Ana mimba yangu lakini ndugu wameniambia nisimuoe kisa dini zetu tofauti

Mlundilwa Jr

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
2,863
4,231
Habari wakuu
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, nipo njia panda nahitaji ushauri wa ziada.

Me ni muislam mwenzangu kristo lakini ndg wamesema nisimuoe kisa dini zetu ni tofauti na wamesema nikitaka kumuoa basi mahari nijilipie mwenyewe.

Nilijaribu kuhoji wameniambia wengi walioa wakiristo hawakufika popote kimaendeleo na kimahusiano yani mahusino yanakua hayaeleweki pia ukiangalia huyu binti anamimba yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unashindwa nini kujilipia mahari mwenyewe kama mimba ulimpa mwenyewe

Mimba umpe wewe then usimuoe, unataka mwenzio awe singo maza

Kuna ndoa za bomani, kuna kuweka makubaliano baina yenu na maisha yakaendelea tu
 
Huna akili ndugu anakupangiaje mtu wa kumuoa au kutomuoa? Maamuzi Fanya mwenyewe ili ukikosea au kupatia ujadipongeza au kujilaumu wewe,
 
Sasa unashindwa nini kujilipia mahari mwenyewe kama mimba ulimpa mwenyewe

Mimba umpe wewe then usimuoe, unataka mwenzio awe singo maza

Kuna ndoa za bomani, kuna kuweka makubaliano baina yenu na maisha yakaendelea tu
Cna mkuu mahari ila ninapo pakujiegesha kwani babu kanipa chamba kimoja naishi buree na ajira bado sina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani anayeoa ni wewe au ndugu zako mkuu?
Wewe ndo unayemjua mtu unayetaka kumuoa, ukiskiliza sana ya ndugu wataingilia uhuru wako hata kwenye mambo ya msingi
 
Eti wanasema kuoa mkirsto kwao nimwiko na familia yake haieleweki hizo nimoja ya 7bu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Waambie ndugu zako waache ubaguzi wa dini, wasichijifanye wao waujua Uislam kuliko waarabu waliouanzisha, Maamuzi yote yapo chini yako na vilevile usibebedhambi ya kumzalisha mtu na kisha ukamuacha imagine angekuwa dada yako ndo anafanyiwa hivyo
 
Cna mkuu mahari ila ninapo pakujiegesha kwani babu kanipa chamba kimoja naishi buree na ajira bado sina.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tafuta kazi/ajira/jiajiri uhame hapo uwe na uhuru wako, Kwahiyo hiyo mimba mlipeana wapi? Hapo kwa babu mwisho wa siku utapangiwa hadi styles za kufanya na mkeo.. jiongeze usikae kiboya

Wanawake tunahuruma sana‍♀️🤦‍♀️
 
wazungu na waarabu wametuharibu sana na hizi dini zao... kwani Adam na Hawa walikuwa dini gani?

usiowane naye sasa lakini usiachane naye pia....

Subiri mwaka mmoja upite kisha jiulize swali hili hili uone jibu lake ni lipi,ukiona unaendelea kushindwa kupata majibu kama sasa vuta subira tena mwaka mwingine na kama hali ni hiyo hiyo vuta miaka miwili zaidi kisha jiulize swali hilo hilo....

Hapa utapata kitu tofauti...
 
Kabla ya dini na imani, kuna wewe kwanza...... Sasa huyo wewe ndie umepata mwenza imekuwaje umeleta tena dini kabla ya kuimarisha upendo....?!

Dini zingekuwa ni kila kitu then maostaadh na wainjirist wasingekuwa na matatizo katika ndoa zao ila sisi ni wanadamu.... Dini kazi yake ni kutuimarisha katika kufanya matendo mema.....

Imani ni kitu binafsi...... Sio jambo la watu wengi...... Kunawatu wengi wanakwenda kanisani na misikitini ila hawana imani napo sababu ya matendo yao.

So kitu muhimu ni kuwa makini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, nipo njia panda nahitaji ushauri wa ziada.

Me ni muislam mwenzangu kristo lakini ndg wamesema nisimuoe kisa dini zetu ni tofauti na wamesema nikitaka kumuoa basi mahari nijilipie mwenyewe.

Nilijaribu kuhoji wameniambia wengi walioa wakiristo hawakufika popote kimaendeleo na kimahusiano yani mahusino yanakua hayaeleweki pia ukiangalia huyu binti anamimba yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati unastarehe naye uliwaomba ushauri ndugu zako kabla ya tendo ??????????????
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom