Anachokifanya Hans Poppe ndani ya Simba

Anachokifanya Hans Poppe ndani ya Simba

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,393
Hans pope ni zaidi ya popo bawa anaowalaza wanasimba kifudifudi.... Wala hakuna ubishi tena, yote yanayoendelea ndani ya simba
mpaka kufikia hatua ya harufu ya simba kushuka daraja, kinara mkuu ni mzee hans pope jinsi anavyohusika..

(1) wakati uchaguzi mkuu wa klabu ya simba unafanyika, mzee hans pope alifanya influence kwa mashabiki wa simba wamchague
bwana aveva, na aliwatisha kuwa kama wasingemchagua aveva basi angejitoa katika timu na asingetumia tena pesa zake kuisaidia
simba, kwa kifupi hans pope anajua mapungufu ya bwana aveva na alijua wazi kabisa kama angeingia mtu mwingine madarakani zaidi ya aveva lengo lake lakuitawala simba akiwa nje ya nafasi ya rais lisingewezekana....

Wanachama wengi wa simba wanafahamu msimamo wa bwana wambura michael, siku zote wambura anataka kuiona klabu ya simba ikisimama na kujitegemea yenyewe pasipo kumtegemea mtu,
wambura anajua matatizo ya kumtegemea mtu, na bahati mbaya sana bwana hans pope hampendi michael wambura kwa sababu tu
hataki kuona simba inaendelea kutegemea na kuwanyenyekea watu kwa pesa zao shinikizo la kundi la ukawa kufutwa uanachama lilitoka kwa mzee hans pope, na aliamini akina wambura na wenzake watapofutwa uanachama basi kwake ingekuwa rahisi kufanya mambo yake vile anavyotaka kama afanyavyo sasa kauli zake kuwa kocha phiri ana matatizo katika ufundishaji hans pope anashangaza wadau wa mpira duniani

(1) tukumbuke phiri akuomba kazi ya kuja kufundisha simba bali huyu huyu hans pope na kaburu ndiye walimwendea kocha phiri kumuomba aje kuifundisha simba, na walifanya hivi wakidai kuwa wanamfahamu kocha phiri na phiri naye anafahamu mila, desturi
na soka ya simba, leo hii iweje mzee hans pope aanze kumlaumu kocha phiri kuwa anamatatizo katika ufundishaji wakati yeye mwenyewe alienda zambia kumuomba aje kuifundisha simba kutokana na ubora wake ambao alikuwa anaufahamu?

(2) kocha phiri huyu huyu ambaye mzee hans pope anasema anamatatizo katika ufundishaji, ndiye aliweza kuweka record yakuipa simba ubingwa wa tanzania pasipo kufungwa ata mechi moja, na hiki ndicho kigezo kimojawapo kiliwafanya viongozi wa simba wamrudishe tena kuinoa timu ya simba, iweje leo phiri aonekane ufundishaji wake una matatizo?

(3) hans pope huyu huyu ndiye alisimama kidete mpaka mfaransa lewigy kufukuzwa kwa sababu tu kocha lewigy hakutaka kuingiliwa kwenye programe yake yakutaka kuwatumia vijana wadogo kwa maendeleo ya klabu ya simba

(4) hans pope huyu huyu ndiye alisimamia tena mzee kibadeni na julio kufukuzwa kazi simba baada ya timu kutofanya vizuri pasipo
kusikiliza utaalamu wa kocha ambapo nakumbuka mzee kibadeni aliwaambia watu wa simba kuwa kwa kipindi kile wasitegemee
matokeo mazuri kwa sababu timu ilikuwa bado changa na inahitaji muda wakukaa pamoja ikomae kimashindano, lakini mwisho wa siku kibadeni alifukuzwa

(5) hans pope huyu huyu ndiye alisimamia kocha logarisic kufukuzwa simba, na tukumbuke kuwa mara tu kocha logarisic kuingia simba alisema kabisa timu haina wachezaji ambao wanastahili kuichezea simba kwa sababu viwango vyao vidogo na bado hawapo tayari kimashindano, lakini mwisho wake alifukuzwa kazi kwa kusema ukweli

(6) leo hii mzee hans pope ameanza choko choko tena zakutaka kuandaa na kuhalalisha sababu zakumfukuza kocha phiri akisema kuwa fundisha yake ina matatizo wakati ata report kocha kueleza kwanini timu inatoa sare mfululizo hajaisoma...huku ni kumkosea adabu kocha phiri na kuikosea adabu taaluma ya ukocha duniani ambalo wengi hawalifahamu

