Amwunguza wifi yake sehemu za siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amwunguza wifi yake sehemu za siri

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mungi, Jun 8, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Thursday, 07 June 2012 20:11[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  digg

  Pamela Chilongola
  KATIKA hali ya kushangaza na kusikitisha,mkazi wa moshi bar Manispaa ya Ilala,amedaiwa kumuunguza wifi yake( 15) sehemu zake za siri na kumsababishia maumivu makali.

  Hayo yametokea jana Jijini Dar es Salaam, baada ya askari polisi wa kituo cha Stakishari, kupokea taarifa kutoka kwa majirani juu ya unyama huo aliofanyiwa binti huyo.

  Polisi hao mara baada ya kupata taarifa hiyo, walifika nyumbani kwa mtuhumiwa lakini iliwachukua zaidi ya saa mbili kufanikiwa kumtoa ndani mtuhumiwa ambaye alidaiwa kujifungia.

  Hata hivyo, hali ilikuwa tete baada ya wakazi na majirani wa eneo hilo walioguswa na tukio , walipoamua kuvamia nyumba hiyo baada ya kupokea taarifa za uongo kuwa mtuhumiwa hayupo na kuamua kuwashinikiza polisi wamtoe au wajichukulie sheria mkononi.

  Kufuatia mvutano huo, Polisi waliofika kumchukua mtuhumiwa , walizidiwa na kuamua kuondoka kwa lengo la kwenda kuongeza nguvu kwa kuongeza askari na mabomu ya kurusha ili kuweza kuwatanya wananchi waliokuwa na hasira.

  Licha ya kuongeza askari, haikuwa kazi rahisi kuwatawanya mpaka walipoamua kupiga risasi hewani na kufanikiwa kuwatawanya wakazi hao waliokuwa na hasira sambamba na kumtoa mtuhumiwa aliyekuwa amejificha juu ya dari ya nyumba.

  Mtoto aliyefanyiwa unyama huo alisema, Mei 30, alilazimishwa kunywa maji ambayo yamechanganywa na vipande vya glasi huku akiwa anapigwa na waya wa umeme.

  Alisema siku iliyofuata Mei 31, alipigwa na mama huyo na baadaye kuingizwa kipande cha mti sehemu za haja kubwa ambacho alikaa nacho kwa saa mbili na baadaye mama huyo alimtoa.
  “Nilikunywa maji yaliyochanganywa na vipande vya chupa ya bilauli huku nikiwa napigwa ambavyo vinaniletea matatizo ya tumbo ambapo nimepata choo siku moja hadi leo hii sijapata tena ambacho kilikuwa na damu nyingi”alisema

  Juni 1, mwaka huu majira ya saa 8 mchana mtoto huyo ndiyo alichomwa moto katika sehemu zake za siri, huku akiwa amefungwa mikono na miguu kwenye dirisha.

  Alisema siku hiyo alianza kumpiga kwa saa moja na baadaye alimkamata na kumfunga kamba kwenye miguu na mikono huku akichukua moto na kumuunguza sehemu zake hizo za siri na kumsababishia maumivu makali.

  “Nilivuliwa nguo zote na alinifunga kamba huku akichukua moto na kuniweka sehemu zangu zote za siri ambapo kwa sasa nashindwa kwenda haja kubwa na ndogo.

  Jirani Aziza Saidi alisema, Juni 2, mwaka huu walimuona mtoto huyo akielekea dukani huku akiwa amepanua miguu yake ndipo walipomwita na kumuuliza na aliwajibu kuwa ameunguzwa na moto sehemu zake za mwili.

  Alisema walimwita ma kumwangalia sehemu zake na kukuta zimeharibika ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa dada yake ili amchukue.

  Mtuhumiwa huyo katika utetezi wake alisema, hawezi kufanya vitendo kwa wifi yake na anajua uchungu wa kuzaa kwa sababu yeye ni mama wa watoto wawili.

