GE2025 Amos Makalla: Wanachama 4,109 wamechukua Fomu za Ubunge CCM, Bara na Zanzibar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, amesema jumla ya wanachama 4,109 wamechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao kupitia chama hicho.

Akizungumza leo akiwa Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Makala amesema:

"Kwa takwimu za haraka, waliochukua fomu katika majimbo yote kwa maana ya Tanzania Bara wako 3,585 na Zanzibar 524. Kwa hiyo, katika majimbo tu, wanachama walioonyesha nia wako 4,109, na tuna majimbo 272."

We mzee unajichosha tu, ni hivi hakuma UCHAGUZI October bila Reforms.
 
Bado za Udiwani Tsh 50,000 kwa kila fomu!

Inawezekana wakapata hata Tsh 2.6 Bilioni!Kweli haya ni mapato makubwa sana kwa Chama cha Mapinduzi kwa wakati mmoja!Bado hawajalamba ruzuku!

Unaweza kuwashinda CCM kweli kwa style hii?
 
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, amesema jumla ya wanachama 4,109 wamechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao kupitia chama hicho.

Akizungumza leo akiwa Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Makala amesema:

"Kwa takwimu za haraka, waliochukua fomu katika majimbo yote kwa maana ya Tanzania Bara wako 3,585 na Zanzibar 524. Kwa hiyo, katika majimbo tu, wanachama walioonyesha nia wako 4,109, na tuna majimbo 272."

Mbna kwa Zanzibar nimeona waliochukua fomu ni 2000+ au sikuelewa.
 
Mwaka 2020 walikuwa 10,000 leo mapato yameshuka
 
Back
Top Bottom