(1) mfahamu kuwa kuanzia kocha lewigy mpaka leo hii, usajili wa simba siku zote unafanywa na mzee hans pope pamoja na bwana kaburu, hakuna kocha ata mmoja kati ya niliowataja hapo juu wamewahi kusajili wachezaji kwa matakwa yao na maono yao yakitaaluma, kama makocha wote hawa wamekuwa wakilalamika juu ya ubora wa wachezaji maana yake nikuwa watu wanaohusika na usajili wanafanya usajili ambao uko below standard na siku zote kitu ambacho kiko below standard hakiwezi kuleta positive result,

swali moja la msingi tunapaswa kuwauliza hans pope na bwana kaburu, kwanini makocha wote hawa wanalalamikia juu ya ubora wa wachezaji wanaosajiliwa na simba na wao wanaendelea tu kusajili kwa utashi wao kwanini isifike wakati wawaachie makocha wenyewe wasajili kulingana na utashi wa taaluma yao?

Katika maswala ya ugavi na manunuzi kuna kitu kinaitwa, "money for value and value for money" maana yake ni kwamba unapofanya manunuzi thamani ya pesa lazima ionekane kwa kile ulichonunua, na kama thamani ya pesa imeshindwa kuonekana kwa kile ulichonunua maana yake nikuwa kuna uhuni, ujanja, au wizi umefanyika katika manunuzi husika swala la makocha wote kulalamikia ubora wa wachezaji na bado viongozi hawa wanaendelea kusajili tu pasipo kuamua kuwaachia makocha wenyewe wafanye usajili kulingana na taaluma zao maana yake kuna uchafu unafanyika ambao wahusika wananufaika nao simba ukawa ni kisingizio cha.upuuzi... ( onyo; usipuuzie habari za simba ukawa kwa sababu wapo na wanafanya kazi kwa siri sana they are very contravesial hawa watu kama freemason tu, ni wasiri sana njia wanazotumia kuimaliza simba )

nasema simba ukawa ni kisingizio cha kipuuzi kwa sababu wametengenezwa na akina hans pope wenyewe na wanaonekana wana nguvu kwa sababu aveva, kaburu na hans pope wameshindwa kutekeleza majukumu yao kwa klabu simba imeanza kufanya vibaya tokea kipindi cha kocha lewigy, swali la msingi tunapaswa kujiuliza je kipindi cha kocha lewigy simba ukawa walikuwepo? Lakini pia tunapaswa kujiuliza ligi iliyopita simba ikishika nafasi ya nne simba ukawa walikuwepo? Kinachokosekana sasa hivi katika simba ni weledi wa mpira tu, wachezaji walipwe stahili zao, kamwe kuwafungia wachezaji kwa kudai haki zao siyo njia ya kuisaidia simba leo hii unasema phiri hafai wakati phiri anafundisha wachezaji ambao hakuna ata mmoja ambaye amesajiliwa simba kwa mapendekezo yake wote amewakuta na hana uwezo wa kuwakataa, atawakataaje wakati ndiyo aliowakuta?

Na bahati mbaya zaidi wanamchagulia wachezaji wakucheza, huu ni upuuzi mkubwa wa soka ambao sijawahi kuusikia popote duniani zaidi ya tanzania hans pope soma alama za nyakati, kamwe hauwezi kupambana na nguvu ya watu kiujanja ujanja kwa kuringia senti ambazo unazo, simba ni tajiri zaidi ya unavyofikiri unaiona masikini kwa
kukupigia magoti kwa sababu tu bado haijapata viongozi wenye vision..
 
BINAFSI nimemuona Pope akaitoa shutuma kwa kocha jana, halikuwa jambo jema kabisa. simba ina muda mrefu sasa haifanyi vizuri kabla hata Phiri hajafika pale. kumlaumu Phiri wakati timu ina kila aina ni kutomtendea haki
 
Ila mbona ile siku huyu huyu Hans poppe wakati yupo mbele ya waandishi wa habari anamtambulisha mshambuliaji raia wa uganda Emanuel Okwi kutoka yanga mlimshangilia sana na kumuita shujaa iweje leo tena mnaanza kulia kulia eti anasajili wachezaji bila kufuata matakwa ya kocha!!!!
 
"Nyani haoni kundule"... kwa hio hans pope haoni kama tatizo ni yeye!!
 
kwan hans pope anacheza namba ngap? hahaahaha na bado mpaka.mshuke daraja kuja kufika mwakan
 
Ila mbona ile siku huyu huyu Hans poppe wakati yupo mbele ya waandishi wa habari anamtambulisha mshambuliaji raia wa uganda Emanuel Okwi kutoka yanga mlimshangilia sana na kumuita shujaa iweje leo tena mnaanza kulia kulia eti anasajili wachezaji bila kufuata matakwa ya kocha!!!!

Kambi ya Wambura wanahangaika sana, wanajifanya kama wanauchungu kumbe wanashangilia SSC kufanya vibaya, mnafikiri Wambura angefanya nini SSC bana? Mbona mnakuwa mazuzu, kwani Wambura hajawahi kuongoza mpira nchi hii? Je alifanya nini? Kwa hiyo kama Poppe alishiriki kumleta kocha anapofanya vibaya hana uhuru wa kusema? Wakati Poppe na kundi lake wanatangaza kumleta Phiri mbona wana-Simba wote tulifurahia hata wewe hukutoa angalizo lolote, ila leo mambo yamekuwa mabaya unajifanya kama mtabiri, huyu Poppe wakati anapowafadhili mfanye uchaguzi mnakaa kimya kama hamjui, anaposajili wachezaji mnashangilia, akiongea kwa uhuru wake mnamshambulia, huu tunaita UNAFIKI. Toka lini mzazi amsomeshe mwanae shule ya gharama na kumuhudumia mahitaji muhimu afu mtoto akifanya vbaya darasani eti mnataka mzazi akae kimya!
 
phiri angesajiri vp wakati alikuwa haangalii ligi ya tz,angeota au?! usicopy na kupaste maneno ya shaffi ndugu
 
Tatizo la Simba kwa sasa ni UMOJA...wasameheane, warudi pamoja wacheze mpira. Vinginevyo itakuwa ni majungu, kutegeana na mwisho..timu yaweza kushuka daraja hivi hivi.

Nakumbuka mwaka fulani, simba ilikuwa ishuke daraja..thanks kwa mechi ya Mwisho dhidi ya Yandga ambayo mnyama alimfunga Yanga mbili kwa moja...goli la pili alifunga Sunday Juma nadhani...Timu ikasalia ligi kuu.

Sitarajii kuwa wanasimba wanahitaji presha kama ile tena....
 
hans pop ni tatizo simba.Tangu nianze kumsikia ni vurugu tu za usajiri pale simba...toa huyu weka yule rudisha yule.
 
Ila mbona ile siku huyu huyu Hans poppe wakati yupo mbele ya waandishi wa habari anamtambulisha mshambuliaji raia wa uganda Emanuel Okwi kutoka yanga mlimshangilia sana na kumuita shujaa iweje leo tena mnaanza kulia kulia eti anasajili wachezaji bila kufuata matakwa ya kocha!!!!

Swali zuri sana hilo..wasipojibu ni wanafiki
 
Zakaria Hans Pope, ananikumbusha 1982, alipokuwa mmoja wa watuhumiwa waliotaka kuipindua Serikali ya Mwl JK Nyerere, nadhani anataka endeleza UHAINI. Binafsi tuhuma alizotoa jana mbele ya Media zimewakera wengi.....
 
Mkutano Mkuu wa wanachama wa SSC ndio watakao amua ni vipi club Yao wanataka iwe na iendeshwe vipi, basi wanachama wote jaribuni kuwa watulivu na kujiepusha na Maneno Ya kuudhi au kukashifu mwanacha mwingine" hayo hayaisaidii club wala wanachama!! Natumai mwanachama wa kweli atakuwa na maoni Ya Kujiunga club na si kuinomoa club na wanachama wake" SIMBA NGUVU MOJA NA SAUTI MOJA:
 
brave one kuna vitu flani umeviongea, ngoja nipite kwanza kwa Mangi nikapate mambo yangu, then narudi.
 
Last edited by a moderator:
Mrudisheni Aden RAGE si ndiyo zenu kuzunguka humo humo tu huwa hamwazi jipya, kama ni ugonjwa unafanya kuzunguka njia zile zile tu, sintashangaa Simba mkimrudisha Rage
 
Ukisoma between the line unagundua tu kwamba Brave one una mrengo gani katika siasa za Simba (kama sio JIRANI)........hakuna ubishi kwamba makocha wote waliofukuzwa waifukukzwa kwa sababu ambazo kila mmoja aliziona na hata wewe naamini ulizikubali kwamba inapofika mahali perfomance indicators hazifanyi kazi then you must change approach/strategies.....ukitaka kuamini hivyo naweza kukuwekea picha za jinsi makocha wote hao walivyoingi ana na walivyoondoka

ubaya wa wapenzi wa soka tunasahau haraka sana, leo unamzomea Tegete kesho unamsifu keshokutwa akikosa goli unamzomea tena......ndivyo wachangiaji wanavyojaribu kusema kwenye mada hii

Ukweli Hanspope ana uchungu sana na Simba na anatumia pesa zake nyingi sana kwa timu na kama hujui peleleza safari ya SA................HATA shutuma unazotoa kwamba anasajili kwa maslahi fulani ni kichekoi cha mchana kwa sababu Hanspope hahitaji fedha kutoka simba ila simba inahitaji fedha kutoka kwa Hans..............kama ni maslahi labda ya kisiasa kama walivyofanaya kina Manji, Rage, Gulamali (R.I.P) etc au kama anatumia wachezaji kama alivyowatumia Azim Dewji hapoo sawa kakn si kusema anasajili ili ale cha juu si kweli kabisa

Mpira wa sasa ni pesa ndugu yangu, wenye pesa na mapenzi ndio wanaendesha timu, hebu jiulize ghrama za maandali ya mchezo wa Simba na Yanga vs mapato waliyopata.......ada ya uanachama simba ambayo ni shilingi 1000 kwa mwezi vs maandalizi ya timu kwa mwezi/wiki/siku


kuna wakati Hans aliomba kujiuzulu tukaenda kumpigia magoti arudi (Rage) kwa kutambua umuhimu wake katika uendeshaji wa soka...........mmie simjui na sina masilahi naye lakn nathamni sana mchango wake simba na nadhani mada yako ina ushawishi wa kumfanya a -provoke na kuondoka ili makomandoo mje mle milangoni

wakti fulani unahangaika na kitu ili kupata mafanikio, so unapoona alikwenda Zambia kumfuata Phiri ni sababu ya mahangaiko tu kuona huenda mbinu za Phiri zitatusaidia kwa wakati huu kama iivyokuwa kwa wakati ule lakn kuna ukweli pia kwamba soka linabadilika kutokana na nyakati husika, huenda bado kocha anatumia mbinu za mwaka 47 ambazo hasiisaidii timu hapo unafanyaje? inabidi kuchange approach/tools etc......... siamini kwamba Hans Pope anakua compeled kuhangaika kwa utashi binafsi au inda bali kwa mafanikio ya simba ndio maana penye kasoro anasema ukweli inagawa si kila mahali unaweza kusema jambo kama alivyofanya kupitia media lkn inafika mahali pia unakua provoked kwa hali ya mambo ..................(kuna wakati mfano unaweza kutukana zinga la tusi kwa kuchezewa rafu na dereva mwenzio barabarani bila kujali uko na mkeo/mama mzazi au hata mama/baba mkwe-hiyo yote ni provocation)

mwisho kabisa wengi tunaguswa sana na sintofahamu na mwenendo wa simba na nadhani na wewe pia unaguswa (kama sio JIRANI) na huenda huna maslahi yyte na Hans ila maslahi na simba kufanya vizuri...............nakukumbusha kauli mbiu ya simba ni nguvu moja hivyo basi........leo tumshinda 1-0 na Lipuli

United we Stand, Divided we Fall
 
Ukisoma between the line unagundua tu kwamba Brave one una mrengo gani katika siasa za Simba (kama sio JIRANI)........hakuna ubishi kwamba makocha wote waliofukuzwa waifukukzwa kwa sababu ambazo kila mmoja aliziona na hata wewe naamini ulizikubali kwamba inapofika mahali perfomance indicators hazifanyi kazi then you must change approach/strategies.....ukitaka kuamini hivyo naweza kukuwekea picha za jinsi makocha wote hao walivyoingi ana na walivyoondoka

ubaya wa wapenzi wa soka tunasahau haraka sana, leo unamzomea Tegete kesho unamsifu keshokutwa akikosa goli unamzomea tena......ndivyo wachangiaji wanavyojaribu kusema kwenye mada hii

Ukweli Hanspope ana uchungu sana na Simba na anatumia pesa zake nyingi sana kwa timu na kama hujui peleleza safari ya SA................HATA shutuma unazotoa kwamba anasajili kwa maslahi fulani ni kichekoi cha mchana kwa sababu Hanspope hahitaji fedha kutoka simba ila simba inahitaji fedha kutoka kwa Hans..............kama ni maslahi labda ya kisiasa kama walivyofanaya kina Manji, Rage, Gulamali (R.I.P) etc au kama anatumia wachezaji kama alivyowatumia Azim Dewji hapoo sawa kakn si kusema anasajili ili ale cha juu si kweli kabisa

Mpira wa sasa ni pesa ndugu yangu, wenye pesa na mapenzi ndio wanaendesha timu, hebu jiulize ghrama za maandali ya mchezo wa Simba na Yanga vs mapato waliyopata.......ada ya uanachama simba ambayo ni shilingi 1000 kwa mwezi vs maandalizi ya timu kwa mwezi/wiki/siku


kuna wakati Hans aliomba kujiuzulu tukaenda kumpigia magoti arudi (Rage) kwa kutambua umuhimu wake katika uendeshaji wa soka...........mmie simjui na sina masilahi naye lakn nathamni sana mchango wake simba na nadhani mada yako ina ushawishi wa kumfanya a -provoke na kuondoka ili makomandoo mje mle milangoni

wakti fulani unahangaika na kitu ili kupata mafanikio, so unapoona alikwenda Zambia kumfuata Phiri ni sababu ya mahangaiko tu kuona huenda mbinu za Phiri zitatusaidia kwa wakati huu kama iivyokuwa kwa wakati ule lakn kuna ukweli pia kwamba soka linabadilika kutokana na nyakati husika, huenda bado kocha anatumia mbinu za mwaka 47 ambazo hasiisaidii timu hapo unafanyaje? inabidi kuchange approach/tools etc......... siamini kwamba Hans Pope anakua compeled kuhangaika kwa utashi binafsi au inda bali kwa mafanikio ya simba ndio maana penye kasoro anasema ukweli inagawa si kila mahali unaweza kusema jambo kama alivyofanya kupitia media lkn inafika mahali pia unakua provoked kwa hali ya mambo ..................(kuna wakati mfano unaweza kutukana zinga la tusi kwa kuchezewa rafu na dereva mwenzio barabarani bila kujali uko na mkeo/mama mzazi au hata mama/baba mkwe-hiyo yote ni provocation)

mwisho kabisa wengi tunaguswa sana na sintofahamu na mwenendo wa simba na nadhani na wewe pia unaguswa (kama sio JIRANI) na huenda huna maslahi yyte na Hans ila maslahi na simba kufanya vizuri...............nakukumbusha kauli mbiu ya simba ni nguvu moja hivyo basi........leo tumshinda 1-0 na Lipuli

