John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 111
- 215
Amri 10 za Mungu ni Nini
Amri za Mungu ni nini
Amri za Mungu ni orodha ya amri kuu 10 za Mungu katika Biblia.
Za kwanza nne zinamhusu Mwenyezi Mungu mwenyewe, na zile zinazofuata mpaka mwisho zinahusu jirani, yaani binadamu wengine kuanzia wazazi.
Amri hizo zimeoneshwa katika kitabu cha Kutoka 20:1-17.
Amri hizo pia zimeoneshwa katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:7-21.
Yesu anasema " Mkinipenda, mtazishika amri zangu" …. "Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake" (Yohana 14:15; Yohana 14:21).
Yohana anasema: katika ulimwengu huu watakatifu ni wale wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu...tena anaongeza kuwa wana heri (wamebarikiwa) wazishikao Amri za Mungu, wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake (Ufunuo 14:12, 22:14).
Amri 10 za Mungu katika kitabu cha Kutoka 20:2-17:
1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu
mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
3. Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
4. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
5. Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
6. Usiue.
7. Usizini.
8. Usiibe.
9. Usimshuhudie jirani yako uongo.
10. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Hizo ndizo Amri 10 za Mungu.
Mathayo 5:19: "Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni".
1Yohana 2:4: "Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake".
1Yohana 5:3: "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito".
Mhubiri 12:13: "Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu".