Ana maana gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ana maana gani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by VUTA-NKUVUTE, May 31, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Wana-JF,nikiri kuwa ni mara yangu ya kwanza kuandika kwenye jukwaa hili.Suala hili linamhusu rafiki yangu wa karibu aitwaye Eddock.Eddock alikuwa na mahusiano na msichana mmoja hapa jijini Dar es Salaam.Mahusiano yao ya kimapenzi yalidumu kwa miaka miwili;2010-2012(mnamo mwezi Aprili).

  Nilivyokuwa nawaona,walikuwa wanawezana(naogopa kusema walikuwa wanapendana).Msichana wa Eddock alikuwa na mipango ya kusoma.Walitaarifiana.Wakakubaliana.

  Ghafla bin vuu,Eddock akapokea simu ya msichana wake akimuomba wakutane ili waongee kuhusu suala moja muhimu kwao.Wakakutana.Msichana bila kusita akamwambia Eddock kuwa ameamua kuachana naye Eddock.Sababu zikaulizwa.Msichana akasisitiza kuwa ameshaamua na hana sababu zozote.Akamtaka Eddock atafute mchumba aoe ili amsahau kabisa kuwa waliwahi kuwa pamoja.

  Eddock akakubali matokeo.Akaendelea na zake.Siku si nyingi,akapokea simu ya yule msichana akiomba amkopeshe laki moja.Akamkopesha.Halafu,msichana akaanza tabia ya kupiga simu mara kwa mara,kubeep,kusms na kumtafuta hata kwa rafiki zake Eddock ili amwone.Tabia hizo ndizo zimetawala hadi leo.

  Sasa waungwana,kwa wanaoweza kutafsiri matendo haya,huyu msichana anamaanisha nini hasa?
   
 2. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Anamanisha kua rafiki yako ni BUZI tuu hana hadhi yakuanae .
   
 3. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 560
  Trophy Points: 280
  Umeona tatizo eh? Binti alipata mtu mwingine anayeyaweza na wmwenye hela lakini akakosa utu. Alipomjaribu jamaa yako akamkopesha bila shida (naamini hivyo). NAFSI inamsuta anataka kurudisha majeshi.

  Kwa sababu hawakugombana, afanye "COST BENEFIT ANALYSIS" halafu aamue kuwa warudiane au la, Ingawa kwangu DEMU hana mapenzi ya dhati au hana msimamo.

  Bazazi ni Bazazi.
   
 4. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Pesa mbele mapenzi kapuni
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145

  Huyo binti anaitwa NATAKA SITAKI! Nahisi alikuwa anajaribu kupima maji kwa kuintroduce issue ya kuachana ili aone nini kitatokea na bahati nzuri au mbaya huyo jamaa akaamua kufanya kweli na sasa anatafuta namna ya kurudi.

  Kama jamaa yako Eddock anaweza kufanya uchunguzi wa mara baada ya kuachana huyo binyi alikuwa na nani na kama ataprove kuwa hakuwa na mtu baada ya kuachana then amsamehe tu na kuendelea naye. But akigundua kuwa baada ya kumwagana, huyo binti alipata mtu mwingine, maana yake ni kuwa huyo binti ana tabia za tamaa na hafai kuwa mke na pia huwezi kujua huko alikokimbilia kalikoroga nini mpaka atake kurudi tena.
   
 6. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu,nitafikisha ujumbe kama ulivyo.Pamoja sana...
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  in love life second chances always come with doubts...
  hakuna sababu ya kurudiana hapo kama anaweza kumsaidia kama rafiki aendelee tu kufanya hivyo...
  maana wasichana wanakula kwa mabuzi wanalala kwa wapenzi
   
 8. peoples power

  peoples power JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 468
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  kaka kama ni wewe bora kuwa muwazi wana jamvi tutakupa maakili ya kufanyaga na huyo mdada kwa kifupi ni kwamba huyo bi dada hafai hata kwa kachumbali.
   
Loading...