United we Stand, Divided we Fall
Binafsi ningependa kukubaliana na mawazo yako, ila kuna vitu kidogo tunatofautiana:
1. Ni kweli ZHP ana uchungu na Simba, ni mwehu tu ndiye anayeweza kubisha hilo. Lakini si kweli kwamba hana maslahi yoyote anayohitaji/anayopata ndani ya Simba. La kujiuliza ni je, baina ya mapenzi yake kwa upande mmoja na manufaa anayotarjia kwa upande mwengine, lipi ameliweka mbele zaidi? Tuelewe kwamba hakuna mwanadamu yeyote anayetenda wema wowote bila ya kutarajia chochote. Tunahonga ili kupata mahaba ya tunayemuhonga. Tunaabudu ili tupate Pepo ya Mwenye enzi Mungu. Tunasomesha watoto ili angalau wasiendelee kuwa mizigo kwetu ukubwani kwao, tunasema kweli ili tusije kuadhirika uongo utapodhihiri, tunachangia harambee mbalimbali ili jamii ituone wa maana, n.k. Kwa mtu kama ZHP, manufaa siyo lazima yawe fedha moja kwa moja. Yanaweza kuwa Uluwa (influence), hadhi (status), umaarufu (fame), au hata kumfurahisha mtu mwengine (mf. mama nyumbani). Utulivu unaotokana na manufaa hayo ndio unaompa nguvu na fursa ya kutafuta na kupata zaidi. Kwa yeye anayejua siri kamili ya malengo ya uchangiaji wake, anayachukulia hayo sawa na fedha inayozalishwa nayo. Ni yeye tu ndiye ajuaye kipi ametangliza baina ya manufaa hayo na mapenzi yake kwa Simba. Tajiri anaweza kumnunulia mkewe kila atakacho, lakini asiwe tayari kutoa nusu figo ili kuokoa maisha ya mke huyohuyo.
2. Hata hoja yangu ya juu isingekuwa sahihi, njia ya jehanamu imejaa tele nia njema. Sasa iwapo Mungu anamtia hatiani mja aliyekosea kwa nia ya kutenda mema, iweje Wanasimba wasimtuhumu ZHP pale 'wema' wake unapozua majanga klabuni?
3. Mara ngapi walimu wamekuwa wakilalamika juu ya maswala mbalimbali ya timu, maswala yanayohusiana moja kwa moja na ZHP, na kusiwe na marekebisho yoyote? Loga alipata kulalamikia aina ya wachezaji aliowakuta Simba na kuagiza aina mahsusi ya anaowataka yeye (si lazima nikubakiane naye). ZHP kama bosi wa Kamati ya Usajili hakutekeleza hilo, wala hakupata kumweleza kocha kwamba hakubaliani na mapendekezo hayo. Kibadeni hakutaka makubwa, ni subira tu ili baada ya msimu mmoja timu iwe imezoeana na kukomaa. Phiri amenukuliwa kutohusishwa na usajili wa Okwi wala kutemwa kwa Musoti. Wote hao hatimaye wameonekana/wanaonekana ndio vikwazo na matakwa yao ndiyo yanayochangia kuondoka kwao. Kwa nini asisemwe ZHP? Unapopima performance ya kocha unatakiwa pia kuzingatia umemtekelezea matakwa yake kwa kiasi gani na/au umempa uhuru kiasi gani wa kufanya kazi yake.
4. Inachofanya Simba kupitia kwa ZHP ni kusajili na baadaye kutafuta kocha. Kwa maana hiyo kocha atafundisha kwa mujibu wa uwezo wa wachezaji aliowakuta. Huwezi kumtarajia Mourinho kuipeleka Timu ya Taifa ya India kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia kwa sababu tu yeye ni kocha mzuri. Lazima tukubali kwamba ZHP ameboronga kwenye usajili: Kiongera ni spana mkononi, Kwizera ni dhahabu feki (mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast hawezi kukosa timu za Ulaya), Okwi ni mchezaji wa viongozi, si wa timu (aliyecheza nao Simba awali hawatafurahi naye, aliyowakuta watajisikia wamedhalilishwa), Banda, Maguri,Mgeveke, Manyika ni wachezaji wa kuongezea - sio wa kuanzia. Musoti hakupaswa kutolewa kafara; pengo lake linaendelea kuitesa timu hadi leo. Alaumiwe nani kwa hayo kama sio et al ZHP?
5. ZHP ajue kwamba Aveva, Kaburu ni viongozi wa Simba hivi sasa. Lazima watofautishe baina ya kuongoza Simba na kuongoza FOS. Siri kubwa iliyoifikisha Simba ilipo sasa ni u-FOS wa kushindana na Yanga kwenye Okwi. Kabla ya Okwi, Simba ya Phiri ilikwishatengemaa. Nimeishuhudia ikiifunga KMKM nyumbani kwao 4-0. Mmeishuhudia ikiifunga Gor Mahia 3-0. Maana yake ni kwamba fowadi ya timu ilikuwa fanisi (efficient) tayari, pia safu ya ulinzi ilikuwa imeshatulia. Kuongezeka. Okwi haujaongeza idadi ya magoli yaliyopata kufungwa kabla yake. Kupungua kwa Musoti kumewacha tobo linlovujisha magoli machache yanayofungwa na Simba hivi sasa. Nani alaumiwe kwa hilo kama sio ZHP et al?
Mimi si shabiki wa Simba, nadhani kwa hilo niko na nafasi nzuri ya kuishauri. Nalo ni kwamba kurukaruka sio dawa ya urimbo. Hazina iliyopo ya wachezaji wazawa inakidhi haja. Kocha naye hana matatizo. Kama alivyosema Kibadeni, waachwe wakomae, waelewane. Mwalimu aangalie wachezaji wa kigeni kwa msimu ujao. Waliopo wana kasoro nilizozisema,Owino ana tatizo la majeruhi. Kwa mtindo wa duru za FOS kusajili na kumtafuta kocha baadaye, Wanasimba watarajie kuendelea kulala mapema kwa Ligi nyingi zijazo.
 
