Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uchaguzi hauwezi kusogezwa mbele kwani wamejipanga kushiriki uchaguzi na hawawezi kuwa sehemu ya kuvunja katiba, hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wajipange 2030.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kilosa na Mikumi katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro akimalizia ziara yake ya siku saba iliyokatishwa kupisha maembolezo ya Mzee Cleopa Msuya.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Makalla amesema hakuna jambo la dharura wala vita la kufanya uchaguzi uhairishwe na wala nchi haipo kwenye vita wala jambo lolote la kutisha kusema uchaguzi ushindwe kufanyika.
Amesema CCM ni chama kinachoheshimu demokrasia na hawapo tayari kuvunja katiba na kwakuwa wenye Chadema hawashiriki uchaguzi wasubiri 2030.