Amuua mke kisa wivu wa kimapenzi

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,268
7,779
Leo jumatatu ya tarehe 23/12/2019 mwanaume mmoja amejikuta mikononi mwa polisi kwa kosa la kumuua mke wake kwa kumpiga na shoka kichwani.

Mwanaume huyo ameishi na mke huyo kwa miaka zaidi ya mitano na wanamtoto mmoja. Kisa kipo hivi:

Jamaa alikuwa akiishi na mkewe katikati ya mji. Kuna mtu mwenye hela alinunua eneo lao na kufanya wao kuhamia pembezoni mwa mji.

Kutokana na hela kuwa nyingi(za kiwanja) jamaa alianza kuwa mtu wa totozi na baadae kumtimua mke wake.

Mke alianza kupambana kivyake katika biashara ndogo ndogo, kusaidia mafundi kujenga n.k. mwezi October akapata mfadhiri(mwanaume) ambae akampa mtaji akafungua mgahawa mashambani.

Jamaa aliposikia kuwa mkewe aliyemuacha yupo na jamaa mwingine ameenda na kufanya maamuzi magumu.

Baadhi taarifa kama majina, mahali walipo, umri n.k vimeondolewa ili kutokuharibu upelelezi wa kipolisi maana mazishi ni kesho. So wiki moja baada ya mazishi Uzi utaeditiwa ukiwa kamili.
 
Kwenye journalism kuna 5Ws +H(What,where,when,who,why na How)so jitahidi kujibu ata3 ya hizi kwenye taarifa yako especially what,Who na where..
 
Siku hizi sio magunia tena ni shoka Haya sasa akavae zile nguo zetu za orange bila kusahau adhabu ya kuamka alfajiri mapema kufanyishwa mazoezi kilazima bila kusahau bakuli letu pendwa la uji umejaa kama wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee! Tulianza na vipigo heavy, tukaja kwenye visu, tukaja kwenye mapanga, tukasogea kwenye magunia ya mkaa, tukatumia risasi za kichwani!

Sasa ni mwendo wa mashoka!
Sijui kifuatacho kitakuwa nini?

Yaani Ibirisi ametukamatia kwenye mapenzi siku hizi. Wanaume siku hizi hatutaki suluhu! Tukizinguana tu tunaona halali ya mwanamke ni kumtanguliza mbele ya haki!

Mungu atusaidie sana airekebishe mioyo ya wanaume wote Tz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye journalism kuna 5Ws +H(What,where,when,who,why na How)so jitahidi kujibu ata3 ya hizi kwenye taarifa yako especially what,Who na where..
Nangezea hapa.

Sio kwa Journqlism tuu, katila mfumo wowote wa taarifa muhimu sana 5w and H alafu malizia na SO WHAT.

Hapo taarifa inakua na mjalizo.
 
Aisee! Tulianza na vipigo heavy, tukaja kwenye visu, tukaja kwenye mapanga, tukasogea kwenye magunia ya mkaa, tukatumia risasi za kichwani!

Sasa ni mwendo wa mashoka!
Sijui kifuatacho kitakuwa nini?

Yaani Ibirisi ametukamatia kwenye mapenzi siku hizi. Wanaume siku hizi hatutaki suluhu! Tukizinguana tu tunaona halali ya mwanamke ni kumtanguliza mbele ya haki!

Mungu atusaidie sana airekebishe mioyo ya wanaume wote Tz.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah kwakwel aisee ila Haya mambo nilijua yataisha lakini ukikaa miezi kadhaa linaibuka tukio lengine

Daah huko kupenda kwengine ni kwa ajabu sana yaan unakua na wivu mpaka kutoa roho ya mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom