Ana mimba yangu lakini ndugu wameniambia nisimuoe kisa dini zetu tofauti

Mbona uke wake haukuhoji dini ya uume wako?
Inabidi watu tubadilike, mitazamo ya kuzuia wapendanao kuolewa kisa dini ni vigezo mfu.
Ikiwa dini iliwakuta babu zenu wanaishi pamoja leo wajukuu zao wanashindwa kuoana, sasa je dini imeimarisha upendo au imehatarisha upendo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawa pia suala la dini ni muhimu sana linapotokea suala la ndoa lakini hayo ni mambo yenu ninyi wawili kuyajadili na kufikia muafaka.
Ila we jamaa bado haupo tayari kuoa, yani ndugu wanachagua kwa ajili yako, ina maana hata ukioa bado watakuwa wakifanya maamuzi kwa ajili yako.
Wao wanapaswa kuwa washauri tu lakini si kukuchagulia cha kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, nipo njia panda nahitaji ushauri wa ziada.

Me ni muislam mwenzangu kristo lakini ndg wamesema nisimuoe kisa dini zetu ni tofauti na wamesema nikitaka kumuoa basi mahari nijilipie mwenyewe.

Nilijaribu kuhoji wameniambia wengi walioa wakiristo hawakufika popote kimaendeleo na kimahusiano yani mahusino yanakua hayaeleweki pia ukiangalia huyu binti anamimba yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina imani una pesa ya mahari, fanya muoane. Mpaka mlipofikia inaonesha mnapendana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom