RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja Jackson Andungulile, Mkazi wa Kijiji cha Ibililo Wilayani Rungwe kwa tuhuma za kumuua Baba yake mzazi kwa mapanga na kumjeruhi Mama yake mzazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Justus Kamugisha, amesema kijana huyo ametekeleza mauaji hayo akidai kuwa wazazi wake hao ni wachawi.
Amesema katika mahojiano na kijana huyo, amekiri kutekeleza mauaji hayo na kudai kuwa lengo lake lilikuwa ni kuwauawa wote wawili kwa kuwa wanashirikiana kumloga.
Kamanda Kamugisha ameeleza kuwa hali ya mama huyo ambae amejeruhiwa na kijana huyo ni mbaya sana na yupo katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya uangalizi na matibabu zaidi.
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara tu baada ya mahojiano kukamilika kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.