Baba Askofu Mwamakula: Rais Magufuli awe makini na wanafiki ndani ya Serikali yake

saidi kindole

JF-Expert Member
Sep 21, 2012
310
792
RAIS MAGUFULI AWE MAKINI NA WANAFIKI NDANI YA SERIKALI YAKE

Mwaka jana niliandika nikitahadharisha kuhusu viongozi wanaotoa sifa za kupindukia kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Katika kundi hili wamo baadhi ya Wabunge wa CCM, Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa na Mawaziri.

Hawa ndio watu waliotakiwa kumshauri, kumuelekeza na hata kumuonya Mheshimiwa Rais Magufuli ili kumsaidia kuongoza vizuri nchi. Watu hao wameacha maslahi mapana ya taifa na wanapigania maslahi binafsi. Kummwagia sifa Mheshimiwa Rais sio kuonyesha upendo kwake na wala sio uzalendo kwa nchi bali ni kutaka kujipendekeza kwake ili awateue au aendelee kuwaweka katika Serikali.

Katika juma lililopita tulimshuhudia Mheshimiwa Rais akimwambia aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Kangi Lugola kuwa pamoja na kumsifia sana lakini yeye Rais alifikia hatua ya kumkataa Mheshimiwa Lugola katika Baraza lake la Mawaziri. Hapo ndipo ikagundulika kwa wengi kuwa sifa zote ambazo Mheshimiwa Lugola alizokuwa akimmwagia Mheshimiwa Rais zilikuwa zimejaa unafiki na kujipendekeza!

Mheshimiwa Kangi Lugola ni ishara tu! Wapo viongozi wengine wengi katika maeneo niliyoyataja wanamwaga sifa kwa Rais hadharani ikiwa ni kichaka cha kufichia maovu yao. Huenda hao ndio wanafiki zaidi kumzidi hata Lugola! Wananchi wanawajua na huenda hata Mheshimiwa Rais ameshaanza kuwajua! Watu hawa wanafikiri kumwaga sifa kwa Rais na kudhibiti Wapinzani na hata kuwashughulikia wakosoaji wa Serikali itakuwa ni rushwa ya kumfanya Rais aendelee kuwabakiza. Inafaa waanze kujitathmini. Wawe ni watu wa kumshauri Rais kuliko kujivika majukumu ya kusifia ambayo hayapo kikatiba! Ni heri mtu akajiuzuru au hata akatumbuliwa kwa kutoa ushauri wenye tija kuliko kuondolewa kwa mambo ya aibu.

Hawa watu wanaomzunguka Rais kwa sifa za kupindukia wanaweza hata kufikia hatua ya kumchonganisha Rais na watu waadilifu. Kwa kujipendekeza kwao ndio wanaomshauri vibaya Rais kuhusu Wapinzani na wakosoaji ili waonekane kuwa wanamchukia Rais na Serikali.

Tunaendelea kumshauri Mheshimiwa Rais aendelee kuwatupia jicho baadhi ya Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa na Mawaziri ambao wanaimba nyimbo za kumsifia huku wakikosa kumwambia ukweli kuhusu hali halisi ya nchi. Asiwategemee watu wa namna hiyo kuijengea imani Serikali yake kwa wananchi.

Ukweli ni kuwa watu hao hufanikiwa kujenga chuki na hofu katika mioyo ya wananchi. Ni watu ambao wanachangia sana katika kuleta ubaguzi wa kisiasa katika nchi hii kwa sababu tu ya kujipendekeza. Kwao kuwaonea watu, na kuwasingizia na kuwabambikizia watu kesi za uongo na kutoa tathmini za uongo sio shida ili mradi wakiona hayo wanayofanya yatampendeza Rais ili aendelee kuwaamini.

Mheshimiwa Rais akiwagundua watu wa aina hiyo na akaogopa kuwatoa basi atakuwa anaasisi anguko lake mwenyewe! Tunamuomba Mheshimiwa Rais atafakari kwa kina hekima iliyomo katika Zaburi 101.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Aina ya serikali au viongozi kwa nchi zetu hizi za kiafrika huwa zina-reflect na uongozi uliopo juu,,kuna muda mwingine baadhi ya viongozi wanamsifia Rais hadi unaona AIBU mtazamaji sasa sijui tunatengeneza taifa la aina gani la watu wa kusifia tuuu bila weledi kutangulizwa.
 
UVCCM wakitoka kwenye vikao vyao watakuja na matusi na zile kauli zao za kuchanganya dini na siasa
 
MAKONKI YA UNAFIKI yapo Roman Catholic na bakwata hawa jamaa wanarudisha nyuma Sana,laiti kama hawa wachumia tumbo wangekuwa wanakemea maovu ya viongozi Leo hii Tanzania tungekuwa mbali...
Hawa malofa bakwata na Roman Catholic wakipata ujasiri kama wa KKKT hii nchi itatulia sana
 
Hivi inakuwaje mtu unasimama kumsifia sana kumbe yeye anakuchora tuu kuwa unajipendekeza? Maana kwa kauli take Rais kuhusu Kange ni kuwa anawajua wanao msifia sana na kwa nini wanamsifia.
Mtu kama Makonda, atajisikiaje anapomsifia sana Jiwe kisha ajue kuwa ananichora tuu na wananchi wananidharau tuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askofu wa matukio Kama chadema ilivyo Chama Cha matukio

Anasubibiri tukio ndio anatoa ewaraka ha ha ha
 
Back
Top Bottom