikawa namkubalia! Lkn nikawa naona tofauti akawa anakuja ela na nguo akidai ndugu zake wamempa! Bac mapenzi yetu yakawa ya dizain iyo ikawa anaweza kuondoka hata miez 2 pasipo kuonana na me wala kuwasiliana! Nikimpigia cm yake haipatikan au inaita pasipo kupokelewa na akirudi nikimuuliza ananijibu ooh cm yangu hakuwa na chaji au siwez kuongea nawe nikiwa kwa ndugu zangu! Bac 2kaendelea kuwa ivyoivyo! Nakumbuka ilikuwa mwaka 2006 ndo ilikuwa mwisho wa kumuona kwan alikuja kuondoka pasipo kuniaga! Daaah!! Nilikuwa mpweke sn hasa ukizingatia kwamba nilikuwa nikimpenda sn! Kila nikijaribu kumpigia alikuwa hapatikan! Na nilipokwenda kumuulizia kwao dada yake alikuwa akinipa majibu ya kunivunja moyo "wala ucangaike kumtafuta mdogo wangu kashapata mume" daah! Sio siri nilikuwa nikiudhunika sn na roho kuniuma na kujutia hali yangu ya kutokuwa pesa! Bac maisha yaliendelea taribu nikaanza kumsahau na nikapata mpenzi mwingine na kuanza kufanya biashara! Bac nikawa nikipata habari zake kwamba ana mtoto! Bwana aliyezaa nae kamwacha! Aaah! Nikawa ctaki tena kuckia habari zake hata kumuona! Mungu akanisaidia nianza kuishi na mchumba wangu mpya* xaxa yapata miaka 4 pasipo kuonana ane! Juz nikiwa kwenye gari narudi zangu kwenye mishemishe zangu kuna binti kaja na kunishika bega nikastika kutazama nikakutana na sura yake! Hakika moyo ulinistuka akanisalimia na kuomba kuongea nami japo dk 3 nilimkatalia lkn akawa king'ang'anizi! Nikajikuta namkubalia kuongea nae! Akanambia bado aninipenda lkn amegundua kwamba me nimeoa na amekuwa akinifuatilia karibu kila siku amejua nafanya kazi wap na mchumba wangu anamjua! Anadai bado ananipenda na ni msamehee kwa yote yaliotokea ni mwache mchumba wangu na nimchukue yeye na km nitapingana nae! Bac nijipange kwa mabaya yanayokuja kwangu me na mchumba wangu!! Akaniachia namba yake na kunipa siku 3 niwe nimempa jibu! Nimerudi home cjamwambia lolote mchumba wangu! Naogopa kumweka na wasiwasi na mashaka juu yake na me kuhusu uhusiano wetu! Nimekuwa nikiwaza sn cpati jibu nifanye nn? Naombeni ushauli wenu wana jf nipo njia panda!!