  Mtoto huyo alipelekwa katika hospitali ya Amana kwa uchunguzi zaidi.

  source: mwananchi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mama zetu mbona mna roho mbaya hivi?
   
 3. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  This is too much. This Barbaric woman deserves to be banished forever
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Nani katoa access ya private parts za wifi?
   
 5. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hakika huu ni unyama usiovumilika!! Anastahili adhabu stahiki ikiwa atagundulika na hatia.
   
 6. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ee mungu ndie uliyeniumba nisaidie sijawahi mfanyia mtu yyte ubaya na nisikae nimfanyie .ROHO YANGU INASIKITIKA SANA KUONA WATU WANATESWA HIVI JAMANI,WANAUME KAENI CHONJO NA WAKE ZENU KIDOGO KIDOGO ZUNGUMZENI NA NDUGU ZENU MNAOISHI NAO HASA HUKU MJINI DU WANATESWA MAWIFI SIO WATU SISI SOMETIME.NAKUMBUKA NILIMNASUA MWAKA HUU TU DADA MMJA ALIKUWA ANAMTESA MTOTO WA KAKA YAKE ,ALIKUWA ANAMPIGA HASA USIKU ANAMTUMA DUKANI YANIALIKUWA ANAMTESA SNA NIKAMWAMBIA UNA NAMBA YA MTU YYTE AKANIPA YA DADA YAKE NIKAMPIGIA AKAJA KUCHUKULIWA ALIKUWA KAMA KICHAA.DU.
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Yaani kuna wanawake wengine hapa duniani wana roho za kishetani
  Ningekuwa eneo la tukio ningehakikisha namchapa makofi huyo mwanamke kwa hasira ninayosikia hapa ...
   
 8. Miss-Thang

  Miss-Thang JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Mhh jamani duniani kuna watu wana roho mbaya hivi. Mtoto wa mwenzio kumfanyia unyama kama huu jamani kwa kosa gani alilokufanyia. Huyu mama si mzima kabisaaa, haiwezekani mtu kuwa mnyama kiasi hiki. Uhhh inaniuma na simjui huyo binti, sasa mama yake na ndugu zake je! Na huyo kaka yake yu wapi jamani mkewe akimnfanyia unyama huu dada yake?:sad:
  Inabidi wamfanyie angalau kitu kimoja alichomfanyia huyo binti aone utamu wake...:angry:
   
 9. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Tatizo la habari hii haikukamilika. Hakuna hata kidokezo cha sababu ambazo huyo mtesaji zinaweza kuwa zimemfanya kufanya unyama huo usiomithilika. Si kwamba zitaeleweka. Lakini zitatusaidia kuzidi kuipima akili yake. Yuko aliyepondaponda miguu ya mke kwa kucheleweshewa ugali! Kwa kifupi tu, anahitaji kufanyiwa uchambuzi wa akili ili ama afikishwe mahakamani mara moja (akithibitika mzima) au atue Mirembe moja kwa moja. Manake hawezi kuwa mzima mtu wa aina hii.

  Halafu, binti huyo naye ni ngangari; unywe maji yenye vipande vya chupa bado uwepo na uwe na uwezo wa kusimama na kuongea?
   
 10. M

  MaMkubwa1 Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  UKICHAA si lazima kuokota makopo na kuhangaika barabarani tu! Ukichaa una aina nyingi tofauti tofauti. Alimradi kitendo alichokifanya mama huyu sio cha kawaida na ni cha kumdhuru kijana mdogo kwa kutumia 'adhabu' aliyoitumia, inaonyesha dhahiri kwamba ni mgonjwa wa akili na wote wanaoishi nae hawako salama! Huyo mume na watoto wake atakuja kuwafanyia vitendo vibaya na vya kikatili siku moja. Ni wa kupelekwa hospitali kwa wataalam wa kichwa
   
Loading...