Amshukuru Rais Samia kwa kugharamia matibabu ya mtoto wake

Amshukuru Rais Samia kwa kugharamia matibabu ya mtoto wake

Joined
Apr 15, 2025
Posts
91
Reaction score
174
Mkazi wa Dar es Salaam, Simon Bryson amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugharamia matibabu ya mtoto wake Nilsa Simon kufuatia ombi lake kupitia mitandao ya kijamii mtoto wake asaidiwe matibabu .

Bw. Simon ametoa shukurani hizo leo Januari 13, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Taasisi ya MOI ambako mtoto wake anaendelea na matibabu.

“Ninamshukuru sana Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa upendo na utu... Bila msaada wa serikali, isingekuwa rahisi kumpatia mtoto wangu matibabu haya ya kibingwa. Mwenyezi Mungu ambariki Rais wetu na aendelee kuwasaidia Watanzania wenye uhitaji.” amesema Bw. Simon

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema Serikali imeendelea kuonyesha dhamira ya dhati katika kusaidia wananchi, hususani wenye changamoto za kiafya zinazohitaji matibabu ya gharama kubwa.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia imeweka kipaumbele katika afya za wananchi. Tumeendelea kupokea wagonjwa wengi wanaosaidiwa kupitia mifumo mbalimbali ya serikali, jambo linaloonesha dhamira ya kweli ya kuwahudumia Watanzania,” amesema Dkt. Mpoki.

Naye Dkt. Hamis Shabani, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo wa MOI, amewataka wanawake kuchukua tahadhari mapema kabla ya ujauzito ili kuepuka matatizo ya kiafya kwa watoto wachanga.

“Tunawasihi wanawake wote walio kwenye umri wa kuzaa kunywa madini ya folic acid kabla na wakati wa ujauzito. Hii husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia watoto kuzaliwa na matatizo kama kichwa kikubwa na mgongo wazi,” amesema Dkt. Shabani
IMG-20260113-WA0102.jpg
IMG-20260113-WA0082.jpg
IMG-20260113-WA0083.jpg
 
Pole kwao M'Mungu azidi kumsimamia mtoto wao.

Hapo Changamoto iliyopo ni ukosefu wa elimu kuhusu unywaji wa hizo Folic Acid, sababu sidhani kama wale wanawake huko vijijini na wengine hata huku mijini wanajua kuwa wakishajijua ni wajawazito mapema tu waanze kunywa hizo folic acid.

Wengi wanazianza wakianza clinic baada ya miezi mitatu ambapo inakuwa si muda sahihi.
 
Back
Top Bottom