Amkata bosi wake kiganja cha mkono kisa deni la shilingi 65,000

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Moja kwa Moja kwenye mada.

Kijana mmja aliyejulikana kwa jina la Baraka Alphone Mkazi wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe anashikikiwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kumkata Kiganja Cha Mkono Boss Wake kisa Deni la sh.65,000.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe,Kijana huyo aliingia kwenye mzozo na boss wake akidai malipo hayo baada ya kumlimia shamba boss wake huyo kwa kutumia ng'ombe..

Mabosi muwe mnawalipa wafanyakazi wenu kwa wakati,nao Ni binadamu Wana mahitaji Kama nyie.👇

---

Baraka Alphonce (20), Mkazi wa Ludewa Kijijini Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumkata kiganja cha mkono wa kushoto Boss wake aliyekuwa akimdai Tsh Elfu 65 alizolima kwa kutumia ng’ombe.

Kwa mujibu wa Patrick Mdege (35) aliyejeruhiwa na Mtuhumiwa huyo anasema Kijana huyo alikuwa ni Mfanyakazi wake lakini amemgeuka na kumkata kiganja chake mara baada ya kutokea ugomvi baina yao.

“Alikuwa amefanya kibarua kwa Mtu cha kulima kwa kutumia ng’ombe wangu wanaotumika kulimia, aliyemlimia akaja kusema ile hela imetoka na Mimi nilimzuia asimpe ile hela bila Mimi kuwepo, nilipomfuata yule Dogo akaanza kunitukana nikamwambia Dogo uwe na busara nimekulea kwa muda mrefu nikampiga kofi kumbe kwenye jembe la ng’ombe kulikuwa na panga akachomoa sasa Mimi ile ni panchi likafika mkononi”

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema kiganja hicho kilianguka ardhini na kuokotwa wakati majeruhi akikimbiakimbia, na alipofikishwa Hospitali kiganja hakikuweza kuunganishwa lakini hata hivyo Mtuhumiwa yuko mikononi mwa Polisi akisubiri kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kiganja.PNG
 
Back
Top Bottom