Amuua mkewe kisa kuchati kwenye simu na mchepuko

Amuua mkewe kisa kuchati kwenye simu na mchepuko

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,603
Reaction score
22,716
Jeshi la polisi Mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Salum Mzee Kondo (38),fundi ujenzi mkazi wa Kidongo Chekundu, Bagamoyo aliyehusika na tukio la mauaji ya mkewe, Mwajuma Omary (27) kisha kutoroka baada ya kutenda kosa hilo.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa septemba 2 mwaka huu Yombo Buza jijini Dar es salaam ambako alikimbilia baada ya kufanya kitendo hicho Agost 31,2018, saa 9 alasiri nyumbani kwao Kidongo Chekundu.

Akiweka bayana kuhusiana na tukio hilo kwa waandishi wa habari ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema, mtuhumiwa alipokamatwa alikiri kutenda kosa hilo ,na kudai alichukua hatua hiyo kutokana na wivu wa kimapenzi.

Alieleza kwamba, mkewe alikuwa akichat na simu huku akiwa anacheka mwenyewe ndipo alipoamua kumnyang’anya simu na kukuta message alizokuwa akichat na mwanaume mwingine. “Jambo hilo lilisababisha mgogoro kati yao ,ambao ulisuluhishwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Magomeni B, lakini marehemu alishikilia kuchoshwa kuishi na mumewe huyo na kuomba kupewa talaka na mumewe aligoma kutoa talaka ” alifafanua Nyigesa.

Pamoja na hilo ,Nyigesa alisema wawili hao walikuwa na mgogoro mwingine, uliotokana na mtuhumiwa kuchukua ATM Card ya marehemu mkewe na kwenda kutoa sh.50,000 bila ridhaa yake.
 
Jirani yangu NJILE njoo uone hii kitu.
Unamdharau mumeo kisa siku hizi ana sukari na pressure jogooo hapandi mtungi kwa sana.
Tumeshakuonya tabia yako ya kuchat na wanaume hata mbele ya mumeo hadi juzi mumeo kakunyang'anya simu akafuta contacts zako zote.
Njileeee Njileeee I wish ungekuwa unaijua JF ungepita hapa usome hii kitu, na wewe ungejirekebisha. Acha dharau kwa mumeo na kuendekeza wanaume wa nje tena hadharani.
Ulimtengea mumeo chakula bila kijiko, anakwambia kijiko kiko wapi wewe hata husikii unachat tu hapo dinning, hadi akachukia akaenda zake chumbani, baadae ndio unastuka, "hivi baba fulani yuko wapi?", mbona hajala, mdogo wako" akakuambia si amekuomba kijiko muda mrefu weee unachat tu...."
 
Tunawalaumu wazungu na ndoa zao za mikataba lakini kumbe waliona mbali,
 
Back
Top Bottom