Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 260
- 707
Habari za Viumbe wenzangu, poleni kwa kadhia mbalimbali. Wale mnaoteswa na mapenzi, siasa na uchumi, tambueni ya kuwa hamko peke yenu.
Naomba nianze na swali. Unafikiria picha aina maana yoyote katika maisha yako? Kiimani au hata kisaikolojia?
Unafikiri rangi ya Watu inayotumiwa kumchora Mwokozi wako au Mungu wako haijalishi na aina maana yoyote?
Huu ni mtihani wako.
Em jaribu hili zoezi dogo, funga macho yako kwa sekunde 10. Fikiria kuwa Yesu ni mtu mweusi au fikiria kuwa sura ya Yesu ni tofauti na picha ambazo umeziona maishani mwako.
Tayari ee? Jaribu na hili
Funga macho yako, na fikiria malaika weusi wamekuja kwako. Aidha kwa ndoto au wamekutokea mahala popote
Fikiria malaika Michael, Gabriel na wengine ni weusi.
Umejaribu?
Umeonaje? (nijibu kwenye koment)
Kuwa mwaminifu, usidanganye.
Hili ni jaribio la kisaikolojia.
Hivyo ndivyo akili yako ilivyopangwa na
Kutengenezwa kupitia picha.
Mchungaji mmoja aliwahi kuniambia jinsi shetani alivyomjia kwenye ndoto kama malaika wenye ngozi nyeusi na akamkemea, kwasababu alisema malaika lazima wawe Wazungu

.......Inaumiza sana.......
Kwa mfano malaika wakiwatokea, malaika wakiwa na rangi nyeusi za Kiafrika kama nyie wenyewe, nina hakika wengi wenu mtafunga, kuomba na kuwakemea mkidhani ni wachawi ama mashetani.
Nadanganya? Nikiwaita watumwa nitakuwa nakosea?
Yesu, malaika na manabii wote kuchorwa Katika rangi ya mkoloni haikuwa jambo la bahati mbaya, walifanya hivyo kwa makusudi ili waweze kuzitawala Akili zetu. Kwasababu Akili ya mwanadamu inaifadhi kila kitu Katika picha.
Baadhi ya Wakristo wa Kiafrika husema haijalishi Yesu ana rangi gani, lakini ndani yao wanafurahia kuwa yesu ni mzungu na ndio maana wasomi husema, mkristo mzuri ni MTUMWA mzuri wa Wazungu.
Lakini ngoja tusema haijalishi yesu ana rangi gani.
Sawa!
Ebu jaribu kuchora rangi ya Yesu na malaika weusi kwenye tisheti zenu, vitenge vyenu na kente zenu alafu uone jinsi Wakristo wenzako kutoka jamii zingine watakavyo kushanga, na kwa unyonge watawakubali kama wewe ulivyofanya bila kujua.
Akili hufanya kazi kupitia picha. wewe kwa ufahamu au kwa kutokufahamu upendo wa Yesu mweupe umekufanya kuwapenda wazungu wanao fanana na Yesu.
Waafrika tuna takiwa kukubali kwamba tumechezewa akili zetu, na Sasa ni wakati wa kuanza kujikomboa na kuzijenga upya Akili zetu ziwe timamu.
Wenye kunipinga nipingeni watakaokubaliana na mimi sawa lakini kauli yangu ni moja tu
Amka Mwafrika