Hans pope ni zaidi ya popo bawa anaowalaza wanasimba
kifudifudi.... Wala hakuna ubishi tena, yote yanayoendelea ndani ya simba
mpaka kufikia hatua ya harufu ya simba kushuka daraja, kinara
mkuu ni mzee hans pope jinsi anavyohusika.. (1) wakati uchaguzi mkuu wa klabu ya simba unafanyika, mzee hans
pope alifanya influence kwa mashabiki wa simba wamchague
bwana aveva, na aliwatisha kuwa kama wasingemchagua aveva
basi angejitoa katika timu na asingetumia tena pesa zake kuisaidia
simba, kwa kifupi hans pope anajua mapungufu ya bwana aveva na
alijua wazi kabisa kama angeingia mtu mwingine madarakani zaidi ya aveva lengo lake lakuitawala simba akiwa nje ya nafasi ya rais
lisingewezekana.... Wanachama wengi wa simba wanafahamu msimamo wa bwana
wambura michael, siku zote wambura anataka kuiona klabu ya
simba ikisimama na kujitegemea yenyewe pasipo kumtegemea mtu,
wambura anajua matatizo ya kumtegemea mtu, na bahati mbaya
sana bwana hans pope hampendi michael wambura kwa sababu tu
hataki kuona simba inaendelea kutegemea na kuwanyenyekea watu kwa pesa zao shinikizo la kundi la ukawa kufutwa uanachama lilitoka kwa mzee
hans pope, na aliamini akina wambura na wenzake watapofutwa
uanachama basi kwake ingekuwa rahisi kufanya mambo yake vile
anavyotaka kama afanyavyo sasa kauli zake kuwa kocha phiri ana matatizo katika ufundishaji hans pope anashangaza wadau wa mpira duniani (1) tukumbuke phiri akuomba kazi ya kuja kufundisha simba bali
huyu huyu hans pope na kaburu ndiye walimwendea kocha phiri
kumuomba aje kuifundisha simba, na walifanya hivi wakidai kuwa
wanamfahamu kocha phiri na phiri naye anafahamu mila, desturi
na soka ya simba, leo hii iweje mzee hans pope aanze kumlaumu
kocha phiri kuwa anamatatizo katika ufundishaji wakati yeye mwenyewe alienda zambia kumuomba aje kuifundisha simba
kutokana na ubora wake ambao alikuwa anaufahamu? (2) kocha phiri huyu huyu ambaye mzee hans pope anasema
anamatatizo katika ufundishaji, ndiye aliweza kuweka record
yakuipa simba ubingwa wa tanzania pasipo kufungwa ata mechi
moja, na hiki ndicho kigezo kimojawapo kiliwafanya viongozi wa
simba wamrudishe tena kuinoa timu ya simba, iweje leo phiri
aonekane ufundishaji wake una matatizo? (3) hans pope huyu huyu ndiye alisimama kidete mpaka mfaransa
lewigy kufukuzwa kwa sababu tu kocha lewigy hakutaka
kuingiliwa kwenye programe yake yakutaka kuwatumia vijana
wadogo kwa maendeleo ya klabu ya simba (4) hans pope huyu huyu ndiye alisimamia tena mzee kibadeni na
julio kufukuzwa kazi simba baada ya timu kutofanya vizuri pasipo
kusikiliza utaalamu wa kocha ambapo nakumbuka mzee kibadeni
aliwaambia watu wa simba kuwa kwa kipindi kile wasitegemee
matokeo mazuri kwa sababu timu ilikuwa bado changa na inahitaji
muda wakukaa pamoja ikomae kimashindano, lakini mwisho wa siku kibadeni alifukuzwa (5) hans pope huyu huyu ndiye alisimamia kocha logarisic
kufukuzwa simba, na tukumbuke kuwa mara tu kocha logarisic
kuingia simba alisema kabisa timu haina wachezaji ambao
wanastahili kuichezea simba kwa sababu viwango vyao vidogo na
bado hawapo tayari kimashindano, lakini mwisho wake
alifukuzwa kazi kwa kusema ukweli (6) leo hii mzee hans pope ameanza choko choko tena zakutaka
kuandaa na kuhalalisha sababu zakumfukuza kocha phiri akisema
kuwa fundisha yake ina matatizo wakati ata report kocha kueleza
kwanini timu inatoa sare mfululizo hajaisoma...huku ni kumkosea
adabu kocha phiri na kuikosea adabu taaluma ya ukocha duniani ambalo wengi hawalifahamu (1) mfahamu kuwa kuanzia kocha lewigy mpaka leo hii, usajili wa
simba siku zote unafanywa na mzee hans pope pamoja na bwana
kaburu, hakuna kocha ata mmoja kati ya niliowataja hapo juu
wamewahi kusajili wachezaji kwa matakwa yao na maono yao
yakitaaluma, kama makocha wote hawa wamekuwa wakilalamika
juu ya ubora wa wachezaji maana yake nikuwa watu wanaohusika na usajili wanafanya usajili ambao uko below standard na siku
zote kitu ambacho kiko below standard hakiwezi kuleta positive
result, swali moja la msingi tunapaswa kuwauliza hans pope na bwana
kaburu, kwanini makocha wote hawa wanalalamikia juu ya ubora
wa wachezaji wanaosajiliwa na simba na wao wanaendelea tu
kusajili kwa utashi wao kwanini isifike wakati wawaachie
makocha wenyewe wasajili kulingana na utashi wa taaluma yao? Katika maswala ya ugavi na manunuzi kuna kitu kinaitwa, "money
for value and value for money" maana yake ni kwamba unapofanya manunuzi thamani ya pesa
lazima ionekane kwa kile ulichonunua, na kama thamani ya pesa
imeshindwa kuonekana kwa kile ulichonunua maana yake nikuwa
kuna uhuni, ujanja, au wizi umefanyika katika manunuzi husika swala la makocha wote kulalamikia ubora wa wachezaji na bado
viongozi hawa wanaendelea kusajili tu pasipo kuamua kuwaachia
makocha wenyewe wafanye usajili kulingana na taaluma zao
maana yake kuna uchafu unafanyika ambao wahusika wananufaika
nao simba ukawa ni kisingizio cha.upuuzi... ( onyo; usipuuzie habari za
simba ukawa kwa sababu wapo na wanafanya kazi kwa siri sana
they are very contravesial hawa watu kama freemason tu, ni
wasiri sana njia wanazotumia kuimaliza simba ) nasema simba ukawa ni kisingizio cha kipuuzi kwa sababu
wametengenezwa na akina hans pope wenyewe na wanaonekana
wana nguvu kwa sababu aveva, kaburu na hans pope
wameshindwa kutekeleza majukumu yao kwa klabu simba imeanza kufanya vibaya tokea kipindi cha kocha lewigy, swali la msingi tunapaswa kujiuliza je kipindi cha kocha lewigy
simba ukawa walikuwepo? Lakini pia tunapaswa kujiuliza ligi iliyopita simba ikishika nafasi
ya nne simba ukawa walikuwepo? Kinachokosekana sasa hivi katika simba ni weledi wa mpira tu,
wachezaji walipwe stahili zao, kamwe kuwafungia wachezaji kwa
kudai haki zao siyo njia ya kuisaidia simba leo hii unasema phiri hafai wakati phiri anafundisha wachezaji
ambao hakuna ata mmoja ambaye amesajiliwa simba kwa
mapendekezo yake wote amewakuta na hana uwezo wa kuwakataa,
atawakataaje wakati ndiyo aliowakuta? Na bahati mbaya zaidi wanamchagulia wachezaji wakucheza, huu ni
upuuzi mkubwa wa soka ambao sijawahi kuusikia popote duniani
zaidi ya tanzania hans pope soma alama za nyakati, kamwe hauwezi kupambana na
nguvu ya watu kiujanja ujanja kwa kuringia senti ambazo unazo,
simba ni tajiri zaidi ya unavyofikiri unaiona masikini kwa
kukupigia magoti kwa sababu tu bado haijapata viongozi wenye
vision..

Wacha tusubiri
 
Gentlemicyne, upo wapi,njoo huku uone hawa watu wanavyoiongelea simba yetuuuuu
 
Last edited by a moderator:
Chezea Hans Poppe wewe, mpaka mshuke daraja nasikia Hans Pope ni Yanga wa kufa mtu.
 
Back
Top Bottom