Ketoka
JF-Expert Member
- Sep 23, 2015
- 1,121
- 1,983
- Jamaa mmoja nchini Zimbabwe alingia hospitalini hadi katika wadi ya wanawake na kulala na mkewe aliyelazwa humo
- Mwanamke huyo alieleza kuwa hangeweza kumkataza maana mumewe huyo angemjeruhi
Mmiliki wa hospitali moja ya kifahari nchini Zimbabwe anaendelea kuhojiwa baada ya ripoti kutokea kuwa aliingia katika wadi ya kina mama hospitali mwendo wa 3am na kufanya mapenzi na mkewe aliyelazwa humo.
Jamaa huyo alifanya kitendo hicho hadharini mbele ya wagonjwa wengine kumi ambao pia walikuwa wakiendelea na matibabu.
Mwanamke huyo alieleza kuwa hangeweza kumkataza maana mumewe huyo angemjeruhi.
Kabla kuingia humo, inadaiwa kuwa jamaa huyo alizozana na wauguzi wa hospitali hiyo waliomkataza kuingia ndani alipodai anataka kumuona mkewe.
Kisa hicho kilithibitishwa na mkurugenzi wa matibabu hospitalini humo Amedeus Shamu ambaye alieleza kuwa uchunguzi unaendelea kubainisha ukweli.
''Ilikuwa mwendo wa 3am ambapo baadhi ya wagonjwa katika wadi hiyo walipiga ripoti kwa wauguzi kuwa kuna watu waliokuwa wakifanya tendo la ndoa katika wadi hiyo. Wauguzi hao waliwaarifu maaskari wa hospitali waliomtoa jamaa huyo upesi,’’ alisema.
Alipohojiwa na wauguzi, mwanamke huyo alieleza kuwa hangeweza kumzuia mumewe kufanya tendo hilo maana angempiga.
''Singekataa kufanya mapenzi naye maana ningepigwa mbele ya wagonjwa, maana yeye hupenda vita sana,’’ mwanamke huyo alisema.