DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limeishutumu vikali serikali ya Uganda kwa kuendesha kile ilichokiita kampeni ya ukandamizaji wa kisiasa dhidi ya upinzani, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 15.
Amnesty imesema kuwa vikosi vya usalama vya Uganda vimekuwa vikitekeleza ukamataji wa kiholela, mateso, vipigo na matumizi ya gesi ya kutoa machozi dhidi ya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani, National Unity Platform (NUP), kinachoongozwa na msanii na mwanasiasa Bobi Wine.
Kwa mujibu wa shirika hilo, lengo la hatua hizo ni kuwatisha wapinzani, kuvunja mikutano ya kisiasa na kuzima kabisa sauti za upinzani, hali inayotishia misingi ya demokrasia na haki za binadamu nchini humo. Amnesty imesema imekusanya ushahidi wa kutosha unaowaunganisha moja kwa moja maafisa wa usalama wa serikali katika vitendo hivyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mazingira ya sasa yanaashiria uchaguzi unaoendeshwa chini ya hofu, vitisho na nguvu za dola, jambo linalozua wasiwasi mkubwa ndani na nje ya Uganda.