Anaandika Semeni Nyerere mwaka 2016

mkubhi

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
2,204
3,308
(Hii nimeikuta sehemu)

Anaandika Semeni Nyerere mwaka 2016

Kwamba;-

Ukisikia Rais Nyerere yuko sehemu kuongea na wananchi, wananchi walikuwa wanajawa na shauku,walikaa kando na redio zao, Hapo sasa inamwaga shule kuhusu historia ya taifa litokako, lilipo na dira linakoelekea, zinashushwa nadharia (theories) zilizojaa madini kuhusu maendeleo zenye mlengo wa kumkomboa mama Tanzania, alikuwa haishi utamu huyu mzee (R.I.P)

Mwinyi sijawahi kumfatilia (kwahiyo hata sijui alikua anasemaga nini, but juzi nimemsikia akisema taifa linaendeshwa kama gari bovu yani mkweche)

Mkapa hakuwa Mtu wa kuropoka hovyo sana, alikuwa Rais adimu ukisikia anaongea kuna kitu hasa mwisho wa mwezi, kila Mtanzania alikaa kando ya Luninga, watoto walikemewa wanyamaze Mfalme anaongea, alikuwa mtu makini, mtu wa kukemea, na aliamini katika uwekezaji kupitia wageni (ubinafsishaji) alilisimamia hilo na kama Tanzania si haba tulivuna kitu.... Nilisoma shule ya Mkapa O-Level.

Kikwete hakuwa na makuu, aliheshimu Uhuru wa mawazo. Alijitahidi kuutimiza yale yote ya msingi kwa rasilimali kidogo alizokua nazo. Kwa Mfano enzi zake Ajira mpya zilipatikana kila mwaka, posho na mishahara ya watumishi zilipanda kwa wakati muafaka, madawa hospitalini yalikuwepo, barabara zilijengwa, wanafunzi walipata mikopo etc. Pia aliheshimu utawala wa sheria na uhuru wa mawazo, ukisikia anaongea na wazee wa Dar kimbia ukasikilize anavyompa makavu live Tundu Lissu, Mhe.Mbowe au Dr.Slaa, ila wakikutana wanacheka na kukumbatiana. Kwenye siasa za vyama aliziweza fitna za majukwaani, lakini kwenye mambo ya kitaifa alikubali mawazo ya upinzani na aliweza kuwaita Ikulu wakamshauri.

Kikwete aliheshimu mchango wa Mataifa yaliyopiga hatua katika kumkwamua mama Tanzania, Nikiambiwa niseme maneno sita tu kuhusu Kikwete nitasema kwa herufu kubwa, TANZANIA YETU SOTE TWENDENI TUTAFIKA TARATIBU'

Huyu wa sasa hivi (JPM) hatuwezi kumpima maana bado ni mapema mno.

But aliwahi kuwepo Mwingine kabla ya Nyerere na wenzake, yeye alikuwa hana breki ya ulimi, husema ajisikiacho, ukisikia yuko sehemu tegemea aibu, utatamani kuzima TV yako la hasha usikilize huku ukiziba masikio na macho at some point. Kwenye misiba badala ya kuomboleza anataja orodha ya wake/waume za marehemu. Alijaa vitisho, Ghiriba na Lawama kila wakati na ahadi za Uongo uongo hata kwa mambo madogo yatekelezekayo, alijaa ubinafsi sana na kujiona kama mungu-mtu. Enzi zake ajira mpya hakuna, hakukua na nyongeza ya mishahara, watumishi hawakupanda madaraja, madawa hakuna, watu walikufa hata kwa kukosa chanjo ya tetenesi, mikopo kwa wanafunzi hakuna na zaidi ya yote taifa halikuwa na vipaumbele wala dira. Ilikua 'kanyanga twende super danger kanyaga twende' ni mixer mixer kachumbari, bamia na nyanya ntole humohumo. Huyo alikuwa Gavana wa Kijerumani kabla ya Uhuru wa Tanganyika, miaka ya 1960's.

Kwani we ulihisi ni nani?? . Tufanye kazi nchi yetu isonge mbele. Wakoloni hawakuwa watu wazuri.!
 
Back
Top Bottom