Amplifaya ya Clouds FM

Amplifaya ya Clouds FM

Mkenye Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
218
Reaction score
402
Kwa miaka ya hivi karibuni kipindi cha Amplifaya kinachorushwa na Clouds Fm kuanzia jumatatu hadi ijumaa saa kumi hadi kumi na mbili jioni, kikiendeshwa na Millard Ayo na Frida Amani; kimekuwa kipindi kinachogusia mada mbalimbali kuhusiana na maisha yetu ya kila siku pamoja na desturi zetu kama Watanzania.

Kama mdau umejifunza mambo gani kutokana na hicho kipindi na ungependa waboreshe nini ili kipindi kiwe bora zaidi.
 
Nimesikiliza sana Clouds FM kipindi niko chuo. Saivi kwakweli hata sijuagi nini kinaendelea huko
 
Nipo Vihingo huku Kisarawe. Clouds hatishiki. Embu niambie ni mada gani huwa zinajadiliwa
 
Nimejifunza matangazo ya biashara sio Lazima yawe katika form ya jingles Ila upate watu wa kuyaelezea kwa mbwembwe.Kifupi ni kipindi Cha matangazo.
 
Sisikilizi radio,sitizami Tv,maisha yanabadilika,

Nilikuwa napenda cloud fm,
 
Kuna watu bado mnackiliza iyo station.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Clouds na Sasa h
Kwa miaka ya hivi karibuni kipindi cha Amplifaya kinachorushwa na Clouds Fm kuanzia jumatatu hadi ijumaa saa kumi hadi kumi na mbili jioni, kikiendeshwa na Millard Ayo na Frida Amani; kimekuwa kipindi kinachogusia mada mbalimbali kuhusiana na maisha yetu ya kila siku pamoja na desturi zetu kama Watanzania.

Kama mdau umejifunza mambo gani kutokana na hicho kipindi na ungependa waboreshe nini ili kipindi kiwe bora zaidi.
ata efm haishiki hapa nilipo nimekasirishwa sana na hili jambo clouds ni mpaka nikwee mtini,efm inakoroma TU
 
Nimejifunza matangazo ya biashara sio Lazima yawe katika form ya jingles Ila upate watu wa kuyaelezea kwa mbwembwe.Kifupi ni kipindi Cha matangazo.
Matangazo ni mengi kuliko muda wa kipindi chenyewe
 
Back
Top Bottom